Informer
JF-Expert Member
- Jul 29, 2006
- 1,599
- 6,669
Mgomo wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambao ulitangazwa na Rais pamoja na makamu wao wa serikali yao ya wanafunzi DARUSO unaendelea muda huu ndani ya chuo hicho ambapo wanafunzi wamekusanyika katika eneo maarufu la "Revolution square" kwa amani huku wakiimba nyimbo mbalimbali (kama sio juhudi zako Nyerere..., Sitasimama maovu yakitawala...., Vijana tusilale bado mapambano.... Alisema Nyerere vijana wote tumelegea sharti tuanze mchakamchaka....) Wamesikika wakiimba kwa hisia.
Wanafunzi hao wanadai fedha zao za kujikimu ambao kwa kawaida zinatakiwa kutolewa kila baada ya siku 60 na kwa sasa ni siku zaidi ya 05 zimepita bila wanafunzi hao kupewa fedha za kujikimu kwa madai kuwa serikali haina fedha.
Tayari Jeshi la Polisi limeanza kuwasili ndani ya eneo la Chuo.
Updates to follow...
Wanafunzi hao wanadai fedha zao za kujikimu ambao kwa kawaida zinatakiwa kutolewa kila baada ya siku 60 na kwa sasa ni siku zaidi ya 05 zimepita bila wanafunzi hao kupewa fedha za kujikimu kwa madai kuwa serikali haina fedha.
Tayari Jeshi la Polisi limeanza kuwasili ndani ya eneo la Chuo.
Updates to follow...
Hatimaye Rais wa serikali ya wanafunzi UDSM Erasmi Leon amekabidhiwa cheque ya bilioni 5.7 jioni hii na utawala wa chuo hicho baada ya mgomo uliofanyika kwa siku nzima chuoni hapo ambapo Rais Erasmi na makamu wake Mshangama Shamira waliongozo mgomo huo.
Akiwahutubia wnafunzi hao muda huu amewambia kiasi hicho cha fedha kimepatikana na kufika katika akaunti ya Chuo ambapo Jumla ya wanafunzi 12,673 watapewa fedha hizo za kujikimu ambazo zilikuwa zimecheleweshwa tangu May 27, 2016.
Hata hivyo bado wanafunzi hao wamekataa kuondoka eneo la revolution square mpaka pale watakapothibitisha fedha hizo kuingia katika akaunti zao, Jambo ambalo Rais wa DARUSO ameahidi kuwa linafanyika jioni hii katika hali ya dharula, wafanyakazi wa benki ya tawi la CRDB UDSM wanaendelea na kazi mpaka muda huu.