Mgomo wa Walimu waiva; watoa notisi ya masaa 48 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Walimu waiva; watoa notisi ya masaa 48

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Jul 27, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  CHAMA cha Walimu nchini (CWT) kiko katika hatua za mwisho kutangaza rasmi kuanza kwa mgomo wa walimu nchini, unaotarajiwa kutangazwa rasmi wakati wowote baada ya saa 48 kuanzia asubuhi ya leo.

  Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT), Gratian Mukoba alisema mgomo huo sasa umeiva, baada ya mgogoro baina yao na Serikali uliodumu kwa siku 30 kumalizika bila kufikia suluhisho.

  Msimamo huo wa CWT unatolewa wakati madai ya Madaktari yakiwa bado hayajapatiwa ufumbuziwa kudumu na kusababisha kuzorota kwa huduma za afya katika hospitali za umma
  .
  "Baada ya kushindwa kutatuliwa, zoezi la kupiga kura limeanza tangu jana (juzi) na litaendelea hadi kesho (leo) saa 3 asubuhi, baada ya muda huo kupita, Chama kitakuwa na kazi ya kupokea matokeo ya upigaji kura kutoka kila Wilaya," alisema Mukoba na kuongeza:

  "Ikiwa walimu watakaounga mkono mgomo watakuwa wengi kuliko wale watakaoupinga, Baraza la Taifa la CWT litakutana kwa dharura kutangaza mgomo ambao utakuwa umeamuliwa na muda wa mgomo huo.

  Rais huyo alifafanua kuwa baada ya uamuzi huo kufikiwa CWT itatoa notisi ya saa 48 kwa Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ni Mkuu wa Utumishi wa Umma kumwarifu tarehe ya kuanza kwa mgomo ili alinde mali zake kama Sheria inavyoeleza.

  Mukoba alisema, mgogoro na Serikali ulisajiliwa Tume ya Usuluhishi na Uamuzi Juni 8 mwaka huu na kupewa namba CMA/DSM/ILA/369/12 na msuluhisi aliyeteuliwa na Tume hiyo Cosmas Msigwa kushindwa kuwasuluhisha.

  "Siku 30 zilianza kuhesabiwa Juni 26 na kumalizika Julai 25 mwaka huu, kwa msuluhishi Msigwa kutoa Cheti cha kuthibitisha kuwa mgogoro umeshindikana kusuluhishwa kwa mjibu wa Sheria," alisema Mukoba na kuongeza:

  Ndani ya siku hizo 30 tumekutana kujadiliana kwa vikao vitatu lakini hakukuwa na dalili zozote za Serikali kuhakikisha inatatua matatizo yetu.

  Rais huyo alisema, madai ya Serikali kushindwa kuyatatua ilisema ni kutokuwa na takwimu za walimu wangapi wanastahili kulipwa na huenda wengine wameshakufa.

  "Hoja hii ilikuwa na nia ya kupotosha ukweli wa madai ya walimu kwa kuwa kikao cha Julai 10 mwaka huu, Serikali iliwasilisha taarifa kuwa ingetumia zaidi ya Sh4 trilioni kulipa mishahara ya walimu tu kama ikilipa mishahara kwa viwango vilivyowasilishwa na CWT iweje itake tena takwimu," alihoji Mukoba.

  Mukoba alisema Serikali ilikuwa haijui walimu wangapi wanafundisha masomo ya Sayansi na wangapi wanafundisha katika mazingira maguku kitendo ambacho walikipinga.

  "Tulipinga hoja hizo kwa maelezo kwamba Serikali ndio yenye Shule za mchepuo wa Sayansi na inafahamu fika walimu wa Sayansi ni wangapi kwa kuwa takwimu hizo zilitolewa bungeni katika kipindi cha maswali na majibu" alisema Mukoba na kuongeza:

  Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mlugo aliliambia Bunge kuwa Serikali imetumia Sh22 bilioni kuwalipa walimu wanaofanya kazi katika mazingira magumu Sh500,000 mara moja tu wanapokwenda kuanza kazi, na kama imetambua hilo iweje isifahamu maeneo yenye kuhitaji posho ya mazingira magumu?".

