Mgomo wa walimu na maamuzi ya Serikali, Mahakama

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Mahakama Kuu kitengo cha kazi imezuia kufanyika kwa mgomo wa walimu uliopangwa kuanzi Jumatano. Amri hiyo ilitolewa kutokana na kesi iliyofunguliwa na serikali leo asubuhi, ikiitaka mahakama kuuzuia mgomo huo kwa kuwa si halali.

Aidha, Chama Cha Walimu kimetakiwa na mahakama kutoa matangazo kwenye vyombo vya habari kesho kuwatangazia walimu kuwa mgomo haupo.

Inanikumbusha sakata la mgomo wa NMB
 
Habari niliyoipata punde, Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mkoba amenusurika kipigo kutoka kwa watu wanaosadikiwa kuwa ni walimu, baada tu ya kuwatangazia matokeo ya mahakama kusimamisha mgomo wao unaotarajiwa kuanza kesho. Naomba walio nyumbani watupe habari zaidi ya nini kilichojiri.
 
Habari niliyoipata punde, Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Gratian Mkoba amenusurika kipigo kutoka kwa watu wanaosadikiwa kuwa ni walimu, baada tu ya kuwatangazia matokeo ya mahakama kusimamisha mgomo wao unaotarajiwa kuanza kesho. Naomba walio nyumbani watupe habari zaidi ya nini kilichojiri.

Hao walimu vipi? mshenga huo hauawi wengeenda kumpiga jaji alietoa hiyo injuction
 
Walimu watwangana Dar
Maulid Ahmed
Daily News; Tuesday,October 14, 2008 @20:00

Viongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), jana walivamiwa na kupigwa na walimu wa Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kutangaza kuwa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi imesitisha mgomo wao uliopangwa kufanyika leo nchi nzima.

Vurugu hizo za walimu kugeuka mbogo na kuwashambulia viongozi wao zilianza baada ya Rais wa CWT Taifa, Gratian Mukoba, kuwatangazia walimu waliokusanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee kwa ajili ya uzinduzi wa mgomo huo kuwa sasa haupo.

Ilibidi polisi wafyatue risasi hewani ili kutuliza vurugu hizo ambazo zilianza kuenea hadi barabarani. Mukoba ambaye wakati anaanza kuwahutubia walimu na kuwaeleza kuwa mwanasheria wao anakusudia kuwasilisha rufaa katika Mahakama ya Rufaa, alizomewa na walimu hao na alipowaeleza kuwa mgomo kwa sasa hautakuwapo hivyo wawe watulivu.

Mara alishtukia chupa za maji zikitoka kila pembe ya ukumbi huo na kuelekezwa katika meza kuu walikokaa viongozi wa chama hicho wa Taifa na Mkoa wa Dar es Salaam.

Walimu waliokuwa na jazba mbali ya kutupa chupa pia walianza kurusha viti kuelekea jukwaa la viongozi na kusababisha mkutano huo kuvunjika majira ya saa 6:17 mchana huku wengine wakizomea na kutoka nje.

Wakati hayo yakiendelea walimu wengine waliamua kuvamia meza kuu na kuvunja meza hali iliyosababisha viongozi waliokuwa wameketi hapo kukimbia na kujibanza pembeni huku wakilindwa na askari kanzu.

Miongoni mwao waliovamia meza kuu, walitoweka na simu ya Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Mwanza aliyefahamika kwa jina moja la Raphael ambaye alihudhuria mkutano huo kuwapa salamu za watu wa Mwanza na kuonyesha wanawaunga mkono katika mshikamano wao.

Walimu hao wakati wanafanya mashambulizi walisikika wakisema ‘chama kivunjwe'; ‘Mukoba umetusaliti jiuzulu'; ‘kesho (leo) tunagoma'.Wakati wanaendelea na vurugu hizo huku wengine wakijiangusha chini na kulia na kutoa kauli kali dhidi ya viongozi wao, ghafla mwalimu mmoja alichukua kipaza sauti na kuwaita wenzake ndani huku akiwaeleza mgomo upo pale pale hali iliyowarudisha baadhi ya walimu ukumbini ambapo baada ya kufika walianza tena kushambulia jukwaa kuu wakati huo meza na viti vikiwa vimeshaparaganyika.

Ilipotimia majira ya saa 6:45 mchana na kuona viongozi hao hawatoki ukumbini, walimu wengi wao waliokuwa nje ya ukumbi wakiimba walianza kurusha mawe juu ya bati la ukumbi huo ambapo baada ya dakika chache magari manne ya Polisi yaliwasili eneo hilo.

