Mgomo wa walimu na maamuzi ya Serikali, Mahakama

Habari zilizo fika sasa hivi ni kwamba COURT OF APPEAL imefuta hukumu ya HIGH COURT na walimu sasa ruksa kugoma!

Sijui kama tutafika, hebu kumbuka migomo na migogoro ya NMB, wazee wa EAF, TRL, Wanafunzi vyuo vikuu, sasa walimu na walivo wengi kila kona ya Tz, nao.... hivi kutakalika?

Taratibu naona ile AMANI NA UTULIVU VINA YOYOMA...!

(Mod, p/se waweza iunga kwa ile ya zamani)

Safi sana hii, wakati mwingine mahakama zetu zinafanya maamuzi yenye kutetea haki za Watanzania.
 
Habari zilizo fika sasa hivi ni kwamba COURT OF APPEAL imefuta hukumu ya HIGH COURT na walimu sasa ruksa kugoma!

Sijui kama tutafika, hebu kumbuka migomo na migogoro ya NMB, wazee wa EAF, TRL, Wanafunzi vyuo vikuu, sasa walimu na walivo wengi kila kona ya Tz, nao.... hivi kutakalika?

Taratibu naona ile AMANI NA UTULIVU VINA YOYOMA...!

(Mod, p/se waweza iunga kwa ile ya zamani)

Excuse me?!

.
 
sasa wakigoma si shule zinafungwa na wote wanaamriwa kurudi nyumbani hadi waandike barua ya kuomba msamaha na kuahidi kutoshiriki migomo mingine huko mbeleni?
 
Sidhani kama sirikali inaweza kucheza igizo hilo. Wafanye hivyo ili?
 
HATIMAYE walimu sasa wanaweza kugoma baada ya kushinda rufaa yao ya kupinga amri ya muda ya kuzuiwa mgomo uliopangwa kuanza Oktoba 15 iliyotolewa na Mahakama ya Kazi Oktoba 13.

Amri hiyo ya kuzuia mgomo kwa muda ilitolewa na Jaji William Mandia aliyeeleza kuwa mgomo huo ungeathiri sekta ya elimu na hasa wanafunzi wa kidato cha nne ambao walikuwa kwenye mitihani yao ya kumaliza elimu ya sekondari.

Lakini jana, akisoma kwa niaba ya Jaji Emmanuel Rutakangwa hukumu ya rufaa ya walimu dhidi ya amri hiyo ya muda, Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufaa, Pellajia Barnabas alisema hati ya serikali iliyowasilishwa Mahakama ya Kazi haikutakiwa kupitishwa kwani ilikuwa na makosa na kwamba, mahakama ya rufaa haiwezi kuendeleza makosa hayo.

Barnabas alitaja vifungu vya sheria ambavyo serikali haikuvitumia kuwa ni kifungu cha 94 na 84 ambavyo ndivyo vyenye dhamana ya kujadili masuala yote ya migomo ya wafanyakazi na kwamba walimu wana haki.

“Jaji Mandia alitakiwa kuyatupa maombi hayo kwani makosa yalikuwa yanaonekana, lakini aliyafumbia macho... sisi hatuwezi kuendeleza makosa hayo,” alisema Barnabas kwa niaba ya Rutakangwa.

Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema amefurahishwa na uamuzi huo na kwamba, chama chake kitatoa taarifa yake leo kuhusu mustakabali wa mgomo wao.

Walimu hao waliitisha mgomo huo kuishinikiza serikali kuwalipa walimu malimbikizo ya madai yao, ikiwa ni pamoja na fedha za nauli, nyongeza za mishahara, posho na pia wanadai barua za kupandishwa madaraja na baraza la maridhiano.

Serikali imekuwa ikijitetea kuwa inaendelea kulipa walimu madai yao kulingana na kukamilika kwa zoezi la uhakiki na wiki iliyopita Waziri Jumanne Maghembe aliliambia Bunge kuwa, zoezi hilo limekamilika nchi nzima isipokuwa wilaya tatu za mkoa wa Dar es salaam na Dodoma Mjini na kwamba tayari walimu wameanza kulipwa madai yao.

Hata hivyo, Mukoba amekuwa akieleza kuwa wanaopaswa kusema kuwa wameshalipwa haki zao ni walimu wenyewe ambao wanadai na si serikali inayodaiwa.

