Mgongano wa kimaslahi CCM

DaveSave

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
440
634
Kwa makusudi tu, niliwachokoza wana CCM wa kijiweni kwetu.
Niliwaambia sera ya viwanda ni ndoto na anayebisha atoe maelezo ya kisayansi – we, kidogo wanile nyama! Wote 15 wakasimama wakitaka kunifafanulia.

Kabla ya kuanza nikapendekeza kuwa, ili kuepusha maoni yenye mgongano wa kimaslahi, watumishi wa serikali wasishiriki huu mdahalo. Jamaa wawili, watatu wakakaa chini.
Halafu nikapendekeza kuwa, yeyote aliyewahi kuuziwa nyumba ya serikali asishiriki pia. Wote wakakubali kuwa, mtu aliyebahatisha nyumba kwa bei poa hawezi kuwa na mawazo huru kwenye huu mjadala. Wawili wakakaa chini.

Tulikuwa tayari kuanza, ila pia nikaomba. Makada wanaotegemea kugombea nyadhifa mbalimbali za kisiasa kupitia CCM wasishirki. Hapo baadhi walitaka kupinga lakini nilipowafafanulia kuwa ni vigumu kwa mtu kupinga sera ya chama chake na asiitwe msaliti, wote wakakubaliana na mimi halafu wote wakakaa chini na mdahalo wetu ukaisha!
Gayo
 
Back
Top Bottom