Gari moja liliegeshwa katika mlango wa nyuma wa ukumbi huo na polisi waliokuwamo ndani baada ya kuona walimu wanazidi kurusha mawe walifyatua risasi tano hewani kuwatawanya walimu na kutumia muda huo kuwaondoa Mukoba na Makamu Mwenyekiti wake, Honoratha Chotanda.

Baada ya viongozi hao kuondoshwa eneo hilo, walimu waliendelea na vurugu huku wakiimba na kucheza katikati ya barabara na kusimamisha magari mengine huku wakiwaimbia ‘kama sio juhudi zetu walimu, madereva mngesoma wapi'; ‘mnanunua magari ya ufisadi na kutumia fedha zetu'; na nyingine zenye mwelekeo wa kisiasa.

Kama hiyo haitoshi walimu walivamia gari la Polisi lenye namba T 210 AMV na kulizunguka huku wakiwaimbia ‘kama sio juhudi zetu walimu polisi mngesoma wapi ?' huku wakilisindikiza gari hilo lililoingia ndani ya ukumbi kwa kupitia mlango wa mbele na kuwachukua viongozi wengine waliobaki wa CWT.

Wakati gari hilo linatoka lilirushiwa chupa za maji lakini polisi hawakujibu mashambulizi. Baada ya viongozi hao kuondoka walimu hao waliendelea kuimba na walianza kuondoka kwa makundi.

Awali walimu hao wakati wanaanza mkutano wao majira ya saa 4:00 asubuhi walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kumtukuza Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere na kuonyesha picha yake kuwa alikuwa mtetezi wao.

Mbali na hizo waliimba nyimbo nyingine kuonyesha kuwa wao ni muhimu na kumshutumu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe kwamba; ‘Kama sio juhudi zetu walimu, Maghembe ungesoma wapi'; Hakuna kulala hadi kieleweke'; walimu ndio sisi tunaotegemewa kuleta maendeleo katika nchi'.


Hata hivyo hali katika ukumbi huo ilianza kubadilika aliposimama Mwenyekiti wa CWT wa Mkoa wa Mwanza na kueleza kuwa watalazimika kuacha mgomo kwa sababu ya amri ya Mahakama ila baadaye wataweza kulizungumza hilo, ndipo akaanza kuzomewa akitakiwa kukaa.

Aliposimama Naibu Katibu Mkuu, Ezekiah Oluoch na kutaka kuzungumzia juu ya tuhuma za ufisadi kuhusu jengo la Mwalimu House, ghafla alisimama mwalimu mmoja na kumtaka akatishe kwani hiyo haikuwa mada ya mkutano wao.

CWT ilitoa notisi ya kukusudia kugoma Oktoba 15 lakini Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi juzi iliamuru kusitishwa kwa mgomo huo baada ya serikali kuwasilisha mahakamani hapo hati ya zuio la mgomo.

Walimu hao walikusudia kugoma hadi hapo serikali itakapotekeleza madai yao ikiwamo kuwalipa malimbikizo ya mishahara, posho za uhamisho, kujikimu, usafiri na upandishaji wa madaraja.
 
Hiyo ni positive kwani msg inaenda kwa serkali kuwa mgomo si invention ya viongozi wakiwa pump walimu wagome. Ukweli ni kuwa walimu wamechoka kuonewa. Hata ukiwanyamazisha viongozi wa walimu bado kelele itakuwa palepale.
 
ina maana serikali ilikimbilia mahakamani, kama wanaona kuwa walimu wanakosea kwanini wasiwafukuze kazi, otherwise lazima wawalipe pesa yao wanayodai.

Ilikuwaje kwani serikali ilisema itawalipa kabla ya september kuisha, kwanini hawakuwalipa mpaka wakaamua kukimbilia mahakamani.
 
