Mgomo wa Wafanyabiashara ya Mafuta Sasa ni Janga la Kitaifa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Wafanyabiashara ya Mafuta Sasa ni Janga la Kitaifa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ndallo, Aug 9, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Hatimaye Naibu spika bwana Ndugai imebidi akubaliane na hoja ya muheshimiwa Makamba ya kuiita kamati ya bunge na kwenda faragha ili kujadili mustakabali wa hali ya wafanyabiashara nchini kugomea kufungua vituo vya mafuta kutokana na wafanyabiashara kugomea kushusha bei ya mafuta kutokana na serikali kukurupuka bila kuwapa muda wa kutosha kwa wafanyabiashara hao kujipanga. inavyoongea sasa hivi hapa kwa jiji la Arusha wafanyabiashara wenye vituo vya mafuta nao pia wamegoma hali si shwari kabisa naona sasa hili ni janga la kitaifa.
   
 2. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Huwa kuna sekta nyeti kwa taifa ambazo serikali lazima iweke mkono wake.
  Sekta hizo ni pamoja na nishati (umeme, mafuta,makaa ya mawe nk), Reli, Bandari nk. Kwetu TZ tuliiua TIPER, TPDC nk tukaweka kila kitu mikononi mwa watu binafsi, ni vigumu kuwalazimisha bei kwani hujui wanavyonunua.
  Suluhu ya mafuta ni serikali kushughulika na importation then watu binafsi washughulike na usambazaji nchini; then you can set prices or even subsidise them
   
 3. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  mbona hawakuhitaj muda wa kujipanda wakati bei ya mafuta ya taa ilivyopandishwa? na ingekuwa wanauza nyanya wangetaka muda? ni wakati wa vitendo,hii aibu imefikia mahali pake!
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Leo ni siku ya saba tokea sakata hili likiendelea nchini bado serikali haijachukua hatua yoyote kwanini serikali ya ccm isikubali kua ni Legelege.....!!!
   
 5. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2011
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  ndiyo faida ya kubinafishisha kila kitu, wameua TPDC yetu ili wafungue makampuni yao binafisi wale washibe wenyewe - haya sasa zigo hilo.
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2011
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,499
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Sawa kabisa. Tuanzishe thread ya wauza mafuta nchini ni akina nani? yaani wale wanaoagiza nje na kuuza jumla.
  Nakumbuka wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 1995, Dr. Masumbuko Lamwai alikuwa akisema Gapco ni ya kiongozi mkubwa sana wakati huo. Labda tuanzie hapo.
  Juu ya wao kushiba, hilo tusilitarajie ndugu yangu. Hela ni balaa akipata leo laki anatamani ingekuwa milioni, akipata milioni anatamani ingekuwa bilioni nk. Matumbo yao hayawezi kujaa; unakumbuka yule rais wa nchi fulani aliyekutwa ana chumba kimejaa noti za dollar?
  Dawa yao imeshachemshwa kule algeria na misri, kilichobaki ni kuitumia.
   
Loading...