Mgomo wa waalimu ni sahihi, wengine pia fuateni

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,009
2,171
Nchi hii haina utaratibu wa kutoa mishahara inayowiana. Hebu angalia Bunge kujipangia mishahara. Hiki ni chanzo cha matatizo sugu ya nchi hii. Inasikitisha kwamba sasa hivi bunge linaweza kuamua kujiongezea mishahara kwa makubaliano na spika. Spika mwenyewe anapatikana kwa kuchaguliwa na wabunge.

Bunge tena eti nalo lina mfuko wake wa matibabu. Wakitaka kwenda nje au familia zao, ni kiasi cha kushawishi ofisi ya Bunge na unakwenda.

Nchi inapokuwa na utaratibu wa aina hii, kwamba ktk hiyo mihimili mitatu, serikali, Bunge na mahakama, ni bunge tu ambalo watumishi wake wanajadili na kuamua malipo
yao, hatutegemei kama iko siku serikali itafanikiwa kuwahimiza watumishi wake kuongeza tija.

Watumishi wa serikali wakitaka mishahara wanaambiwa wapitie ktk vyama vyao, lakini wabunge hata hawana chama kilichosajiliwa!

Wanachokifanya waalimu na madaktari ni sahihi kabisa kwa sababu hakuna atakayetuletea mishahara mizuri majumbani kwetu. Ningefurahi
sana kama polisi nao wangegoma kabisa lakini eti wanaambiwa hawanruhusiwi kugoma.
 
Back
Top Bottom