Kibaya zaidi ni kwamba hata kama mgomo rasmi haupo, walimu tayari wako katika mgomo usio rasmi kutokana na kulazimika kufanya kazi katika hali ya kusononeka na kukosa motisha. Pengine serikali ingeelewa ni bora kukosa kabisa waalimu kuliko kuwa na walimu waliokata tamaa kiasi hiki, maana hawawezi kuifanya hiyo kazi ya kufundisha. Hivi ukimlazimisha mwalimu aingie darasani, na akaingia kweli lakini bila kufundisha, kuna faida gani hapo? Wapo walimu wengi wanakubali kazi ili wapate tu "anwani", mahali pa kupatikana iwapo kuna "dili", na wala si kwa kupenda kazi. Ile kuweza kusema "mimi ni mwalimu, niko Azania pale", inamtosha mtu kuagizia wanaotaka huduma zake kumfuata pale kwa ajili ya mapatano! Sasa hiyo "anwani" ya Azania mwalimu atailipia kwa kufundisha vipindi vichache, vingine anavunga visingizio kibao, apate muda wa "dili" zake. Na hii ndio sababu sehemu ambako hakuna "dili" waalimu hawaendi, wako tayari kubangaiza Dar kwa kuanzisha "vituo vya tuisheni" kuliko kwenda huko Simanjiro na kwingineko kwa namna hiyo. Na siku hizi vijana wanavyofeli mitihani ya form 4 na 6, imekuwa kama neema kwa wale walimu "machinga", wanapata "madili" ya kufundisha wanaotaka kurudia mitihani! Matokeo yakitoka tu jamaa wanaanza kubandika matangazo makuuuubwa ya kuvutia wateja wa "kurudia mitihani". Mtaji wake: chumba kimoja alichokodi au kiambaza cha nyumba, turubali na ubao. Mtu anatengeneza hela tu (hiyo biashara siku hizi Dar hata wasio waalimu wanaichangamkia sana, wewe ukijua tu hesabu mbili tatu za "quadratic equation" fungua banda lako, utashangaa wateja wanavyomiminika!). Sasa yote hii inashusha viwango vya elimu, na kiini chake kwa sehemu kubwa ni kutokana na kupuuza walimu hadi wanafikia kiasi cha kupoteza kabisa ule motisha wa kufundisha mashuleni, wanaishia "kuganga njaa" tu. So pitiful!
 
ina maana serikali ilikimbilia mahakamani, kama wanaona kuwa walimu wanakosea kwanini wasiwafukuze kazi, otherwise lazima wawalipe pesa yao wanayodai.

Ilikuwaje kwani serikali ilisema itawalipa kabla ya september kuisha, kwanini hawakuwalipa mpaka wakaamua kukimbilia mahakamani.

Nakumbuka siku si nyingi kuna kiongozi wa serikali aliongelea kuhusu mapendekezo ya kubadilishwa sheria ya "injunction" baada ya wafanyabiashara ya mafuta kwenda mahakamani kupinga kuzuia kufanya biashara ya mafuta na EWURA baada ya kubainika kuwa wanachanganya mafuta ya petroli na vitu vingine.

Leo naona serikali hiyo hiyo imetumia sheria hiyo hiyo kuzima mgomo wa walimu, then sijui kama kuna marekebisho yatafikiriwa tena au wakibadilisha itakuwa zaidi kuibeba serikali.

Ila kwa kweli walimu miaka hii wanadhalilika vya kutosha na sijui kitu gani kitakuja kuibadilisha hii profession iwe na heshima yake tena.
 
Nasikia zuio la Mahakama ni batili kisheria maana limefanyika nje ya masaa ya kazi hivyo walimu hawafungwi nalo. Wajuvi wa sheria kuna ukweli wowote kuhusu hili? Tuelimishane.
 
si mara ya kwanza injuction order kutolewa nje ya muda wa kazi, katika ile kesi ya kusimamisha ucgaguzi wa meya kitwana kondo ilifanyika hivyo hivyo, jawabu nikuwa je mtu wa kawaida anaweza kupata huduma hii chaP CHAP KAMA SERIKALI ILIVYOIPATA HATA BAADA YA MASAA YA KAZI?
 
kazi kweli kweli jamani jamii yote ya tanzania inaangukia kwa walimu tutate tusitake kwa nini madai yao yasifanyiwe kazi mara moja nao wakaishi kwa amani na kuendeleza kazi yao ya maana..?
 
Walimu wamechoka, ukiwaangalia unaona machungu waliyonayo. hicho ni kielelezo kimojawapo cha hali na hisia walizonazo WaTZ kuna wengi ambao wako kwenye sekta zisizo rasmi hawana sababu ya kugoma ila wanamachungu sana. Kweli walimu hawathaminiwi na Raisi wao ameshindwa kuwa kiongozi wakati muhimu HAFAI. hakuna haja ya kuwa na kiongizi wa raha tu hasa kwenye vyama vya kutetea haki. WALIMU ALUTA KUNTINUA NA SISI WANANCHI TUNAWAUNGA MKONO
 
Migomo ni suluhisho la matatizo? Je haki za walimu zitapatikana kwa migomo? Nimesikiliza vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na sakata la madai ya walimu. Ninashindwa kuelewa madai ya walimu ni ya haki au la? Sidhani kama walimu ni wajinga wadai kitu ambacho si haki yao. Kilimanjaro nimesikia wahusika wa malipo ya walimu walikuwa wakihaha kuhakikisha walimu wanalipwa ili wasigome. Na pia kutishiwa wasigome. Ina maana serikali ni lazima iamshwe ndio ilipe haki za walimu?

