Mgomo wa Walimu Tanzania: Ripoti toka Maeneo mbalimbali ya nchi

Nipo igunga hapa mjuni kuna shule inaitwa Igunga Day nimeongea na walimu wamesema hawajaenda kazini ila kwa taarifa waliyonayo mkuu pekee ndie yuko kazini Safisana
 
DODOMA
walimu hawapo shuleni na baadhi ya shule wamerudi nyumbani kabisa
SOLIDARITY 4 EVER
 
Huku Mwanza kuna shule nyingi walimu wamehudhuria shuleni lakini wamekaa nje tu wakiwa wanaota jua.
 
Mimi naona kama vile hawa watoto wameandaliwa kufanya maandamano, nimeshangaa sana nilipokutana nayo barabarani leo asubuhi wakielekea manispaa nilipomuuliza mmojawapo akasema walimu wamegoma kufundisha kwahiyo wanaenda kudai haki yao.

Na hao wa mabango hayo mabango wamendaa saa ngapi maana mgomo umeanza leo asubuhi. Hawa watoto wameandaliwa na walimu wao kabisa.
 
Huku tabora, nimebahatika kupitia shule tano mpaka mda huu, Chemchem, Town School, Isike, Gongoni, Rufita na Kiyungi, watoto wameonekana wakicheza tu. Total chalks down.
 
Rafiki yangu ni mwalim wa halmashaur ya CHUNYA ameni-sms kuwa WAO WAMEFUNGA SHULE
 
Masasi huku kimenuka na MAAFISA ELIMU WILAYA AKIONGOZWA NA ASHA NGEDERE wanarandaranda mashuleni bila kukuta mwalimu yeyote zaidi ya WASALITI MAHEADMASTER/MISTRESS.

Karibu tutasikilizwa wadau TUENDELEE KUKOMAA. TUMEWASHIKA PABAYA
 
Huku kibaha napo kimenuka..wanafunzi wamerudi majumbani kwao..hakuna kinachoendelea!
 
mimi nimekutana wanafunzi wa shule za msingi wakiandamana hapa mtongani wametokea mbagala
 
Mimi naona kama vile hawa watoto wameandaliwa kufanya maandamano,nimeshangaa sana nilipokutana nayo barabarani leo asubuhi wakielekea manispaa nilipomuuliza mmojawapo akasema walimu wamegoma kufundisha kwahiyo wanaenda kudai haki yao. Na hao wa mabango hayo mabango wamendaa saa ngapi maana mgomo umeanza leo asubuhi.hawa watoto wameandaliwa na walimu wao kabisa.
safi thats is the final tool teachers have got......hamsisha wanafunzi waingie barabarani basi mapinduzi kwisha kazi. ukiwapiga mabomu watu wazima wanaingilia watoto wao kuumizwa then safari ya magwepande inakuwa imetimia kwa mkoba
 
Sijui taratibu za migomo Tanzania zikoje, lakini ninavyokumbuka ni kuwa kuna mambo muhimu ya kuzingatia katika migomo:

1. Serikali haina haki ya kuwazuwia wafanyakazi wa umma kugoma, ikiwa hawa watafuata sharti lifuatalo:
- Taasisi ya umma inapoamua kugoma, lazima waandae utaratibu wa kutoa huduma ya chini kwa asilimia fulani.
2. Mgomo ni hiari ya mtu, kwa hivyo vyama vya wafanyakazi havipaswi kuwalazimisha kugoma wale wasio taka, bali kutumia ushawishi wao kwa njia za kistaarabu.
3. Wale wanaoingia kwenye mgomo, wanapoteza haki ya malipo yao kwa siku watakazogoma.
4. Ikiwa mgomo utachukua muda mrefu na sababu ya 3 hapo juu, Chama cha Wafanyakazi waliogoma kina jukumu la kuwahudumia kimahitaji wale waliogoma.

Naomba anayeelewa taratibu za migomo Tanzania atufafanulie juu ya "Haki na wajibu wa mfanyakazi anayegoma."
 
Msihofu serekale itatumia wastaafu na wanajeshi kufundisha
 
Baadhi ya updates tola Lushoto ni kwamba baadhi ya Walimu wako shuleni, kweli wameniudhi sana
 
Back
Top Bottom