Mgonjwa hazuiwi tiba, tuache kuwabeza waloenda Loliondo kupata kikombe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgonjwa hazuiwi tiba, tuache kuwabeza waloenda Loliondo kupata kikombe.

Discussion in 'JF Doctor' started by Tutor B, Jan 16, 2012.

 1. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #1
  Jan 16, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Mgonjwa hazuiwi tiba, tuache kuwabeza waloenda Loliondo kupata kikombe. Ona hii; habari ya kweli! Sikuwa nikijua kuwa nina madonda ya tumbo, ila nilikuwa nikisumbuliwa na matatizo ambayo ndo zilikuwa dalili za madonda ya tumbo. Siku moja nikazidiwa na kuamua kwenda kupima, majibu nilopewa hayakuwa tofauti na hisia zangu – nilikuwa na Acers. Nilijaribu tiba za hospitali zikawa zinapoza tu, kwa kweli niliteseka sana. Siku moja nikiwa nyumbani nimetandikiwa mkeka nje – nagalagala na maumivu makali kama vile tumbo linawaka moto; alipita babu mmoja akasimama akinishangaa kwa namna nilivyokuwa nikiteseka. Alinijulia khali – nikamjibu; baadaye akaniomba maji ya kunywa. Nilitoa sauti kumuita binti wangu alete maji ya kunywa na binti alifanya kama nilivyomwamulu.
  Babu yule alipomaliza kunywa maji alinishukuru na kuniuliza nasumbuliwa na nini. Nilimjibu kuwa nasumbuliwa na madonda ya tumbo. Babu alinipa pole na aliniuliza ni tangu lini. Nilimjibu kuwa ni kipindi cha miaka kama mitatu tangu nimetambua tatizo hilo. Alinambia kuwa yeye anajua dawa lakini anaishi mbali na mji ule nilikokuwa naishi. (Ilikuwa ni wilaya tofauti na nilipokuwa naishi). Nilimuuliza njia ipi naweza kutumia ili niweze kupata hiyo dawa. Babu Yule alinambia nimpatie pesa kwa ajili ya safari ya kurudi mjini kuniletea dawa na alinambia nikipona ndo nitamlipa. Kwa namna nilivyokuwa nimeteseka na hali hiyo sikuwa na pingamizi lolote kwa ushauri alonipa. Nilimpatia pesa mara mbili ya kiasi alichonitajia nikiamini kwamba anaweza kuja mjini kuniletea dawa akakuta nimeishakata kauli akashindwa kurudi kwake. Babu yule alikataa na kuchukua kiasi alohitaji tu kama nauli. Baada ya siku tatu; babu yule alikuja na dawa kwenye kopo, alinikuta niko ndani nimelala. Niliamshwa na mke wangu akiwa na mshangao mkubwa kuniona naingia katika tiba za vibabu. Nilijikongoja na kuja sebuleni kumsalimia mgeni hiyo. Baada ya maongezi kidogo, yule babu alinisogelea na kunionyesha kopo lenye dawa, alitumbikiza vidole vyake viwili na kuchukua kiasi cha dawa na kuweka mdomoni kwake. Alitafuna kwa muda na kasha kumeza – baada ya hapo alinambia hivi “Nimeamua kula mimi kwanza ili usije ukawa na wasiwasi kwamba nakupatia sumu; nikaondoka ukaitupa” Aliniamuru nami nichukue na kutafuta hiyo dawa. Aliomba nauli ya kurudi nami nilimwamuru mama watoto ampatie kiasi fulani cha fedha. Niliitumia hiyo dawa kwa muda wa wiki moja ikawa imeisha na katika kipindi hicho matatizo yote niliyokuwa nayo yalipotea kabisa. Kosa nililokuwa nimefanya ni kutokumdadisi kijiji alichokuwa anaishi (nilijua wilaya tu). Marafiki zangu waliokuwa wakijua kuwa nasumbuliwa na ugonjwa huo walishangaa sana kuona narudi katika hali ya kawaida nikiwa natumia vyakula vyote pasipo kubagua. Wale waliokuwa na tatizo hilo waliniomba niwambie wapi nilipata dawa – nilishindwa kuwajibu kwa kuwa sikujua babu alikuwa akipatikana wapi. Kwa sababu ya shida niliyokuwa nayo sikuuliza hata babu yule aliitwa nani, aliishi kijiji gani, sikuuliza hata gharama iwapo nitapona kwa kuwa sikuamini kama nitapona ila nilikuwa najaribu tu. Hivyo ndugu zangu tusiwalaumu walopata kikombe kwa babu – tulaumu chanzo cha malazi tu. Baada ya siku kadhaa nilifanikiwa kukutana na babu huyo mjini, nilimsalimia na kumkumbusha huduma alonipatia hadi nikapona. Alinambia kuwa alikuwa na uhakika na hakutaka malipo yoyote tofauti na kuniomba siku moja aje na mjukuu wake kwangu wanitembelee. Tulipanga siku ya kuja kunitembelea na nilimpatia pesa kiasi cha kumuwezesha kusafiri yeye na mjukuu wake kuja mjini kunitembelea. NIlimwomba aje na dawa kiasi kwa ajili ya dharula ikitokea tatizo likajitokeza tena – naye alinikubalia. Siku ya siku Babu yule alikuja kunitembelea akiwa na mjukuu wake. Familia yangu, babu na mjukuu wake tulifungua urafiki mpya wa kifamilia. Nafahamu kwake vizuri na mjukuu wake amekuwa akitumika kuleta dawa pale inapohitajika. Angalizo alinipa ni kwamba yeye hafanyi biashara ya dawa kwa sababu hata yeye alionyeshwa bule na wazazi wake. Marafiki zangu walokuwa wakisumbuliwa na tatizo la acers walipata huduma hiyo na wanaendelea vizuri. Ni zaidi ya watu hamsini ninaowafahamu walotumia dawa hiyo wakapona kabisa na mimi nikiwemo. TIBA ZA ASILI ZIPO NA ZINAFANYA KAZI YA KUOKOA MAISHA YA BINADAMU – TUSIZIBEZE!
  Nina mifano mingi mno kuhusiana na huduma ya tiba za asili.
  MNASEMAJE WANAJAMII FORUM
   
Loading...