Jana Mukoba alisema baada ya hukumu hiyo kuwa uhakiki unaofanywa na serikali na zoezi la kulipa walimu ni makosa matupu kwani upande wa madaraja hakuna haki inayotendeka na kwamba taarifa anazoendelea kuzipata kutoka kwa walimu zinaeleza kuwa wale wanaotakiwa kupewa E anapewa C.

“Hapa njia pekee ni kulipa haki zetu zote bila kubakiza kitu, vinginevyo hali haitakuwa shwari kwani imeonekana kuwa tunastahili kupewa haki zetu zote,” alisema Mukoba.

Baadhi ya walimu waliokuwa na furaha mahakamani hapo walisema chama chao sasa hakina budi kutangaza mgomo kwa kuwa walichokuwa wanakisubiri kimetimia.

“Walituzuia kugoma kwa kusema kuwa hatukuwa na sababu za msingi, sasa tayari haki imeonekana... bora tufanye kweli tumechoka... wakimaliza malipo yetu watatuita,” alisema mmoja wa walimu hao.

Majaji watatu walikuwa wanasikiliza rufaa hiyo ambao ni Jaji Emmanuel Rutakangwa, Nathalia Kimaro na Benard Luanda.

Walimu wanatetewa na Gabriel Mnyele na Mabele Marando, wakati Wakili wa Serikali ni Donald Chidowu.

Ninapata shaka na taratibu za huu mgomo wa walimu, hasa kwa muda uliopangwa kuanza, ninachoona hapa walimu wamedanganywa, ikiwa kati wanafahamu baadhi au wote hawafahamu. wamesema mgomo wao utaanza jumatatu, na utakwenda mpaka mwakani, hapa haijaeleza mwakani mwezi gani, inawezekana ikawa ni mwakani mwezi wa januari. sasa kwa jinsi ninavyo fahamu ni kuwa kuanzia mwezi desemba mwanzoni hadi januari mwishoni shule huwa zimefungwa, kwa maana nyingine wanafunzi wanakuwa hawapo shuleni. na ninavyoelewa ni kuwa mgomo wa walimu ni kugoma kufundisha. sasa huo mgomo utakuwa unamaana gani ikiwa hauna madhara katika mnalogomea? kwani ili mgomo uwe na maana ni kuona wanafunzi hawafundishwi, ila kwa hapa wanafunzi wapo likizo
 
Katibu Mkuu Kiongozi amewapiga mkwara mzito leo. Amesema kuwa hukumu ya mahakama ya rufani haifanyi mgomo wao kuwa halali. Anasema serikali inakamilisha malipo na hadi kufikia mwisho wa mwezi huu walimu watakuwa wamelipwa.
Amewaonya kuwa mwalimu atakayegoma, mshahara wake akachukue kwa yule aliyemtaka agome.
Serikali pia imekwenda mahakamani kutaka hukumu ya Mahakama ya Rufani ipitiwe upya.
Picha inaanza sasa
 
Jana nimeona kwenye habari Pinda yuko huko dodoma kwa ziara.Wananchi wanaonekana bado wanazo zile Tshirts za CCM 2005 zenye picha ya Kikwete wakati wa uchaguzi zinaonekana bado mpyaaaa! Tunahitaji kuelimisha vijijini maana ndipo uliko mtaji wa CCM
 
Ni kweli. Lakini hata mjini wako ambao bado naona wanavaa tshirt za ccm.
Wengine wanazivaa kwa kukosa nguo si kwamba wanashida ya kuipenda ccm.
Tuwakumbushe kwamba pamoja na kuvaa tshirt zao hizo matatizo yao yanaanzia kwa waliowapa tshirt na vikanga.
Ili wakomboke kwa shida hiyo wavae kanga na wasitoe kura.
 
sasa kama serikali imeamua kutowalipa mishahara waliogoma, mahakamani inakwenda kufanya nini tena. sana sana serikali inataka mahakama ya rufaa ifanye review ya uamuzi wake. na hii haiwezi kufanyika kesho jumapili.

haabari za sasa hivi zinasema walimu wamelipwa madeni yao yote leo kupitia halmashauri za wilaya zao!!

macinkus
 
Aisee hii nchi yetu kweli ni ya kimabavu. Yaani hata kugoma pia inabidi umuombe kibali unayemgomea...akikataa...? Ndo ukaze buti uufyate na kuendelea kuburuzwa.....
Taanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wotee....!!
 
