BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,097
Date::8/12/2008
Mgonjwa wa akili aua wenzake wodini Muhimbili, ajeruhi watano
Na Waandishi Wetu
Mwananchi
IMANI ya watu wengi kwamba hospitalini ni mahali pa kukimbilia kuokoa maisha kwa mgonjwa, imeshindikana kuthibitika baada ya mgonjwa wa akili kuwashambulia wenzake saba wodini na kuua wawili kati yao.
Tukio hilo la kuhuzunisha na la kwanza kutokea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), lilitokea usiku wa kuamkia juzi baada ya mgonjwa wa akili, David Denge (21) aliyelazwa katika wodi ya wagonjwa kuwashambulia wenzake wakiwa wamelala usingizini.
Habari ambazo zimethibitishwa na Mkurugenzi Mkuu wa MNH, Profesa Leonard Lema pamoja na polisi, Denge anadaiwa kucharuka usiku na kuwashambulia wenzake kwa kuwaponda kichwani kwa chuma cha kuwekea maji ya dripu.
Profesa Lema alisema kuwa tukio hilo lilitokea juzi saa 1:30 usiku katika wodi ya wagonjwa wa akili.
Alisema Denge aliyekuwa katika hospitali hiyo tangu Julai 28 mwaka huu, alikuwa katika wodi ya wagonjwa wa akili waliopitiliza walioko chini ya uangalizi maalum.
Kwa mujibu wa Profesa Lema, mgonjwa huyo aliamka ghafla kutoka usingizini na kuchukua chuma wanachowekea wagonjwa maji ya dripu na kuwaponda wenzake.
"Polisi walijulishwa tukio hilo jana (juzi), walifika Muhimbili na wanaendelea na uchunguzi wao. Pia uongozi wa hospitali umewasiliana na viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa hatua zaidi," alisema Profesa Lema.
Alisema wagonjwa wawili walifariki dunia kwa kuumia vibaya kichwani huku wengine wanne wakipelekwa chumba cha upasuaji na hali ya wagonjwa wawili kati ya hao wanne sio nzuri.
Profesa Lema alisema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea kubaini sababu za tukio hilo na kujua endapo kulikuwa na uzembe kwa upande wa wauguzi katika kuwaangalia wagonjwa.
''Kinachoonekana katika suala hili ni kwamba mgonjwa huyo hakupewa dawa mapema kwani dawa wanazotumia zinawafanya wakose nguvu za kufanya fujo,'' chanzo cha habari kilidokeza.
Habari zingine zinasema hospitali ya Muhimbili pia ina tatizo la dawa za wagonjwa wa akili na upungufu wa madaktari na wauguzi.
Katika hatua nyingine, Jeshi la polisi nchini limesema kuwa lina wasiwasi kuwa muuaji wa wagojwa wawili katika wodi ya vichaa Muhimbili alizinduka mapema na kuwaua wenzake wakati wakiwa usingizini.
Wagonjwa wa aina hiyo, huchomwa sindano za usingizi ili walale na polisi ilisema kuwa huenda muuaji alizinduka mapema baada ya dawa walizochomwa kuisha nguvu na kufanya mauaji hayo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Aibula Tanda, alitaja waliouawa na Denge ambaye ni mchoma mkaa wa Kongowe ni Paul Maganga (30) na Abdallah Abeid (20).
Tanda alisema kwa mujibu wa muuguzi wa daraja la pili wa wodi hiyo, Kokumula Severine (26), muuaji huyo alitumia chuma kinachotumika kama stedi dripu na kuwashambulia wagonjwa wenzake wakiwa wamelala.
Kwa kuwa wagonjwa hao huchomwa sindano yenye dawa ili kupunguza makali yao, tunasadiki kuwa dawa aliyochomwa muuaji iliisha nguvu mapema na ndipo alipoamka na kuwashambulia wenzake na wawili kati ya tisa wamefariki na wengine ni majeruhi, alifafanua Tanda.
Alisema tukio hilo ni la kusikitisha kwa kuwa wagonjwa hao, walikuwa wamelala wakati muuaji akiwashambulia.
Kamanda Tanda aliwataja wagonjwa wengine, Hamis Mohammed (41), Athuman Abdallah (23), Peter Joseph (Milanzi) na Maurice Oyala (20) ambao walijeruhiwa vibaya maeneo ya kichwani na kulazwa katika hospitali hiyo na kwamba hali zao si nzuri.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Muhimbili, mgonjwa Jumbe Said amepata majeraha ya kawaida na anaendelea vizuri wakati mgonjwa Bela Mosha hakushambuliwa kabisa, alisema Kamanda Tanda.
Aliongeza kuwa muuaji amekamatwa na polisi na anatarajiwa kufikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma zinazomkabili.
'' Kwa sheria lazima afikishwe mahakamani na wataalamu watampima ili kuchunguza mgonjwa huyo wa akili alipata wapi nguvu za kufanya matukio hayo wakati wenzake walikuwa wamelala,'' alisema Tanda.
Hili ni tukio la kwanza kutokea katika hospitali hiyo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1956, hivyo kutoa changamoto kwa uongozi kuweka mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo katika siku za usoni.
Habari hii imeandaliwa na Kuruthum Ahmed, Jackson Odoyo na Festo Polea