Mgongano wa Katiba na Majukumu: Katiba ya Tanzania na Katiba ya CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgongano wa Katiba na Majukumu: Katiba ya Tanzania na Katiba ya CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Sep 9, 2009.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kinachoingoza Tanzania ni nini? Je ni Katibaya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au Katiba za Vyama vya Siasa na hasa Chama Tawala CCM?

  Je Watanzania waliopewa majukumu na dhamana ya kuingoza Serikali yetu, utii wao ni kwa Chama cha Siasa walicho na mapenzi yao au Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inayotoa mwongozo na mamlaka yote waliyonayo?

  Imebidi kufikia hapa na kujiuliza swali hili na ni lazima tuzichambue katiba hizi, ili tujue mipaka ipo wapi, mapungufu yapo wapi, Utata uko wapi na ni nani mwenye Mamlaka na Haki kudai na kutenda kazi kwa mujibu wa Mwongozo upi?

  Kwa kuwa Vyama vya Upinzani; CHADEMA, UDP, TLP, NCCR, CUF na wengne bado hawajaonja Utamu wa Madaraka na Utawala, nitaangalia mwingiliano wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ile ya CCM.

  Kifupi, katika hili, hakuna la kipi kilitangulia, ama kuku au yai, kilichotangulia na chenye Mamaka ya juu ni Katiba ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na si Katiba ya CCM au Ilani ya CCM hata kama CCM ndio chama Tawala na kimepewa dhamana na mamlaka ya kuongoza Tanzania.

  Ila, jinsi Katiba hizi zilivyoundwa, na makusudi mazima yanayoonekana kama uzao wa makusudi au upungufu, Katiba ya Tanzania na watendaji wa Serikali ya Tanzania, huelekea kumezwa na kulazimishwa kufanya mambo kutokana na Katiba za Vyama vya Kisiasa.

  Kwa mujibu wa Marekebisho ya Katiba ya Tanzania ya mwaka 1992, Utawala wa Chama Kimoja na Chama hicho kujumuishwa ndani ya Katiba ulikoma. Lakini, Udhaifu wa Sheria hii na Katiba ni Upendeleo maalum, uliopewa CCM kwa kuruhusiwa kuendelea na shughuli zake kama Chama bila kupita Usajili na masharti kama vyama vingine vilivyopaswa.

  Sheria ya kuunda vyama vingi inasema na kueleza haya katika Kipengele cha nne
  Halafu Katiba ya Tanzania inasema hivi
  Sehemu ya nne ya Katiba ya Jamhuri inasema wazi ni nani mwenye Mamlaka

  Sehemu ya 8 ya Katiba inazungumza kwa uwazi kuhusu yafuatayo (mkazo ni wangu)

  Kisha ile sehemu ninayoipenda kuliko zote hufuata katika kipengele cha 27 cha Katiba ya Jamhui
  Nikiruka sehemu zingine na kwenda kwenye Urais, Katiba ya Tanzania inasema hivi kuhusu Urais na Mamlaka ya Serikali ya Jamhuri wa Muungano
  Katiba ya Tanzania inasema hivi kuhusu kiti cha Urais kuwa wazi na Uchaguzi wa Urais
  Sifa za mtu kuchaguliwa kuwa Rais ni
  Sasa nikihamia kwenye Katiba ya CCM ya mwaka 2007, nitaanza mkutano mkuu katika vipengele hivi

  NEC baadhi ya majukumu yake ni haya
  Hivyo mtaona mkorogano ulioko ndani ya Katiba ya nchi ambao hutoa nguvu na mamlaka kwa Serikali, lakini CCM nayo ina ubavu wake na nguvu ambazo zinaweza kuleta mgongano na katiba ya Jamhuri hasa la mwanachama wa CCM kuvuliwa uanachama baada ya NEC kuamua.

