MGOMO WA WALIMU WAPAMBA MOTO: Habari na matukio katika picha

Mzalendo JR

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,193
515
Na Gideon Mwakanosya, Songea.

MWALIMU mmoja wa jinsia ya kike aliyefahamika kwa jina moja la Kahimba wa shule ya msingi ya Kambarage iliyopo Kata ya Msamala katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma amajeruhiwa vibaya kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili na kundi linalodaijwa kuwa ni la wanafunzi wa shule hiyo ambao wanadaiwa kuwa na hasira baada ya walimu wengi wa shule hiyo kutoonekana eneo la shule kufuatia mgomo wa chama cha Walimu (CWT).

Akizungumuza na waandishi wa habari hizi Mjini Songea mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kambarage Adolfina Ndunguru alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo alidai kuwa ni udhalilishaji mkubwa kwa mwalimu kupigwa na wanafunzi.

Ndunguru alisema kuwa yeye pamoja na walimu wenzake hawakuweza kufika kwenye eneo la shule kwa kuwa wao ni walimu ambao wamekubaliana kugoma kutokana na Serikali kushindwa kutimiza ahadi yao wanayodai.

Alifafanunua kuwa inadaiwa kundi la wanafunzi lilipomuona mwalimu Kahimba kwenye eneo la shule hiyo lilimvamia na kuanza kumpiga mawe sehemu mbalimbali za mwili na baadaye alifanikiwa kukimbia.

Kwa upande wa baadhi ya walimu wa shule za msingi, Sekondari na Chuo cha Ualimu cha Songea kilichopo Manispaa ya Songea ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa mgomo utaendelea mpaka Serikali itakapo ridhia kuwalipa madai yao hasa ikizingatiwa kuwa wao wanafanyakazi katika mazingira magumu.

Waandishi wa habari walifanikiwa kutembelea baadhi ya shule za Msingi na sekondari ambazo zilikuwa hazina walimu kabisa na kwamba wanafunzi wa shule hizo wakiwa wamezagaa mitaani huku wakiinung`unikia Serikali kwa kuto watendea haki walimu wao ambao alikuwa wakiwaandaa wanafunzi katika Mitihani ya kumaliza Elimu ya Msingi na sekondari.

Shule zilizotembelewa na waandishi wa habari ambazo hazikuwa na walimu kabisa ni Shule za Msingi za Matarawe, Mwembechai, Sabasaba, Mkombozi, Kawawa, Mfaranyaki, Majengo, Songea, Kambarage, Msamala na Majimaji na shule za sekondari za matarawe, Mfaranyaki, Shule ya wavulana Songea na Shule ya wasichana songea.

Kwa upande wake mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Majimaji Tamimu Ajali anayesoma darasa la tano ameiomba Serikali kuharakisha kutekeleza madai ya walimu wanayodai kwani bila kufanya hivyo kunauwezekano mkubwa wa kushuka kwa kiwango cha Elimu hasa ikizingatiwa kuwa wanafunzi wapo kwenye maandalizi ya kufanya mitihani.

Tamimu alisema kuwa ni vyema serikali ikatambua umuhimu wa mwalimu kwa kumuuongezea mshahara sawa na taaluma zingine muhimu kwa mfano. Wanajeshi, Madaktari,Wauguzi na wahudumu wa afya.

Afisa Elimu wa halmashauri ya Manispaa ya Songea Fulgensi Mponji amethibitisha kuwepo kwa mgomo huo wa walimu amabapo alisema Manispaa hiyo ina shule 72, Sekondari za Serikari 23, Shule za seskondari za binafsi 13 ambazo idadi kubwa ya walimu hawakuwepo kwenye maeneo yao ya kazi.

Alisema kuwa tayari ameshawaagiza walimu wakuu wa shule za msingi na waratibu Elimu kata wote kukutananao katika shule ya msingi Mfaranyaki kwa lengo kuwakutanisha walimu ili kuzungumzia namna ya kutatua tatizo hilo.

Naye Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Ruvuma Luya Ng`onyani alisema kuwa mgomo huo ni halali na umezingatia sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 kifungu cha 80 (1) ambapo hatua ya kwanza CWT kwa niaba ya wanachama tayari imetekeleza kutangaza mgogoro wa siku 30 kwa kujaza fomu CMA No: 1.

