Mgomo wa walimu: Watoto wa wakubwa wanasoma private? Hakiwashtui | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa walimu: Watoto wa wakubwa wanasoma private? Hakiwashtui

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Profesa, Jul 1, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Bado mnataka kura 2015?

  Kama wewe ni kingozi wa kweli wa nchi hii, mwenye mapenzi mema na taifa hili, waondoeni watoto wenu kwenye hayo mashule ya private ya ki-st... na muwarudishe kwenye mashule ya serikali ikiwemo primary na sekondari (kwa sekondari, ni hasa wale waliofaulu). Walimu hebu ibukeni na data za wanafunzi ambao hawakuripoti shuleni hata kama walichaguliwa na wakapelekwa Feza... na kwengineko? Na watoto wangapi wa wakubwa wako kwenye mashule binafsi ya msingi na nasary? Maana hili ndilo linalofanya wasijali kabisa maendeleo ya elimu ya wengi wetu. Hawana njaa hao, hawana shida ya nyumba wala usafiri, watoto wao wanaenda shule na magari na wote wako hapa Dar es Salaam, huko nangulukulu watakuja ziarani tu na kama hawajapewa posho ya kutembelea hawaji!

  Walimu na madaktari msikate tamaa, mpaka kieleweke, ninachotaka hawa viongozi mpaka wajifunze kuwa uongoziz ni dhamana sio ufalme kwamba unataka uabudiwe, wawe na utu wakati wa kushughulikia malalamiko ya wananchi wake. Tumewapa dhamana hawa viongozi, kama kitu hakiwezekani wasitoe maneno ya udhalilishaji na ubabaishaji kwa kusingizia upinzani au eti maadui wa chama, wakati ni wazi kabisa ndani ya serikali mambo hayaendi sawa! Kama kuna ugumu, toeni maaelezo na ushahidi wa mambo, kwanini serikali haiwezi kuongeza mafao ya walimu au kuyashughulikia, sio kusema tu hamna fedha, sio jibu linalojitisholeza.

  Kama serikali inataka ichaguliwe tena, kwa kizazi hiki waliko kazini kwenye maofisi mengi ya serikali na binafsi, huwezi kutumia ubabe hata kidogo, kuna idadi kubwa ya vijana ambao wameelimishwa na media na thinking yao is so different, haifanani na yakina Mheshimiwa Wasira na wenzanke. Heshima ina maaana tofauti, si unyenyekevu tena (kwakuwa kipindi kilichopita ukiwa na cheo hata kama unafanya upuuzi hakuna anaeibuka na kukusoa tu, lazima atumie unyenyekevu wa hali ya juu), ila ni heshima na utu, na kuthamini maoni na mawazo ya kila mmoja. Mnalielewa hili? Na tena, kutumia hoja chanya kujibu maoni hasi na pingamizi ya mambo. Amkeni madaktari na walimu walioko kazini idadi yao kubwa ni kizazi kpya hawajapita JKT, wala hawakusoma katiba ya CCM kama somo kama wengi wenu mlioko madarakani. Hawafikiri na kuamua kama nyinyi!

  Hawa ndiyo, wapiga kura 2015! CCM mlioshika hatamu please change and adopt new trends, ongeeni na walimu kwa busara na uvumilivu, msituingize shimoni. Ongeeni na walimu na wekeni mambo yenu wazi na mipango na muwe na hoja ili wawaelewe, msitarajie heshima kwa kuwa wababe nakutarajia kuabduiwa hawatafanya hivyo hawa ni kizazi kingine. Na hakuna cha ajabu, Tanzania ina changamoto kama nchi nyingine Afrika, so treat all of the Doctors and Teachers as human being and important, na ni sehemu ya watu ambao nyinyi ni viongozi wao.

  Msisababishe watu wakachagua chama ili mradi tu wanataka mabadiliko, kwakuchoshwa na tabia zenu mbaya za kutokukubali kubadilika na kushughulika na kero za wazi za wananchi.
   
 2. PPM

  PPM JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 839
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Walimu ni wachumba tu hao, hawawezi goma
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Walisema kuanzia leo ni mgomo je nao wako kwenye mgomo....
   
 4. kadoda11

  kadoda11 JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 16,246
  Likes Received: 8,308
  Trophy Points: 280
  natamani formula ya hii migomo iwe hivi:
  ma-doctor+walimu+wauza mafuta+wasafishaji+wafanyakazi=boooooom!:boxing:
   
 5. A

  AMKA Member

  #5
  Jul 1, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Tatizo la walimu wakitishiwa kidogo wanaogopa
   
 6. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  walimu nguvu ya soda,wengi wanaishi kwa mikopo,wanaogopa wakigoma harafu wakafukuzwa taasisi za mikopo zinawakula
   
 7. n

  nsami Senior Member

  #7
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 175
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu waalimu walio wengi ss hvi ni product kutoka vyuo vikuu achana na wzee wa enzi za mwalimu tatzo ambalo lipo hawajapata kiongoz kama ulimboka na hii inatokana na viongozi wengi ni walewale akina mgaya etc.tunahitaji vijana washkile tucta na vyma vingne
   
 8. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Naona mnawachokoza ili muone matunda yao halisi ya kile walichokusudia... Faida ni nini, uma utaamka na kuibana serikali ishghulikie swala hili, ikishindwa, ajenda inabadilika kama kawaida, inakuwa swala lingine kabisa la kisiasa... Aluta Continuum, unless my Leaders change their way and attitude. Mheshimiwa Mwinyi akifunga baraza la maulidi mwaka jana alisema "ukiona mwenzako anayolewa, wewe tima maji kicha chako" akifanya reference kwa hali ilivyokluwa huko kaskazini mwa Afrika katika nchi za kiarabu za Afrika. Sasa basi, badala ya kusubiri mpaka utie maji, CCM just be realistic and start working on the situation.
   
Loading...