  Kilichotokea Dodoma majuzi, je walengwa walikuwa ni Sitta na "Wapiganaji" wenzake, au walioleta vitisho hivi vya kutimuana Uanachama walikuwa wakipima Upepo ili kujua kama malengo yao ya Mapinduzi bila kumwaga damu yanaweza kufanikiwa bila kushirikisha ngazi na hatua za Kiserikali?
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuna haja haraka sana ya kudai katiba mpya ambayo itakuwa accontability kwa watu na sio watawala, hata leo haya matatizo ya mambo mengi katika Tanzania hakuna katiba imara, ndio maana hata hawa CCM wanasema kuwa kama CCM ikiwa watatoka madarakani eti Amani itatoweka, Kama kweli kuna katiba basi itakuwa imara siku zote.
   
 3. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #3
  Sep 9, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 inahitaji marekebisho makubwa sana ikiwemo convening of a constitutional conference a separate entity from the National Assembly in adopting a new constitution.
  Mwaka 1977,a Constitutional Committee consisting of 20 members ten being from Tanzania and ten from Zanzibar walikaa na kuunda katiba ya CCm baada ya Muungano wa TANU na ASP.
  The same consitutional committee were convened by NEC to collect ideas on the makinf a new constitution.Mind you,this comittee ilianza kufanya kazi kabla hata hawajapewa madaraka hayo.
  Nyerere alipitisha a govt notice changing the National Assembly into a Constitutional Assembly.
  Ukiangalia mpaka hapo,misingi ya ku-adopt a new constitution meshavunjwa kwa kiasi kikubwa sana.
  The proportion of the members between Zanzibar and Tanzania was unfair and it had been skewed in favour of Tanzania Mainland.
  NEC sat behind doors adopting the proposals which were later forwaded to the Constituent Assembly to be passed.They sat for three hours making long speeches za kipuuzi na hata Waziri Mkuu aliposimama alisema waziwazi kwamba katiba mpya ina-reflect needs za chama tawala.
  ukijaribu kufuatia yote hayo utaona kabisa katiba yetu jinsi gani inahitaji marekibisho makubwa sana.
  hata baadhi ya mabadiliko makubwa yaliyofuatia katiba yetu ya mwaka 1977 hasa lile la all organs of the state to do its operations in accordance with the Part's objectives.Hiki kipengele kiliondolewa kwenye katiba baada ya mabadiliko ya vyama vyingi ya mwaka 1992.
  Tunahita mabadiliko makubwa sana ya katiba.
   
 4. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kevo,

  Laiti watu wangechukua muda na kusoma na kuzielewa Katiba ya nchi na ya CCM, wasingeshangaa feri kwa ninachoandika!

  Hivi mfano ndani ya CCM wakiamua kumvua Kikwete madaraka ya Uenyekiti wa Chama na Uanachama, atakuwa amepoteza sifa ya kuwa Rais na hivyo kuondolewa madarakani bila Bunge au Mahakama Kuu kuamua kuwa hastahili kuwa Raisi?
   
 5. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  uchambuzi mzuri sana ila ni vizuri kuandika katiba mpya inayoendana na wakti
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu Rev,

  Katiba yetu inasema katika moja ya qualificatons za Uraisi ni lazima raisi awe ni mwanachama wa chama cha kisiasa kilichosajiliwa (mind you hili linakinzana sana na maamuzi ya mahakama kwenye kesi za mtikila za private candidate).
  Hivyo basi itamlazimu raisi wetu kuachia madaraka coz ya lack of the consitutional legitimacy ya ku-retain madaraka!
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Ni lazima tujue kuwa katiba ya Tanzania na ile ya Zanzibar zote zinabainisha wazi kuwa viongozi wote wa Serikali wanawajibika kwa Chama na sio wananchi.

  Hilo na mengine mengi yanapelekea katiba hiyo kuto kidhi matakwa ya wananchi.