---
habari via dj-sek.blogspot.com





Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, wakiandamana jana Jumatatu Julai 30, 2012, kupinga haki yao ya msingi ya kupata elimu kuvurugwa kufuatia mgomo wa walimu ulioanza rasmi jana. Wanafunzi hao waliandamana umbali wa kilomite 10 hadi ofisi za Afisa elimu wa manispaa hiyo na kueleza "kesi" yao ambapo wameitaka serikali kumalizana na walimu ili wao wasome.

Wanafunzi wa shule za Makuburi na Mabibo, wakiwa chini ya mwembe, jana asubuhi Jumatatu Julai 30. Walimu wengi hawakuingia madarasani kufundisha jana wakiitikia mwitoi kutoka chama cha walkimu nchini kilichowataka kutofanya kazi leo Jumatatu na kuendelea hadi madai yao kuhusu maslahi yatakaposhughulikiwa na serikali.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba shule ya msingi Makuburi, wakijisomea baada ya walimu shuleni hapo kugoma kufundisha jana Julai 30, 2012. Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, ambaye hata hivyo alikataa kutaja jina lake, alisema walimu walifika lakini hawakufanya kazi wakiunga mkono agizo la rais wa chama cha walimu Gratian Mukoba, aliyewataka walimu wote kushiriki mgomo usio na kikomo kuanzai leo Jumatatu.

Afisa Elimu Taaluma wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Juliana Mlay (Kushoto) akitafakari nini cha kuwaambia "Wageni" wake, wanafunzi wa shule za msingi Kijichi na Bwawani za jijini walioandamana umbali wa kilomita 10 hadi ofisini hapo wakilaani kutosoma jana, kufuatia mgomo wa walimu ulioanza nchi nzima jana Julai 30, 2012.

Kiongozi wa wanafunzi walioandamana jana jijini Dar es Salaam, Christofa Msifuni Msuya wa darasa la saba, shule ya msingi Bwawani, akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye ofisi za Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam Jumatatu Julai 30, 2012.

Wanafunzi wa shule za msingi Bwawani na Kijichi, zajijini Dar es Salaam, wakiamnadmana jana kupinga kile walichokiita kuvurfughwa kwa haki ya mtoto ya kupata elimu, na hii ni kufuatia mgomno wa walimu ulioanza jana nchi nzima. Wanafunzi hao waliandamana hadi urefu wa kilomita 10 kutoka shuleni kwao hadi ofisi ya Afisa Elimu wa Manispaa ya Temeke, ziliko shule hizo, jirani na uwanja wa taifa ili kufikisha kilio chao.
PICHA: Blogu ya Khalfan Hamis




PICHA: Bashir Nkoromo blog

Wanafunzi wakiwa wanaelekea ofisi ya Mkuu wa wilaya

Wanafunzi wa shule za msingi Vwawa wakiwa wanapiga vidumu huku wakielekea ofisi ya mkuu wa wilaya ni Baada ya walimu kugoma.

Moja ya wanafunzi wa shule ya msingi Meta baada ya kuona walimu hawajaingia darasani yeye alichukua jukumu la kuwafudnisha wenzake

Wanafanzi wa darasa la saba shule ya msingi Meta wakiendelea kupeana mazoezi ya masomo mbalimbali baada ya waalimu wao kugoma kuingia madarasani

Wanafuzi wapo makini kumsikiliza mwanafunzi mwenzao

Mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi muungano akiwa nje ya shule akichezea mchanga maana walimu wamegoma
Picha na Arithy via Mbeya Yetu blog

Mwalimu wa Shule ya Msingi Mmoja, Salma Mtili akisahihisha daftari la mwanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo licha ya rais awa Chama cha Walimu Tanzaniza (CWT) kutangaza mgomo wa walimu nchi nzima.