We wacha tu,kila msimu ukifika waipigie kura CCM ,hao si ndio wanokusanywa kwenye mikutano pamoja na polisi na majeshi na wenginetele na kuipigia debe CCM sasa wanagoma nini wahendelee tu kuchapa mzigo , hizo ndizo fazila wanazolipwa na Serikali ya CCM.
Tena wahalakishe kulipwa na Serikali hiyo yao ya CCM ,wanaume wakiingia Ikulu hesabu inaanza upya,kama ulikuwa unadai basi kaidai serikali iliyopita ikiwezekana wafungulie mashtaka waliokuwa na serikali hiyo iliyopita ili wakulipe feza yako ,mpo.
 
Katibu Mkuu Kiongozi amewapiga mkwara mzito leo. Amesema kuwa hukumu ya mahakama ya rufani haifanyi mgomo wao kuwa halali. Anasema serikali inakamilisha malipo na hadi kufikia mwisho wa mwezi huu walimu watakuwa wamelipwa.
Amewaonya kuwa mwalimu atakayegoma, mshahara wake akachukue kwa yule aliyemtaka agome.
Serikali pia imekwenda mahakamani kutaka hukumu ya Mahakama ya Rufani ipitiwe upya.
Picha inaanza sasa

Kweli picha inaanza sasa. Starring Govt Tz and CWT? Au siyo? Tena hapa serikali ina hidden agenda. Eti inadai inalipa na huku ikiweka rekodi ya waliogoma ambao hawatalipwa which is very cheap method to act as an enemy wakati unadaiwa. Dawa ya deni ni kulipa hata serikali hili imelisahau? Inashangaza sana ujue!! Tumekwisha watanzania nasema tumekwisha.

Ukianalyse nchi nzima sasa imegoma au inaanza kupata enzymes za kugoma na hata watafika mahali sukari ikipanda tutagoma na hapo ndio demokrasia ya kweli na freedom of speech itakuwa imefikiwa
 
CCM watishika na migomo ya waalimu washawisi serikali kuikomesha
Na Jackson Odoyo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka serikali iwachukulie hatua za kisheria viongozi wa Chama cha Walimu nchini (CWT), kikidai viongozi hao wana agenda ya siri ya kutaka kuharibu utulivu na mshikamano wa nchi kwa kuhamasisha migomo ya walimu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana ofisini kwake jijini Dar es Salam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itifaki na Uenezi, John Chiligati alisema Serikali inapaswa kuwashughulikia viongozi hao na kwamba, ina haki ya kufanya hivyo kwa sababu ndiyo mwajiri wao.

''Serikali kama mwajiri wao ina haki kuwashughulikia viongozi wa Chama cha Walimu wanaohamasisha mgomo huu kwa kuwa, wana agenda ya siri ya kuharibu utulivu na mshikamano wa nchi yetu, serikali isiwaonee huruma,'' alisema Chiligati.

Alisema CCM imeshangazwa na kauli ya Rais wa CWT ya kuitisha mgomo usio na ukomo wa nchi nzima, wakati uhakiki wa madeni ya walimu umekamilika na wataanza kulipwa kunzia leo.

“Katika mazingira haya tunajiuliza mgomo huo una nia gani hasa wakati kile Walimu walichokuwa wanakipigania sasa kimepatikana, tunajiuliza mgomo wa nini na hao wanaopigania mgomo uanze kesho (leo) nia yao ni ipi?,” alihoji Chiligati.

Hata hiyo Chiligati alisema CCM inawasihii na kuwashauri Walimu wenye nia safi kutojiingiza katika mgomo huo aliosema una nia mbaya na badala yake waendelee na kazi.

Aliongeza kuwa kitendo cha Walimu hao kuingia kwenye mgomo huo batili na haramu kwa kuwa malengo yake ni kuumiza watoto na kuingiza wasiwasi ndani ya nchi bila ya sababu za msingi.

Katika hatua nyingine Chiligati alisema kwamba, iwapo kuna mtu yeyote mwenye ushahidi kuwa Tanil Somaiya anahusika na tuhuma za rushwa ya rada pamoja na kukwepa kodi za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) apeleke ushahidi huo katika vyombo vya dola.

''Somaiya alitoa Sh400 milioni kwa ajili ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM utakaofanyika Desemba 16 mwaka huu Mjini Dodoma. Tumepokea msaada huo kwa mikono miwili na ilifanyika hadharani pasipo kificho, wala si kweli kwamba CCM inapokea fedha zilizopatikana kwa njia haramu na wala si ishara ya kukumbatia ufisadi,'' Chiligati alisisitiza.

