Mgonjwa wa akili ailiyeua wenzake kortini tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgonjwa wa akili ailiyeua wenzake kortini tena

Discussion in 'Matangazo madogo' started by Pdidy, Aug 28, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Aug 28, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Mgonjwa wa akili ailiyeua wenzake kortini tena
  Na Pauline Richard

  MGONJWA wa akili, David Denge (21), ambaye anadaiwa kuua watu wawili na kujeruhi wengine wanne ambao walikuwa wanapatiwa matibabu katika wodi ya wagonjwa wa akili Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jana amefikishwa kwa mara nyingine katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam ambako kesi yake imetajwa kwa mara ya pili.


  Mtuhumiwa huyo alifikishwa katika mahakama hiyo saa 2.45 asubuhi akiwa kwenye gari la mahabusu aina ya Isuzu yenye namba STK4310 huku akiwa chini ya ulinzi wa askari magereza.


  Mgonjwa huyo, alipelekwa katika gereza la keko ambako anaishi ili upelelezi wa kesi hiyo ukamilike.


  Mara baada ya kufikishwa katika mahakama hiyo, mshitakiwa aliteremshwa ndani ya gari hilo huku akiwa amefungwa pingu na kupelekwa moja kwa moja kwa Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Joyce Minde .


  Mtuhumiwa huyo alivaa shati la rangi ya kahawia na suruali yenye michirizi meusi na alionekana kuwa mpole na kutetemeka kana kwamba alikuwa anajisikia baridi, tofauti na mara ya kwanza alipofikishwa katika mahakama hiyo.


  Awali wakati anafikishwa katika mahakama hiyo, Denge alionekana kuwa msumbufu kwa askari waliokuwa wanamlinda.


  Baada ya kutajwa kwa kesi yake ya mauaji inayomkabili, Mwendesha mashitaka mkuu wa Polisi Naima Msangi aliiomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo kwa madai kuwa upelelezi haujakamilika.


  Mahakama iliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10, mwaka huu itakapotajwa tena, mtuhumiwa amerudishwa mahabusu na upelelezi wa kesi yake unaendelea.


  Baada ya tarehe hiyo kutajwa, alirudishwa ndani ya gari akiwa mnyonge na kutulia kwenye kiti alichokuwa amekaa mpaka gari hilo, lilipoondoka eneo la, mahakama saa 3.15 ili kumrudisha mtuhumiwa huyo katika gereza la Keko


  Mwananchi lilishuhudia mtuhumiwa huyo akiwa amekaa kiti cha mbele karibu na dereva wa gari hilo akiwa ametulia, huku akiwa anaongea sauti ya chini na kutetemeka hali ambayo haikuwa rahisi kubaini alikuwa anaongea nini.


  Muda mfupi baada ya mtuhumiwa huyo kurudishwa gereza la keko, watu wengi walimiminika mahakamani hapo kwa ajili ya kumuona Denge.


  Awali ilidaiwa katika mahakama hiyo kuwa Agosti 11, mwaka huu, saa 1.45 usiku mtuhumiwa huyo, alidaiwa kumuua Paulo Maganga na Abdukadir Abed ambao walikuwa wanapatiwa matibabu katika wodi ya wagonjwa wa akili Muhimbili.


  Mtuhumiwa huyo kwa mara ya kwanza alifikishwa mahakamani hapo Agosti 13 mwaka huu na alisomewa shitaka hilo la mauaji mbele ya Hakimu Samel Maweda wa mahakama hiyo.


  Siku ya kwanza mtuhumiwa huyo mara baada ya Mwendesha mashitaka Mkuu Naima Msangi kumsomea shitaka hakutakiwa kujibu lolote, lakini cha kushangaza mshitakiwa huyo, alimjibu akisema,'' Ushindwe kwa jina la Yesu''.
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Refer to the Penal Code Cap 16 R.E 2002 Section 13 whereby a person will not be liable for an act if his mind is affected by disease at the time of commiting the offence that he was incapable of understanding the nature of the crime,incapable of appreciating that he ought not to do the act or omission and does not have control of the act or omission.
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  The M'Naghten Rule provides as follows: "Every man is to be presumed to be sane, and ... that to establish a defense on the ground of insanity, it must be clearly proved that, at the time of the committing of the act, the party accused was laboring under such a defect of reason, from disease of mind, and not to know the nature and quality of the act he was doing; or if he did know it, that he did not know he was doing what was wrong.

  Upon being taken to jury accused of murder they have to prove his mens rea (evil mind) and actus reus (evil act) but in this case there was an evil act but the evil mind was not there as the act itself of him being admitted on a psychiatric ward proves that he was insane and there is no need of proving his insanity, therefore he will not be liable of murder but manslaughter and the punishment for his act is to admit him on a psychiatric ward which will be nonsense that is taking him out of the ward and return him to the same place it will be a circle of which is undefined to be done with reasonable people. I think it is nonsense to bring the man to court.
   
 4. Sam GM

  Sam GM JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 536
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hapa inaonekana huyu mgonjwa ndio very sane na hakimu pamoja na waziri aliyeunda tume ya kuchunguza hii isshu kuwa insane. Hii case ina defense ya insanity haina haja hata ya kwenda mahakamani.
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Aug 28, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mama mia , sijafahamu lengo lako la kuweka habari hii katika ukumbi wa matangazo madogo dogo. Je hili ni tangazo ama habari, naomba unifahamishe...
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Wajameni. Nampongeza mama mia kuweka hii habari hapa ili kuonyesha jinsi ambavyo serikali yetu inatumia fedha kulipa tu kamati zisizo na tija. Pia kutumia muda wa hakimu na wanasheria wa serikali kwa kesi kama hizi badala ya kuushughulikia kesi zenye tija na maslahi kwa taifa. Kevo ameelezea vizuri sana jambo hili kwenye hii post. Kibunango nenda hapo juu soma post za kevo. Any way, labda ni kuwaridhisha ndugu wa wafiwa au kuona kweli kama kulikuwa na uzembe ulifanywa na manesi/madaktari lakini ukweli ni kwamba amefanya kosa out of his mind (Kichaa). Ndiyo maana tunaambiwa tuwe makini sana unapokutana na kichaa hasa kama ata damage hata property yako ni kesi ambayo kwako ni kuachana nayo tu. Ila tu kama wewe una akili timamu let say unaendesha ukamgonga akaumia au akafa, my friend unahesabiwa tu Criminal case kwa kuwa umekuwa na akili timamu wakati kosa linatendeka. Hata hivyo, kama watagundua manesi wa zamu/dakari alikuwa mzembe unafikiri kuna hatua zitachukuliwa? Another, government failure. Thanks.
   
Loading...