MGOMO WA WALIMU WAPAMBA MOTO: Habari na matukio katika picha

Udhaifu wa Kikwete na Kawambwa hauwezi kutatua madai yalosababisha mgomo wa walimu, hapo ndio pakuanzia.

Ombi ni kuwa taasisi/asasi kama bunge, mabaraza ya haki za kiraia na NGOs waishinikize serikali hii kukaa chini na walimu na kutekeleza madai yao ambayo mengi ni ya msingi. Masikitiko ni kuwa tayari kiwango cha elimu kimeshuka mno na madhara ya mgomo huu yatazidi kuharibu mambo.

Hawa watoto kwenye picha ni wadogo, sasa kama tutawalea kwenye utamaduni kuwa kudai haki ni mpaka fujo baadaye hali itakuwa mbaya sana.
 
Serikali i.e. CCM, waache propaganda za kipuuzi. Hoja mfu za udini, hujuma (hasa kuihusisha CHADEMA) na vitisho hazina maana na zimeshindwa tokea awali. Kwa mfano kitisho cha kuzuia mshahara wa walimu ni dhaifu kabisa. Hivi mwalimu anadai posho na malimbikizo ya zaidi ya miaka 10, wewe unakuja kumzuilia mshahara wa mwezi 1 i.e. wa July....basi mlipe hizo staili zake ulizohodhi bila idhini yake uone kama atalia dhiki!

Mimi na declare interest, kwamba naunga mkono madai ya walimu. Hivyo naunga mkono mgomo.
(Ingawa kwa masikitiko na maumivu sana).
 
kuna kundi kubwa la wanafunzi wamevamia jengo la ITV na wanapiga kelele tunataka walimu wetu..aya yanaendelea ivi sasa hapa Mwenge.

mkuu sasa itv na madai ya walimu wao imekuiwaje tena.....sipati connection hapo ebu nisaidie au wanataka wauze sura maana hawa watotowetu wa kiduku, face book, na .com hawa ni hatari sana
 
Wasije wakaanza kuteka watoto wetu manake hawa jamaa hawana huruma kabisa.Nimemwambia mtoto wangu asiende shule asije akatekwa
 
Kazi ya ualimu ni wito, Tafadhalini rudini darasani mkafundishe. hakuna haja ya kudai maslahi, kwani mnapata baraka kwa kujitoa kwenu sadaka kwa maendeleo ya taifa hili. hakuna mtaalamu au kiongozi ambaye hakupita katika mikono ya waalimu. kwa wale wakrisu turejee maandiko kwa upande wa waislamu kwa kweli sijui, lakini biblia inasisitiza kujitolea sadaka.
 
serikali tatueni matatizo haya jamani taifa la kesho linaangamizwa
kila kitu huanza kidogokidogo "usipoziba ufa utajenga ukuta"
 
Kazi ya ualimu ni wito, Tafadhalini rudini darasani mkafundishe. hakuna haja ya kudai maslahi, kwani mnapata baraka kwa kujitoa kwenu sadaka kwa maendeleo ya taifa hili. hakuna mtaalamu au kiongozi ambaye hakupita katika mikono ya waalimu. kwa wale wakrisu turejee maandiko kwa upande wa waislamu kwa kweli sijui, lakini biblia inasisitiza kujitolea sadaka.
Unakumbuka Yesu aliwaambiaje Mitume wake kuhusu Uongozi?.
"Atakaye kuwa mkubwa na ajifanye mdogo".
Hii inamaana kuwa ukijifanya mdogo utajua mahitaji ya wadogo hivyo utawatimizia!.
 
Nchi sijui inaenda wapi,halafu kuna watu wanaona haya mambo ni madogo tu,eti ni upepo tu utapita,ni BOMU. shame on this Govt!
 
Kazi ya ualimu ni wito, Tafadhalini rudini darasani mkafundishe. hakuna haja ya kudai maslahi, kwani mnapata baraka kwa kujitoa kwenu sadaka kwa maendeleo ya taifa hili. hakuna mtaalamu au kiongozi ambaye hakupita katika mikono ya waalimu. kwa wale wakrisu turejee maandiko kwa upande wa waislamu kwa kweli sijui, lakini biblia inasisitiza kujitolea sadaka.
kafanye wewe kama ni wito! ndio wamekutuma kuja kumwaga huu ***** hapa???
 