Umefika wakati sasa wa kuwa na utaratibu wa kuhakiki haki ya kila mfanyakazi wa serikali na kulipwa kwa wakati na kwa haki yake. Kwa technologia iliyopo sidhani kwamba ni vigumu kutatua haki za walimu. Unajua mwalimu akienda likizo anatakiwa kulipwa nini na nini halipwi. Itengenzwe programme amayo ukiikomand inatoa kiasi cha kila mwalimu. Wanaofanya mahesabu ya malipo ya walimu kazi yao ni ipi.

Swali: Migomo ina madhara kwa nchi na kidunia?
 
Mi nadhani hata kama mahakama imetoa zuio la mgomo wao waendelee kugoma tu kwani watawafanya nini? Najua hata jeuri ya kuwafukuza kazi hawana kwani hao walimu wa kuziba hizo nafasi hata nusu yake hawatapatikana......Walimu wana hali mbaya sana jamani tuache utani nadhani hata ile morali ya kazi hawana tena.
 
uongozi kazi jamani acheni tu... angalia hizi picha
 

Attachments

  • mkoba.jpg
    mkoba.jpg
    5.9 KB · Views: 114
  • mkoba2.jpg
    mkoba2.jpg
    6.6 KB · Views: 106
Hizo ni salamu za rasharasha. Kipanya wa Mwananchi sijui umekumbuka pia kumpelekea Vasco kama ile barua ya jana. Watu wamechoshwa na usanii na wameanza kufanya kweli kweli. Hakuna kulala tena mpaka kieleweke.
 



Asante kwa hizo picha.
Alipigwa jiwe, au ilikuwaje. Ni dhahiri alikuwa ananusuru maisha yake



.

Ama kweli, ukistaajabu ya Musa, utaona ya Firauni. Hizi zote zinaonyesha dalili za kazi nzuri na kukubalika kwa Serikali iliyoko madarakani (nukuu kutoka Mkurugenzi wa habari ikulu). Tunapofikia mahali ambapo kula kukicha ni migomo, maandamano, vurugu, kufungia magazeti, kuwapiga raia, kuzuia msafara wa rais, kupigwa kwa viongozi wa kisiasa, kupigwa kwa viongozi wa vyama vya wafanyakazi, kuzomea viongozi wa serikali. Hali ina tisha. Hapa tunatakiwa kusema, simama, tafakari. wapi tumepotoka, turekebishe au tuanze upya.

Hapa naona kuna kitu kimoja kikubwa, KUKATA TAMAA. Hali iko kama vile umefumwa na unaambiwa ukisimama nitakuuwa kwa UPANGA, na ukikimbia nitakuuwa kwa MSHALE. Vyote hivi ni vifo, hakuna kupona. Wananchi wamechoka, sasa hawaoni nani msaada wala kimbilio liko wapi. Ni kazi kubwa sana kuwatawala watu walikata tamaa. Hatuwezi kuwahimiza waalimu kuendelea na moyo wa kazi wakati wamekata tamaa.

Mimi nadhani serikali ya Kikwete itafakari na kutenda kwa kasi waliosema watakuwa nayo na isiwe kasi ya kuwatetea mafisadi. Ukweli watanzania sasa wanaujua. Kuwa linapokuja suala la wanyonge, serikali inatafakari, ila likija suala la MAFISADI, serikali inaliangalia kwa makini isije IKAVUNJA HAKI ZA MSINGI ZA WATU (JK). Hapa unajiuliza wao waalimu waendelee na halii hii hadi lini?

NI BORA WAKIMBIE wafe kwa MSHALE, kuliko wasimame wafe kwa UPANGA.
 
Waalimu wengi uchaguzi wa 2005 walionyesha mwamko wa mageuzi, wengine wakaenda kugombea udiwani kupitia vyama vya upinzani. Walitiwa moyo sana na waalimu wenzao.

Tunachokiona leo ni kulipiza kisasi. Nasikia JK ni bingwa wa visasi.




.
 
Hizi ni habari kwao na hao wenye ndoto za kuongoza nchi hii kwamba watu wamechoka na usanii.watu wamechoka na maneno yasiyo ambatana na vitendo.Safari ndo kwanza imeanza na watu ndo tunazidi kuchanganyikiwa.
 
Back
Top Bottom