Mgonjwa wa Mwisho wa Maafa ya Arusha Atoka Hospitalini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgonjwa wa Mwisho wa Maafa ya Arusha Atoka Hospitalini.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Arusha Mambo, Feb 15, 2011.

 1. Arusha Mambo

  Arusha Mambo Senior Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  IMG_2884.jpg
  Na Arusha Mambo.

  Mgonjwa wa mwisho wa maafa ya maandamano ya kisiasa yaliyofanyika Arusha na kusababisha vifo vya Watanzania wawili na Mkenya Mmoja ameruhusiwa leo kutoka hospitalini.

  Muhanga huyo Ally John Ogaga (mwenye kidonda mguuni) amekishukuru Chama cha Chadema, wananchi wa Jimbo la Arusha, Mbunge na wadau mbalimbali waliojitolea kuwasaidia wahanga wa maafa hayo.

  Mwenyekiti wa Chama cha Chadema Mkoa wa Arusha Bw. Samson Mwigamba (hayupo pichani) amesema madhara aliyoyapata muhanga huyo yanatokana na matumizi mabaya ya vyombo vya dola.

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Arusha Bw, Elifuraha Paul Mtowe (mwenye suti nyeusi) amesema Taasisi hiyo imetoa kiasi cha Shilingi Milioni Mbili na Laki Mbili kugharamaia matibabu ya muhanga huyo ambaye alikuwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Selianai Arusha.

  Katibu wa Chadema Mkoa wa Arusha Bw Amani Golugwa (aliyevaa suruali nyeupe na koti jeusi) wakati wa tukio hilo amesema Chama cha Chadema kwa kushirikiana na ArDF wataendelea kufuatilia matibabu yalisosalia kwa mgonjwa huyo mpaka kidonda chake likichosababishwa na kupigwa risasi mbili za mguu kipone.

  Ally mkazi wa Moshono ambaye anafanya biashara ya Madini akizungumza katika tukio hilo amesema alipigwa risasi akiwa maeneo ya Hospitali ya St. Thomas na askari aliyempiga risasa alinyanganya kiasi cha Shilingi Milioni Mbili na Laki Saba alizokuwa nazo.

  Ameliomba Jeshi la Polisi kumsaidia kuzipata fedha hizo ambazo zilikuwa ni mtaji wake wa biashara na Serekali iwachukulie hatua watu wote waliohusika na maafa hayo ikiwa ni pamoja na wale wanaoendelea kuficha idadi kamili ya vifo vilivyotokea.
   
Loading...