Wakati huohuo, Chiligati alisema CCM imesikitishwa na namna ambavyo viongozi wa vyama vya upinzani walivyokipaka matope chama hicho kupitia sakata la Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA)

Alisema ukweli ni kwamba, CCM haikuchukua fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuongeza kuwa iwapo katika orodha ya watuhumiwa wa EPA wapo wana CCM au wakereketwa wake, walifanya hivyo kwa maslahi yao wenyewe na wala hawakutumwa na chama hicho.

Source: Mwananchi.

Hivi kweli kiongozi (Chiligati) tena senior katika chama kutoa maoni, ushauri au maelekezo kama hayo kwa serikali si kuhatarisha amani nchini!! Walimu wanadai haki yao, leo hii kiongozi wa chama kinachoongoza serikali kutoa madai kama hayo ya kuwashughulikia viongozi wa CWT ni ukosefu wa busara na fadhila kwa walimu wetu. Na hii isiangaliwe kwa CWT pekee, kutakuwa na vyama vingine ambavyo vinawaunganisha wafanyakazi wengine nchini ambavyo navyo vitapewa vitisho vya namna hiyo ili visidai haki yao.
Kisieleweke kitu hadi haki itakapopatikana.

Kumshughulikia Mkoba (Rais wa CWT) hakitasaidia lolote bali itaamsha chuki zaidi ya walimu dhidi ya serikali. sasa hapa nani atakuwa auamia.....ni wanafunzi ambao wanapaswa kupewa haki yao ya msingi (ELIMU). Muda wa kutishiana umepitwa na wakati, serikali inawajibu wa kutoa haki kwa hawa walimu, waliokuwa wafanyakazi wa EAC na wengine. Tuache mambo ya kuburuzana na kupeana vitisho, kisa kudai HAKI

mi nwashauri walimu wagome tu maana mimi ya EAC imenipa fundisho kubwa sana hii serikali yetu imezoea kutudanganya kama mtoto si unajua mtoto anavyolilia nguo dukani then unampa pipi asilie ndo hivyo wanavyofanya watawalipa vihela vidogo vidongo watadanganya wengine walikuwa vibaruana wengine vyeti vyao ni feki alimradi mchezo uishe kwa penati, sasa wao wagome tu baada ya muda na sisi wenye watoto wetu wanaosoma izi shule za kina kanumba tutaandamana mpaka ikulu kumuuliza rais watoto wetu itakuwaje kama atawaombea kwa muda Mzizimz au Almutazin, STmary's poa lasivyo tubaki nyumbani kufundisha watoto wetu tusiende kazini maana utendaji utakuwa hafifu na kufukuzwa kazi siku hizi ni kama kunywa maji, hapo basi uchumi utazidi kudidimia na watu wataamua kuingia msituni, wakirudi huko na wawekezaji mnaowaheshimu kama miungu watakimbia ahh hii movie ni nzuri mno
 
duh umeona mbali sana,ni kweli kabisa hizi ni mbinu shetani anatumia anampiga mchungaji na kondoo wanatawanyika.na huo ndo utakuwa mwisho wa story.Naiomba serikari ikae na cwt kwa utaratibu sio kuwachukulia hatua viongozi ikifanyika kiustarabu haitaleta madhara vinginevyo walimu wanaweza kuleta fujo kubwa.
 
CCM watishika na migomo ya waalimu washawisi serikali kuikomesha
Na Jackson Odoyo

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka serikali iwachukulie hatua za kisheria viongozi wa Chama cha Walimu nchini (CWT), kikidai viongozi hao wana agenda ya siri ya kutaka kuharibu utulivu na mshikamano wa nchi kwa kuhamasisha migomo ya walimu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana ofisini kwake jijini Dar es Salam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itifaki na Uenezi, John Chiligati alisema Serikali inapaswa kuwashughulikia viongozi hao na kwamba, ina haki ya kufanya hivyo kwa sababu ndiyo mwajiri wao.

''Serikali kama mwajiri wao ina haki kuwashughulikia viongozi wa Chama cha Walimu wanaohamasisha mgomo huu kwa kuwa, wana agenda ya siri ya kuharibu utulivu na mshikamano wa nchi yetu, serikali isiwaonee huruma,'' alisema Chiligati.

Alisema CCM imeshangazwa na kauli ya Rais wa CWT ya kuitisha mgomo usio na ukomo wa nchi nzima, wakati uhakiki wa madeni ya walimu umekamilika na wataanza kulipwa kunzia leo.

“Katika mazingira haya tunajiuliza mgomo huo una nia gani hasa wakati kile Walimu walichokuwa wanakipigania sasa kimepatikana, tunajiuliza mgomo wa nini na hao wanaopigania mgomo uanze kesho (leo) nia yao ni ipi?,” alihoji Chiligati.

