Mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini waandaliwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini waandaliwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Oct 7, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,608
  Trophy Points: 280
  Date::10/7/2008
  Mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini waandaliwa
  Na Jackson Odoyo
  Mwananchi

  UMOJA wa Vyuo Vikuu nchini (Tahiliso) umepanga kufanya mgomo wa wanafunzi wa vyuo vikuu vyote nchini utakaofanyika Oktoba 27 mwaka huu serikali itakapo kubali kubadili sera ya elimu nchini.

  Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Katibu Mkuu wa umoja huo, Mtatiro Julius alisema katika mgomo wanafunzi hawataingia darasani mpaka hapo serikali itakapo kubali mapendekezo yao.

  Alisema lengo la mgomo huo ni kuishinikiza serikali ibadili sera zote zinachangia kudidimiza maendeleo ya elimu nchini ili usawa wa elimu uwepo kati ya mtoto aliyezaliwa katika familia isiyokuwa na kipato kizuri na familia yenye kipato kizuri.

  Aliongeza kuwa moja ya mambo watakayo yapinga katika sera hiyo ni kitendo cha wanafunzi kufukuzwa chuoni kufukuzwa wasimafanye mitihani ama kunyimwa matokeo yao baada kufanya mitihani.

  ''Sera inayosimamia maendelea ya elimu nchini inachangia kudidimiza elimu ya nchi na hasa kwenye suala la ada ya wanafunzi ambalo husababisha wanafunzi kufukuzwa chuo kwa kushindwa kulipa ada,'' alisema Mtatiro.

  Alifafanua kuwa kitendo cha serikali kumpunguzia ama kumfutia ada mwanafunzi aliyetoka katika familia isiyokuwa na uwezo wakati akisoma elimu ya chini lakini anapingia elimu ya juu alipie sawa na wale wenye uwezo haileti uwiano wa elimu nchini.

  Aliongeza kuwa hali hiyo ndiyo inayosababisha wanafunzi wa vyuo vikuu kufukuzwa chuo kila wakati, kama ilivyotokea katika Chuo Kikuu cha Ardhi mwaka huu.

  ''Kitendo cha serikali kuwafukuza wanafunzi 227 wa chuo hicho ni kuongeza migogoro vyuoni, makazini na hata kuongeza utitiri wa vyeti bandia maofisini,'' alalamika Mtatiro.

  Hata hivyo, alisema serikali inashindwa kuwajali wasomi watakaoisaidia nchi baadaye na badala yake inawakumbatia wawekezaji wasiokuwa na uwezo wa kulipa mishahara ya wafanyakazi wao.

  Alifafanua kitendo cha serikali kushindwa kuwatetea wasomi wanaotoka katika familia maskini bila kujali kwamba wao pia ni sehemu ya jamii ya watanzania nikuwanyima haki yao ya msingi.
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Fighting the govt is quite a long process and to get what you want is another stage!Wnafunzi wanakandamizwa kwa kweli na sijui kama watawahi kusikilizwa maana as we all know sheria ipo kwa ajili ya kumlnda yule mwenye nafasi kubwa zaidi ila siyo wa lower class
   
 3. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #3
  Oct 8, 2008
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Tusipoangalia nchi hii watu hawatasoma, nilikuwa iringa wiki hii pale ruaha uniiversity college, ili mwanafunzi asajiliwe ni lazima awe na na tshs 725,000, aidha umepata mkopo au hapana hizi lazima uzitoe ndo uingie chuoni.watoto wameaga kwao kuja shule wanazurura mjini wakisubiri hiyo bodi ya mikopo ambayo haija-process mikopo na haijulikani ni lini itakamalisha kazi hiyo, watoto wa kike ukikutana nao wanakusaklimia bila sababu, muda si mrefu au tayari washajitumbukiza kwenye umalaya.nawaunga mkono hawa kwenye mgomo wao, hawana njia nyingine dhidi ya serikali bubu, isiyowasikiliza waliyoichagua
   
 4. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #4
  Oct 8, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Migomo mingine ni ya kujiumiza wenyewe. Vyuo havitobadilisha ratiba zao ipasavyo kuweza kurusu huu "mgomo", na wanafunzi wao wenyewe ndio wataopata shida ya kujaribu kujifunza vile ambavyo walitakiwa wafundishwe awali kufuatana na ratiba ya awali. Matokeo yake? Wanafunzi kushindwa kumaliza kusoma modules vizuri na labda kushindwa kufanya mitihani inavyotakikana.


