MGOMO WA WAFANYAKAZI WOTE TAREHE 15.08.2012 Mgaya kufunguka

Mwanaharakatihuru

JF-Expert Member
Mar 21, 2012
477
120
Katika sakata dhidi ya serikali na wafanyakazi Mgaya kutoa neno hivi karibuni lakini taarifa za ki intellegensia zinasema kuwa tarehe 15 ndio siku pendekezwa.

Madai pendekezwa:
Maslahi kiduchu
PAYE ipunguzwe
Sheria kuhusu mafao ya kujitoa ibadilishe kipengele cha miaka 55 au 60 hadi miezi miwili.
Serikali iwajibishe polisi kuhusu uchunguzi wa kipigo cha dr Ulimboka
Huu ni upepo tu
 
Na mwaka huu mpaka wakome au la wakimbie nchi hii hawa ccm maana nchi imewashinda kabisa
 
Jamani hiyo tarehe 15,mm naona kama mbali.....hivi waliangalia na vigezo vya WHO ambavyo vinasema kiwango cha maisha kwa Wananchi wa TZ kimeshuka hadi kufikia miaka 45?
 
Nasikia harufu ya damu...sichochei vurugu ila naona vurugu inakuja TZ yaweza geuka Rwanda..sijui..siamini, muulizeni rais Kiwete
 
Nasikia harufu ya damu...sichochei vurugu ila naona vurugu inakuja TZ yaweza geuka Rwanda..sijui..siamini, muulizeni rais Kiwete
..
Hizi zama Za dot com mwananchi huyu anaongelea vurugu.. Kijamii, kisiasa, kijiografia kidini wala kimila si rahisi TZ IKAKUNJIKA NA KUINGIA KWENYE UMWAGAJI WA DAMU WA AINA YOYOTE,. Wewe uliona wapi, baba Chaka tofauti Na mama, makabila tofauti, dini tofauti saa ngapi chokochoko ya kihasimu itazuka, ni kimbunga tu cha kuwang'oa mafisadi Na Mbona watang'oka..
 
Hii serikali inachezea watumishi..ngoja tugome tu tuone watafanya nini.
Ila ni vyema hili likafanyika mapema
 
Katika sakata dhidi ya serikali na wafanyakazi Mgaya kutoa neno hivi karibuni lakini taarifa za ki intellegensia zinasema kuwa tarehe 15 ndio siku pendekezwa.

Madai pendekezwa:
Maslahi kiduchu
PAYE ipunguzwe
Sheria kuhusu mafao ya kujitoa ibadilishe kipengele cha miaka 55 au 60 hadi miezi miwili.
Serikali iwajibishe polisi kuhusu uchunguzi wa kipigo cha dr Ulimboka
Huu ni upepo tu

Kwa kweli wakati mwingine serikali na wabunge wake tena wasomi kabisa wengine ni ma-doctor, maprofesa, na ma-graduates wengine, wanapitisha sheria ya mbunge kulipwa mafao baada ya miaka mitano ya ubunge. Mfanyakazi mwingine ili alipwe mafao yake na NSSF, n.k, lazima afikishe at least miaka 55. Hivi life expectancy ya mtanzania ni miaka mingapi? Je, ni miaka 60, kweli? Be careful! wananchi wakichoka, sijui kama viogozi hamtakimbilia ughaibuni. Maana nikikumbuka ya akina Hosni, Muamar, na wengine wengi, kama yanainyelea nji yetu, vile!!
 
katika jambo ambalo limenigusa katika uongozi wa jk ni hili la mafao.tutaandamana hata tukiwa uchi hatukubali hata kidogo.
 
Tarehe 15 ni mbali sana bana. angalau ingekuwa tarehe 6 August basi, wiki hii tuwaache walimu wajiachie.
 
katika jambo ambalo limenigusa katika uongozi wa jk ni hili la mafao.tutaandamana hata tukiwa uchi hatukubali hata kidogo.
Nilidhani mmeshaandamana kumbe mtaandamana? Lini? Au ku-post hapa ndio maandamano menyewe? Watz kwa porojo? Nyie tulieni mkamuliwe vizuri hadi pale akili zitakapowarudia. Namshukuru Mungu sipo kwenye hiyo nchi ya Wadanganyika! Khaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!! Full Sanaa, si Rais, Wabunge, Majaji, Wanausalama, Wananchi wote ni Ze Comedy tupu! Watz wote ni mastaa na wasanii wazuri, mkicheza filamu na M.k.w.e.r.e akawa ndio Starring mtauza dunia nzima! Big up sana!
 
jamaani tumechoka na kupoteza matuwaini na serikari hii ya walarushwa na wakanandamiza,wanaojali matumbo yao na familia zao,ukwe tumechoka liwalo na liwe!
 
Wa-tz tuaje porojo jamani kwanin tusiingie barabarani tu,mambo ya kusubiria miongozo ya ssra ni ungese mtupu,tar 15 ni mbali sana!! Paye ni nyingi sana wanayochukua na ndio maana watu hatutaki kuajiriwa mda wote maana tunawafaidisha wauza nguzo za afrika kusini ya kichina(iringa) na wauza vipuli (misumali) na wachumia tumbo(wabunge wala rushwa),Fao la kujitoa ndio kaburi la ccm!!
 
Back
Top Bottom