Hata hiyo Chiligati alisema CCM inawasihii na kuwashauri Walimu wenye nia safi kutojiingiza katika mgomo huo aliosema una nia mbaya na badala yake waendelee na kazi.

Aliongeza kuwa kitendo cha Walimu hao kuingia kwenye mgomo huo batili na haramu kwa kuwa malengo yake ni kuumiza watoto na kuingiza wasiwasi ndani ya nchi bila ya sababu za msingi.

Katika hatua nyingine Chiligati alisema kwamba, iwapo kuna mtu yeyote mwenye ushahidi kuwa Tanil Somaiya anahusika na tuhuma za rushwa ya rada pamoja na kukwepa kodi za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) apeleke ushahidi huo katika vyombo vya dola.

''Somaiya alitoa Sh400 milioni kwa ajili ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM utakaofanyika Desemba 16 mwaka huu Mjini Dodoma. Tumepokea msaada huo kwa mikono miwili na ilifanyika hadharani pasipo kificho, wala si kweli kwamba CCM inapokea fedha zilizopatikana kwa njia haramu na wala si ishara ya kukumbatia ufisadi,'' Chiligati alisisitiza.

Wakati huohuo, Chiligati alisema CCM imesikitishwa na namna ambavyo viongozi wa vyama vya upinzani walivyokipaka matope chama hicho kupitia sakata la Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA)

Alisema ukweli ni kwamba, CCM haikuchukua fedha katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na kuongeza kuwa iwapo katika orodha ya watuhumiwa wa EPA wapo wana CCM au wakereketwa wake, walifanya hivyo kwa maslahi yao wenyewe na wala hawakutumwa na chama hicho.

Source: Mwananchi.

Ebu jamani angalieni viongozi wanao mshauri rais wetu ndio kama hawa wakina Chiligati. Wamejaa ideology za kijeshi na wao kila kitukwao wanaona ni rahisi kufanya.
Sasa wanashauri serikali ambayo wao hao hao ni sehemu yao kwamba wawachukulie hatua viongozi wa chama cha walimu. Je wanadhani hiyo itanyamazisha walimu?
Wajaribu waone jinsi nchi itakavyoendelea kutikisika na hasa kwa mgomo mkubwa katika nchi kuliko waliowahi kuona.
Kama wana ushauri mzuri basi wajishauri ( Maana na yeye ni sehemu ya hiyo serikali) kulipa malimbikizo ya mishahara ya walimu na wafanya kazi wengine na wasije na vitisho maana watanzania wa leo hatuogopi tena vitisho.
Wao si Mungu lakini wanaweza kutawala kwa shida maana watawaliwa wamefika mwisho wa uvumilivu.
Nchi hii tunahitaji viongozi lakini kama ni viongozi kama Chiligati basi tumekwisha.
 
1. Mara zote mfanye mwalimu mwoga kwa chama na serikali.
2. Mlaghai kwa wito na si kipato.
3. Mfundishe kuwa mpole asidai haki.
4. Mfanye asiajiriwe sekta nyingine ili umtumie.
5.Mlipe kidogo atumike milele.
6. Mtumie kwenye chaguzi na sensa, ajione bora.
7. Msifie kila siku, avimbe kichwa.
8. Weka viongozi wa CWT asifurukute.
9. Mtumie kama ubao wa matangazo kwa t-shirts za chama.
10. Mara zote wagawe na kuwatawala.

I am very opmistic kuwa siku zinahesabika, walimu watazibanjua amri zote, wameshaanza kuzibanjua baadhi kama ya 1, 3 na ya 8! Zote zitabanjuliwa!
 
sasa wakigoma si shule zinafungwa na wote wanaamriwa kurudi nyumbani hadi waandike barua ya kuomba msamaha na kuahidi kutoshiriki migomo mingine huko mbeleni?

Mkjj mgomo huu ni wa walimu wa mijini tu, Vijijini walimu wanamgomo wao tangu enzi za Mwinyi ila hautangazwi rasmi kwani wanahabari hamfiki huko, wao wanachojua ni Kilimo kwa kwenda mbele, Kimpumu Kangara,Rubisi,Ugimbi,Mbege, Pingu kwa kwenda mbele na inapofika mwisho wa mwezi ....wilayani wanachukua kamshahara kao wanarudi kijijini bila kelele kama hao wa mijini
 
Back
Top Bottom