  Ni lazima kabisa wananchi kudai KATIBA MPYA na wala sio kudai mabadiliko ya katiba
   
 8. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2009
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Nakuunga mkono kwa hoja hii.katiba yetu hivi sasa imejaa patches(viraka).
  Amendments kila la leo.
  Ni majuzi tuu hapa tumesikia stakeholders wameshakaa na kujadili kuhusu katiba mpya na tayari first constitutional draft ipo tayari ila bado haijafanywa for public bado inafanyiwa matengenezo zaidi.Nilipata kuiona kwa Dr Sengondo Mvungi a reputable constitutional lawyer na nadhani sasa serikali yetu itaikubali without any reservations ila ni safari ndefu kupata katiba mpya kama hatutakuwa na serikali kichwa ngumu.
   
 9. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  haha...interesting sana Rev. Nadhani NEC ikikuvua uanachama, utaweza kuendelea kuwa Rais/mbunge kutokana kwanza na Ibara ya 39 kusomeka "Mtu hatastahili kuchaguliwa kushika kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano isipokuwa tu kama-.."
  Hapo emphasis kwenye neno kuchaguliwa. Point hii imetiliwa nguvu zaidi na mahakama kama alivyosema Dr Slaa kwenye hii post:

  "Recta,
  Statement yako kuwa mtu akinyang'anywa uanachama Ubunge wake una cease automatically siyo kweli sana. Nadhani turudi kwenye Historia ya Bunge letu, ambapo CUF kupitia vikao vyake halali viliwafukuza uanachama wabunge wake wa Viti Maalum. Wabunge hao walienda mahakamani na Wakarudishwa na Mahakama, na wakaendelea kuwa Wabunge hadi mwisho wa uhai wa Bunge hilo. Nadhani tufanye utafiti kuona kuwa kinachosemwa kuwa Chama kina absolute power siyo kweli. Tatizo ni kuwa wengi hawafahamu "avenues" nyingi za haki katika Sheria zetu. Tujenge utamaduni wa kufanya utafiti wa kina ili tuweze kuisadia jamii yetu na Taifa kwa ujumla. Tunaweza kuwakatisha Tamaa, wakati Precedence ipo.
  "

  Hii post inapatikana thread hii hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/36712-je-ccm-kuingilia-uhuru-wa-bunge-imevunja-katiba.html

  Hivyo nadhani Katiba ya Chama haiwezi kutawala Katiba ya Nchi hata siku moja, na sidhani kama Mahakama zitaruhu jambo hili kutokea. Hii ni kutokana na Vyama kupewa limited powers katika Katiba, kama ulivyogusia.
   
 10. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2009
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Kinachotokea sasa hivi Dodoma cha Wabunge kupigana kikumbo na Serikali Kuu ni matokeo ya Katiba ya nchi kuingiliwa na Katiba ya CCM hasa kutokana na mazoea ya kugeuza mambo ya Serikali kuwa ya Chama pindi inapoelekea kuwa matakwa ya Chama hayaendani na jinsi sehemu moja ya Serikali iwe ni Serikali Kuu, Bunge au Mahakama inavyofanya kazi.

  Nilipoleta hoja hii, niliegemea sana kuhusiana na suala la Urais, lakini hata katika ngazi nyingine, utaona mkorogano huu na ndio maana sasa hivi Wabunge na Serikali Kuu wanavimbishiana vichwa na haitachukua muda kusikia kuwa Wabunge wa CCM wameitwa na kukaa kama kamati ya Chama na "kusawazisha" mambo!
   
 11. Tangawizi

  Tangawizi JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 2,835
  Likes Received: 927
  Trophy Points: 280
  Ingawa mjadala wa kubadilisha katiba unaonekana kama ni kitanzi kwa wanasiasa, naona njia pekee ya kuboresha mambo ni kuangalia katiba kama inakidhi mahitaji yaliyopo. Ni kweli, tunaweza kuwa na watu wazuri wasioamini katika vyama vilivyopo, ila hawawezi kuwa viongozi kwasababu tu hawana vyama.
  Kinachowaogopesha sijui ninini ila naona kama kuwa na katiba inayokubaliana na hali halisi iliyopo itakuwa vema pia kwa CCM maana watatengeneza mazingira mazuri ya kujiboresha kama chama kikongwe cha siasa.
   
Loading...