Huyo mwl aliyepigwa safi sana..Ivi inakuaje wenzao wanashikamana ili kufanikisha zoezi lao la maisha bora yeye anaona eti sio haki kwa wanafunzi kuacha kufundishwa....Na huyo mwalimu wa kike anaesahihisha mie nadhani CWT imuwajibishe kwa utovu wanidhamu na kujipendekeza pia ifuatilie na vyeti vyake ndo hawa hawa walionunua vyeti sio bure...CWT HONGERENI ATA KM MABUBU BADO YAPO KIMYA YAKIPIMA UPEPO HALI INAVYOENDELEA MABUBU YATANENA ATA KM NI KWA LUGHA
 
Tunaiomba SERIKALI isichukulie swala hili kimzahamzaha na kupandikiza PROPAGANDA lukuki. Ni vema serikali ikawa makini hasa kwa kuelezea namna wanavyoyashughulikia matatizo ya walimu na kuyatekeleza. Tunafahamu huu mgoma ulianza siku nyingi na ndiyo chanzo kikubwa cha elimu yetu kushuka (rejea matokeo ya mitihani shule za msingi na sekondari). Vilevile tunawajenga vijana wetu kutoiamini serikali na kuamini kuwa haki ni lazima ipiganiwe ndiyo ipatikane. Baada ya miaka 10-15 ndiyo tutaona madhara makubwa ya kuachia upepo huu upite.

Fefensiv mekanizm ya serikali yetu imebaki kulaumuswala hili kama ni nyendo za kisiasa. Nilimsikiliza waziri leo Clouds Fm akilalama kua malipo yamefanyika ikiwa na 14% increase ya salary. Lakini cha ajabu walimu kutoka sehemu tofauti walikua wakipiga simu na kumkosoa maelezo yake. TANZANIA zaidi ya uijuavyo!
 
Udhaifu wa Kikwete na Kawambwa hauwezi kutatua madai yalosababisha mgomo wa walimu, hapo ndio pakuanzia.

Ombi ni kuwa taasisi/asasi kama bunge, mabaraza ya haki za kiraia na NGOs waishinikize serikali hii kukaa chini na walimu na kutekeleza madai yao ambayo mengi ni ya msingi. Masikitiko ni kuwa tayari kiwango cha elimu kimeshuka mno na madhara ya mgomo huu yatazidi kuharibu mambo.

Hawa watoto kwenye picha ni wadogo, sasa kama tutawalea kwenye utamaduni kuwa kudai haki ni mpaka fujo baadaye hali itakuwa mbaya sana.

Mkuu hili hawalitambui, na kwa taarifa tu kule kwa Gadaffi walioshika AK47 walikua wasomi wa vyuo vikuu wasiokua na ajira mtaani. Huu ni mwanzo tu bado wale wa Shule za kata pia kudai walimu hawatoshi.
 
Huyo Mwalimu wa Shule ya Msingi Mmoja, Salma Mtili hapo juu ataonekana ni msaliti kwa walimu wenzake. Awe mwangalifu!
 
mkuu sasa itv na madai ya walimu wao imekuiwaje tena.....sipati connection hapo ebu nisaidie au wanataka wauze sura maana hawa watotowetu wa kiduku, face book, na .com hawa ni hatari sana

Hahahaaaaaaa nahisi wanataka publicity ya jambo hili kwa kua TBC1 tangu kuondolewa kwa Mhando haijihusishi na taarifa kama hizi!
 
utasikia ni upepo tu utapita .......hizi nimesha sema kwene thread yangu huko juu sinema hizi na watawala wanafuraia tu ila mwisho wake tutakimbiana hapa
 
Kazi ya ualimu ni wito, Tafadhalini rudini darasani mkafundishe. hakuna haja ya kudai maslahi, kwani mnapata baraka kwa kujitoa kwenu sadaka kwa maendeleo ya taifa hili. hakuna mtaalamu au kiongozi ambaye hakupita katika mikono ya waalimu. kwa wale wakrisu turejee maandiko kwa upande wa waislamu kwa kweli sijui, lakini biblia inasisitiza kujitolea sadaka.

"QUID PRO QUO" Nothing goes for nothing. Haiwezekani mwalimu mwenye shahada alipwe laki 2 na 30 kwa mwezi. Kwa maisha ya mjini hata tarehe 14 haifiki huna kitu.
 
Ukiwauliza mmoja mmoja kwanini unaandamana, kila mmoja anajibu lake
Kuna mtoto ameulizwa kwanini unaandamana kajibu sijui, unaenda hadi wapi kajibu sijui, mbona uko barabarani kajibu basi tu kwa sababu wenzangu wamekuja na mie nimekuja tunashangilia.! Unashangilia nini kajibu mwenge.lol!

Kwahiyo unataka kusema nini hapa, majitu mengine hapa watoto hawasomi badala ya kuleta hoja za msingio unataka kutuaminisha kuwa hao watoto wanatembea tu barabarani, kama huyo mmoja hajui sawa yawezekana ni kutokana na umri wake kuwa mdogo au ametoka atokako akuta wenzake wanaandamana akajiunga nao, suala la walimu kugoma au kutogoma kwake hajui, ila wenzake wengi wanajua. Hata mimi mwanangu aliniuliza jana mbona walimu wanalipwa hela nyingi aliposikia mshahara wa laki mbili kwa mwezi, ingawa yeye yuko std 2 nalipa karibu Tsh. mil.2 kwa mwezi, sasa unadhani ni haki kusema hapa laki 2 ni hela kwa sasa?
 
Back
Top Bottom