Picha na Habari Mseto Blog







Wanafunzi wa shule ya msingi Ipembe, Nyerere, Unyankindi na Singidani katika Manispaa Singida (picha na Nathaniel Limu)


Source: wavuti - wavuti
 
Tunaiomba SERIKALI isichukulie swala hili kimzahamzaha na kupandikiza PROPAGANDA lukuki. Ni vema serikali ikawa makini hasa kwa kuelezea namna wanavyoyashughulikia matatizo ya walimu na kuyatekeleza. Tunafahamu huu mgoma ulianza siku nyingi na ndiyo chanzo kikubwa cha elimu yetu kushuka (rejea matokeo ya mitihani shule za msingi na sekondari). Vilevile tunawajenga vijana wetu kutoiamini serikali na kuamini kuwa haki ni lazima ipiganiwe ndiyo ipatikane. Baada ya miaka 10-15 ndiyo tutaona madhara makubwa ya kuachia upepo huu upite.
 
Kwa nchi kama Tanzania, jambo hili ni aibu kwa Taifa kwani serikali haijashindwa kutekeleza mahitaji ya walimu kwa kuwalipa stahiki zao, bali inawadharau na kuwanyanyasa walimu......Serikali kwa hili imechemka.
 
Kama ilivyo kawaida ya magamba badala ya kusolve crisis yatakoleza kupitia msitu wa magwepande. Ngoja tuone . Pengine wazee wa dsm wataitwa kwenda kuzomea . Dhaifu sana .
 
tunawaunga mkono walimu katika harakati za kudai madai yao. Hivi kwanini wabunge wao uwa wanapewa tu kila kitu kinongezwa ila kwa kada kama walimu, madokta kazi sana mpaka wagome na tena kupewa kazi ila katika hili mpaka kieleweke
 
natafakari uchaguzi mwaka 2015 sijui tanzania patakuaje!

ili nchi iwe salama 2015v inabidi ccm ife kabisa kabla ya kufika huko la sivyo watatumia sana ujinga wa polisi na wanajeshi kutaka kushinda kwa nguvu kitu ambacho watz waliochoka hivi hawataweza kukikubali
 
Serikali hili jambo si mchezo kama hawa watoto wanaweza kuandamana kwenda kudai haki yao ya msingi ya kusoma ujue hili jambo si kulifumbia macho hili litakuwa bomu kubwa sana na likija kulipuka ujue nchi hii itakuwa katika hali mbaya sana. srikali ichukuwe hatua madhubuti kuhakikisha swala mgomo linaisha mapema ingawa lilianza tatratibu hatua hazikuchukuliwa na hivi sasa unasubiriwa mgomo wa wafanyakazi wote wa serikali.


SIASA HAPA HAITAKIWI KABISA
 
Ukiwauliza mmoja mmoja kwanini unaandamana, kila mmoja anajibu lake
Kuna mtoto ameulizwa kwanini unaandamana kajibu sijui, unaenda hadi wapi kajibu sijui, mbona uko barabarani kajibu basi tu kwa sababu wenzangu wamekuja na mie nimekuja tunashangilia.! Unashangilia nini kajibu mwenge.lol!
 
up dates tafadhali leo maeneo mbalimbali hali ikoje juu ya huu mgomo........ jamjiiforums come on guys..... updates plzzzz
 
QUOTE=POMPO;4347044]Liwalo na Liwe, hizi Picha huziona? ama mpaka uambiwe na TISS?[/QUOTE]


Hawakutishika na wagonjwa ambao wanakata roho hospt mpaka madokta wenyewe wamesalim amri,iwe wanafunzi ambao wanaandamana kwa furaha kabisa na hata wengine hawajui nini kinawafanya waandamane,tatizo la kutanguliza siasa kwenye kila kitu ndio matokeo yake hayo'
 
QUOTE=POMPO;4347044]Liwalo na Liwe, hizi Picha huziona? ama mpaka uambiwe na TISS?


Hawakutishika na wagonjwa ambao wanakata roho hospt mpaka madokta wenyewe wamesalim amri,iwe wanafunzi ambao wanaandamana kwa furaha kabisa na hata wengine hawajui nini kinawafanya waandamane,tatizo la kutanguliza siasa kwenye kila kitu ndio matokeo yake hayo'[/QUOTE]
kwani watawapiga mabomu na wanafunzi?? hebu ngoja mie nichek movie nyingine part 2 ya ukombozi wa taifa kutoka kwa wadhalimu wa nchii hii :yawn:
 
Back
Top Bottom