'Mgomo' wa Wabunge wa CCM dhidi ya Mabadiliko ya Muswada kwa Maslahi ya nani?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Tumesoma Wabunge wa CCM kutaka kugomea muswada wa mapendekezo ya mabadiliko ya sheria ya mabadiliko ya Katiba.Mapendekezo mapya ni matunda ya majadiliano baina ya CDM na Serikali baada yaSerikali kuona mantiki ya hoja za CDM.
Ukweli ni kuwa mabadiliko hayo yatasaidia kutunga Katiba bora zaidi kuliko ilivyokuwa awali.
Wabunge wa CCM walipopata wasaa wa kujadili muswada wa,bila aibu waliacha kujadili muswada wakapoteza muda kuwashambulia wenzao wa CDM. JK kakubali hoja za CDM,kwa nini wanagoma?
 
Kwa maslahi yao binafsi, mpaka posho isainiwe. Wengine walishawaahidi vimada wao magari
 
yote hayo ni ubinafsi
Katiba bora si kwa manufaa ya CCM, wala hakuna chama chenye hati miliki ya kutawala milele, watoto wao si lazima wawe wana CCM, vyama vitakufa lakini nchi inadumu hadi mwisho wa dunia.
Lakini ni kama vile Wabunge hawa hawako tayari kuona CCM inaachia madaraka kidemokrasia na kwa amani, sijui wanaitakia nini Tanzania!
Kwa hili JK astahili pongezi nyingi na nashangaa UVCCM wako kimya, ingekuwa enzi zile wa
ngeshatangaza kumuunga mkono dhidi ya Wabunge
 
Kwa mtazamo wa wabunge wa CCM posho kwanza katiba baabdaye! na maslahi binafsi kwanza uzalendo baadaye
 
CCM wanataka wawe na uwezo wa kuendelea kula mali za serekali kwa uwazi bila ya kutuhumiwa.
 
Katiba ililetwa bungeni.
wabunge wakapewa mda wa kujadili na kuboresha.
wabunge wa CCM na CCM-b (CUF) wakashachamba wa chadema na kuwasuta.
mwishoni mswada ukatoka bungeni.
Chadema wameliboresha.
Sijui wao wana maslahi gani
 
Kwa maslahi mapana ya lowasa.

Yaweza kuwa kweli eh!
Nashangaa tangu lini Wabunge wa CCM wamekuwa na jeuri dhidi ya Mwenyekiti wao tena kwa jambo zuriajabu kwa taifa!
Nakumbuka enzi zile Mkapa aliwalima mkwara mzito wakanywea, leo jeuri hii yatoka wapi? Something is wrong somewhere, haiwezekani.
 
Back
Top Bottom