  Kaimu Katibu Mkuu wa CWT, Ezekia Oluoch alitoa wito kwa wazazi na wanafunzi akiwataka kutowafikiria walimu vibaya wakati wakiwa katika mgomo huo na kitakachofanyika ni kudai maslahi yao.

  "Tunawapenda sana wanafunzi, lakini watambue kiwango ambacho Serikali inatulipa ni kidogo ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji yetu ndio maana tunaamua kugoma hivyo watuunge mkono," alisema Oluoch.


  my take!! huenda walimu safari hii wameamua???
   
 2. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  mishahara ikiongezeka na 2% itapanda!
   
 3. kbosho

  kbosho JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 4, 2012
  Messages: 12,505
  Likes Received: 3,314
  Trophy Points: 280
  tz imearibika bado kuoza2! wakiamka kudai haki zao utaskia wame tumwa na chadema!
   
 4. W

  Welu JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 815
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Mkoba acha uongo!. Nani wa kugoma? Mwalimu? Najua sarikali itakimbilia kwenye lindo lake na kukuamuru wewe utangaze kuwa mgomo haupo. Je wakumbuka kilichotokea mwaka 2007 kwemye wimbo wako kama huu? Alafu ni mgomo gani huo uitishwao wakati wa likizo?
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,197
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu utafikiri CDM ndio wanatakiwa kuboresha maslahi Yao
   
 6. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,799
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  lets wait and see!!
   
 7. paty

  paty JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,257
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  kila la kheri waliimu, tunawa support, ila mjihadhari na msitu wa pande, hakuna kutembea baada ya saa 12 jioni
   
 8. MCHONGANISHI

  MCHONGANISHI JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 363
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  this time tunaweza fanikiwa walimu wana mwamko saana hapa skuli kwetu ktk walimu 19 tuliopiga kura Jana kura ya hapana ni moja tu lazima mgomo upite kwa ASILIMIA 80, tatizo isije CWT inazingua ka 2007. Mkoba we are watching u
   
 9. Kanyapini

  Kanyapini JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 25, 2012
  Messages: 299
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sio kirahisi hivyo kwa walimu kugoma. Tangu lini mtoto wa masikini akachagua malezi?
   
 10. Kingcobra

  Kingcobra JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,008
  Likes Received: 137
  Trophy Points: 160
  Kwa nini wamechelewa hivyo kugoma? Katika kundi la watumishi linalodharauliwa kwa sasa na sirikali ni walimu. Ningekuwa mwalimu nisingeacha hali hii iendelee.
   
 11. N

  Njangula Senior Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hofu yangu tutasalitiana hasa wakati wa sensa na marking kisa pesa zisizotarajiwa.
   
 12. M

  Mbogo Junior Senior Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 198
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hii itakuwa pigo jingine. Na itakuwa habari kwa kipindi kirefu.
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  watathubutu walivyo waoga..
   
 14. Kayabwe

  Kayabwe JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 8, 2012
  Messages: 338
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nikweli walimu this time wanamwamko,Mkoba usituangushe maana walimu wengi wamepoteza imani na ww.Mgomo uwepo.
   
 15. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  lakini si shule zimefungwa,mkoba hii ni cinema au uko serious?
   
 16. Rich Dad

  Rich Dad JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 741
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Waalimu wengi hawana qualifications za kukidhi kiwango! Kama walivyo askari, wengi wao walichagu fani hiyo baada ya kukosa options zingine zaidi ya hizo kutokana na viwango vyao duni vya ufaulu. hivyo basi ni kwamba serikali inawapa fadhila tu kuwalipa hata laki 3 kwa mwezi, otherwise hawakustahili hata kumi.
   
 17. T

  TEGEMEA JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nimekwisha kuanza.
   
 18. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #18
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  my take!! huenda walimu safari hii wameamua???

  Impossible for these people to strike! Mtu wa div 4 ya point 28 hawezi kugoma. These are the most uncoordinated people! These are the kind of people who can be hired and fired at will. Their labour power is tied!
  Wana nguvu ya ajabu alkini hawawezi kuitumia maana hata viongozi wao, ni legelege! Just wait and see!

   
 19. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #19
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Mine are eyes and ears!
   
 20. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #20
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  TUSI hili....we kwenu huna ndugu mwalimu atiii?
   
Loading...