  Hivi wanafunzi wanataka serikali ifanyeje hasa ili iweze kupata ada zao kama sio kuzuia majibu yao ya mtihani?
   
 5. Mushobozi

  Mushobozi JF-Expert Member

  #5
  Oct 8, 2008
  Joined: Aug 20, 2007
  Messages: 543
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  lakini si mtatiro kamaliza chuo? au katiba ya Tahiriso inaruhusu hata watu ambao tayari ni graduates, na hawako chuoni?
   
 6. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #6
  Oct 8, 2008
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  jasho lao ndilo litakalowakomboa, wapiganie chao, kila kitu kinakuwaga hivyohivyo alafu mafanikio yanakuja.selikali inasema imeshindwa kuwalipia watu hadi inawafukuza, wakati mabilioni kibao yanaliwa kama karanga, hii ni nini? si ndo zingesomeshea watoto wetuhizo, afu, kikwete kila siku misafari ya vekesheni marekani kwenye mihoteli ya kufa mtu, watu wanabwia hela mtindo mmoja huko selikalini, matunda yake nini kikwete hadi aanze hizo safari zake? si kutuletea Leon sullivan waliokuwa kuchangia milioni sitini?, ambazo hata mimi ningeweza kuchangia atu ile nauli yake ibakie hapa ipeleke watoto shule? hivi viongozi wetu wana uchungu na nchi yetu kweli? kwanini tusijibane na kupenga mikakati inayotekelezeka ili baadae ulie kivulini?viongozi wanapenda anasa tu. watoto wetu tena toka vijijini hawana hata hela ya kusomea au kunywa maji pala chuo, wakienda mjini hawana nauli wanapishana tu ni migari ya viongozi,migari ya garama. huu si uungwana.
   
 7. D

  Domisianus Senior Member

  #7
  Oct 8, 2008
  Joined: Aug 1, 2008
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Migomo kwa vyuo si jambo la kawaida kama ambavyo watu wanasema.tuangalie huu mgomo hawa wasomi wanataka nini na wamekiomba kwa muda gani mpaka sasa na bado selikeli imekaa kimya.It is just a very simple logic kwa nini serikali inakaa kimya kwa mambo ambayo ni ya msingi wakati upuzi inalipuka kama kifuu cha nazi.Hivi kuna haja gani ya kuwepo kwa bodi ya mikopo hapa Tanzania kwa sasa? iondoke haina maana yoyote zaidi ya kuendeleza ubaguzi.Tunaweza kulalamika kwamba kuna kuvuja kwa mitihani lakini tuangalie source ni nini?
  Zamani ulikuwa ukipata division III na ukipata udahili ulikuwa unashangilia na unaaga nyumbani kuwa unaenda kusoma na hata kisaikolojia unajiandaa kwenda kusoma. je hiyo hali kwa sas ikoje wana ndugu? Hiyo mishahara wanayolipa wanafanyakazi wa bodi ni shilingi ngapi na matumizi ya kawaida ya kiofisi ni shilingi ngapi kwa mwaka achilia mbali vikao vya kila siku na night?
  Inatakiwa ifike wakati tujikomboe kifkira, hizo bilions za walipa kodi zinazokwapulia na manyan'ganyi zingetumika vizuri, tusingeweza kuwalipia ada hao wanafunzi kweli jamani?
  Tanzania tuna migodi mingapi na pesa inayopatikana huko inatumikaje kama siyo kuishia kwenye semina elekezi.Mimi naona wafanye mgomo mpaka kieleweke na hiyo bodi ifutiliwe mbali kabisa ili mtu akifaulu asiwekewe mizengwe tena na kuwa na mawazo jinsi ya kupata mikopo.Ni bora hata waongeze pay as you earn ili watu wasome bure na kupata taifa liloelemika lenye mapenzi na nchi yao.
   
Loading...