Mgonjwa Afariki hospitali Sinza Palestina kwa kukosa dripu ya MAJI

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,850
Wakati serikali ikipambana kuboresha muhimbili, Mgonjwa amefariki hospitali ya Palestina Sinza, kwa kukosa dripu ya maji.
===============

Bwana Chesco Athmani amepoteza maisha katika hospitani ya Palestina Sinza, Dar es Salaam kufuatia hospitali hiyo kukosa maji ya kuongezea wagonjwa.

Ndugu wa marehemu wamemlalamikia daktari wa zamu kwa kushindwa kumpa huduma mgonjwa wao na kuwajibu vibaya.
 
RIP...
serikali iweke mfumo endelevu watu waishi kwa mifumo mizuri...hii
kushitukiza kila siku inasaidia ila watu hawabadiliki/.....
 
Wakati serekali ikipambana kuboresha muhimbili,Mgonjwa amefariki hospital ya palestina sinza kwa hospital hiyo kukosa dripu ya maji.
Source ITV
Haiwezi kuwa habari ya kweli!
Chombo cha habari chapaswa kubalance taarifa ndio kirushe kwa wananchi!
Wanaweza kuongeza tension kati ya watoa huduma na wagonjwa maana mtu anaweza kufikiri kuwa mtu ameuliwa makusudi!
Je, maji ndio yalikuwa tiba ya msingi kwa ugonjwa wake? Je kama mgonjwa huyo angepewa maji angepona Ila kwa kunyimwa ndio amekufa?
Zipo tabia za vijihospital vya private kulazimisha dripu na ndio maana kila mtu akifika tu hospital unadhani anatakiwa awekewe maji!
 
Mgonjwa amekosa maji aina gani? Normal saline? Dextrose? Hartmam? Au maji ya uchumgu? Nashauri Mwiteni Majaliwa aje kufurahisha watu kwa kutangaza kuwa katumbua majipu
 
Wanakufa wengi mkuu.......kuna siku nimekwenda hosp mgonjwa anahitajika drip.nikaambiwa hakuna lakini chakushangaza nilipotoa hela ikatolewa kwenye kabati...... hizi ndio hosp zetu
 
Mja mzito.....
Hao ndugu waliambiwa maji hakuna hospital
Kama kweli walimpenda ndugu yao kwa dhati wangechanga apatiwe maji yaliyohitajika kesi baadaye. Siyo kila kitu kulazimisha upatiwe wakati hakipo. Kuna watu wanapenda sana ligi isiyo Na tija. Acheni kuwatuhumu watenda kazi Wa afya bila sababu ya msingi nao wanachoka na kuishiwa vitendea kazi.
 
Back
Top Bottom