MGOMO wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wa kutokuingia madarasani kushinik | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MGOMO wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wa kutokuingia madarasani kushinik

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kilimasera, Dec 22, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  MGOMO wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wa kutokuingia madarasani kushinikiza wenzao waliokuwa wakishikiliwa na polisi kuachiwa pamoja na kupatiwa fedha kwa ajili ya masomo kwa vitendo, umekwisha baada ya serikali kuwatekelezea maombi yao.

  Wanafunzi hao waliokuwa wakishikiliwa na polisi kwa kuongoza mgomo huo, wameachiwa huru na serikali imeuagiza uongozi wa UDOM kuorodhesha majina ya wanafunzi wa mwaka wa tatu na kuyapeleka Hazina, Tume ya Vyuo Vikuu (TUC) na kwenye Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) ili wanafunzi hao wapatiwe fedha kwa ajili ya masomo kwa vitendo.

  Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Idris Kikula alisema maamuzi hayo ya serikali yalitokana na kikao kilichofanyika juzi chini ya uenyekiti wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa pamoja na uongozi wa Mkoa wa Dodoma.

  Katika kikao hicho kilicholenga kuangalia chanzo cha mgomo chuoni hapo, kilifikia muafaka wa uongozi wa chuo na serikali kuondokana na migomo isiyokuwa na maana.

  Juzi wanafunzi wa Kitivo cha Sayansi ya Jamii waligoma kuingia madarasani na kusababisha vurugu zilizoilazimu polisi kuingilia kati na kuwatawanya wanafunzi hao na wengine kuwashikilia.

  Profesa Kikula alisema kutokana na kikao hicho, serikali imeuagiza uongozi wa chuo kuongeza kasi ya kuhakikisha wanaorodhesha majina ya wanafunzi wa mwaka wa tatu na kuandaa bajeti na kuipeleka serikalini kwa lengo la kuwapatia wanafunzi fedha kwa ajili ya masomo kwa vitendo.

  Kwa mujibu wa maelezo ya Profesa Kikula ambaye alikuwa katika kikao hicho, Waziri Dk. Kawambwa alisema tatizo hilo limetokana na ufinyu wa bajeti ya wizara husika.

  Alidai kuwa uongozi wa chuo ulikaa Septemba 8, mwaka huu na kuandaa bajeti iliyopelekwa serikalini, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti wanafunzi hao hawakupata fedha kwa ajili ya masomo kwa vitendo.

  Alisema serikali imeuagiza uongozi wa chuo hicho kuandaa programu ya masomo kwa vitendo kwa kila kitivo pamoja na orodha ya majina ya wanafunzi na bajeti hiyo kuandaliwa mapema ili kuepuka mgomo.
   
Loading...