pappilon
JF-Expert Member
- Jan 27, 2015
- 3,192
- 3,556
Wana jukwaa habarini za jioni.
Mimi ni mgeni kabisa katika hili jukwaa la sheria na limefika hapa baada ya kutatizwa na hii kitu inayojulikana kama mgongano wa kimaslahi au conflict of interest kwa kimombo. Naomba niende kwenye mada moja kwa moja.
Kuna makubaliano ya uchimbaji wa Madini ya Dhahabu nataka kuingia na Jamaa Fulani hivi, basi katika mkataba huo wakaweka sehemu ya mgongano wa kimaslahi. Katika vipengele vyake kikawepo kimoja ambacho ndo kinanyima Amani Kabisa. Kinasema "Mbia Namba moja (ambaye ndo Mimi) hataruhusiwa kuchimba Dhahabu katika eneo la masumbe au kuwa na hisa ya uchimbaji na mtu yoyote katika eneo hili, pia hatatakiwa kuchimba wala kuwekeza katika uchimbaji katika Wilaya ya KAHAMA kwa kipindi chote cha mkataba huu". Jambo la kusikitisha sana ni kwamba hawataki niwe Mwanachama katika maduara yao ila nina gawio la 10% katika faida itakayopatikana kutokana na uchimbaji tunaofanya.
Sasa wakuu kitu ninachoomba kujua Kutoka kwa wanasheri, je hii kitu ya conflict of interest inatambuliwa na sheria Zetu? Na je application yake inakuweje? Je hiki hawa Jamaa zangu wanachong'ang'ania kibakubalika kisheria?
Kuna Jamaa yangu lawyer nimeongea Naye akaniambia inatakiwa tu ku-declare kwao kuwa nafanya pia Biashara inayofanana na Biashara tunayotaka Kufanya pamoja na si vinginevyo, Je hii ni kweli wakuu Wangu.
Naomba mnisaidie nguli wa sheria maana naona kama mkataba huu unaenda kunifunga pingu kwenye utafutaji Wangu maana shughuli zangu nyingi zinahusisha uchimbaji wa Dhahabu hasa hasa Kanda ya Ziwa.
Naomba msaada wenu wakuu
Kama hii mada ilishawai kuja hapa jukwaani basi naomba radhi kwa kuirudia ila nisaidieni tu wakuu
Jioni njema.