Mgomo wa Waalimu na madaktari Kenya. Demokrasia kenya ni kubwa kuliko Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Waalimu na madaktari Kenya. Demokrasia kenya ni kubwa kuliko Tanzania?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mcfm40, Sep 25, 2012.

 1. mcfm40

  mcfm40 JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,142
  Likes Received: 1,779
  Trophy Points: 280
  Waalimu wa kenya wamekuwa kwenye mgomo kwa muda wa wiki tatu sasa. Na serkali ya kenya imekubali kuwaongezea mishahara yao. katika mgomo huu sijasikia serikali hiyo kuuzuia mahakamani wala watu kukamatwa an polisi. Je demokrasia ya Kenya imekuwa kulik,o ya TZ nchi inayodaiwa ni kisiwa cha amani? Tujadili.
   
 2. m

  muchetz JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Kwasababu sisi bado hatujafikia hiyo demokrasia siwezi linganisha (ni sawa na kulinganisha yai na chungwa, completely two different things). Labda ungeuliza tunawezaje kufikia hiyo demokrasia?
   
 3. j

  jitu la kale Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 69
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Watanzania uwa hatupiganiwi wala kujua kudai haki zetu,mf angalia madr,wanahabari,walimu au kipindi kile TUCTA watumish wote.Juzi wanahabari waliapa kutokuandika na kuripoti chochote kuhusu police wa iringa japo kwa siku 40 za msiba wa mwenzao,lakn haikupita hata siku 10 wakaanza kulipoti tena itv,star nk,madr umeona ile comedy yao.
   
 4. M

  Msengapavi JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 23, 2008
  Messages: 4,809
  Likes Received: 2,753
  Trophy Points: 280
  Bila shaka wenzetu wana ujasiri wa kusema hakuna kulala mpaka kieleweke na wakatenda kama walivyosema. Hata kwa upande wa madaktari, Kenya wameamua kukomaa mpaka kieleweke. Hapigwi mtu, serikali haitumii mahakama kuzuia migomo, wala magazeti hayafungiwi. Hii lazima iwe na maana ya kuwa serikali ya KEnya na wananchi wake wana uelewa na utekelezaji mzuri wa demokrasia.

  Watanzania katika hilo tuko mali sana. Waalimu wamenywea na madakari ndo hao wanaomba msamaha wakati malalamiko yao hayajafanyiwa kazi.

  Njaa mbaya sana!
   
 5. o

  obwato JF-Expert Member

  #5
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tatizo la Tz ni mfumo,wananchi wameshakuwa waelewa na wanaamasika kudai haki zao lakini wanazimwa kirahisi sababu CCM ndio mmilili wa polisi, mahakama na jeshi hivyo ni rahisi kukimbilia mahakamani na kuwapangia hukumu,tukumbuke Kenya KANU imeshazikwa na kuna katiba mpya inayoipa mahakama mamlaka kamili na kuifanya selikari ikose pa kukimbilia na kuamua kusalimu amri.
   
 6. M

  Magimbi JF-Expert Member

  #6
  Sep 25, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 1,069
  Likes Received: 517
  Trophy Points: 280
  Unajua wenzetu baada ya kukosa chama tawala bali utawala wa makundi yenye kujiita vyama vya siasa plus ukabila na ukanda ndio wamefikia huko..hawana uoga kama watafukuzwa chamani au serikalini..ndio maana wasikia baadhi ya Mawaziri wameanzisha vyama vyao..Kenya ni nchi kwa sasa kama vile vile haina mwenyewe wala wakuisemea kila mtu ana haki kupitia katiba mpya kumuwajibisha mwenzake. Hayo ndio matunda ya uhuru wa kweli baada ya kufifia kwa KANU kama chama tawala. Hapa kwetu TUCTA wenyewe viongozi wanagombea uongozi kwenye vyama vya siasa hasa CCM muda gani atakuwa na uhuru wa kupinga chochote cha Serikali..
   
 7. mayoscissors

  mayoscissors JF-Expert Member

  #7
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 24, 2009
  Messages: 762
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  kenya si wenzenu enyi wadanganyika....endeleeni kupioiga poroja tu na majungu....madaktati wabaya...wanaharakati...waalimu....mwangosi...nk
   
 8. mpalu

  mpalu JF-Expert Member

  #8
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 15, 2010
  Messages: 2,491
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  ni kwel mkuu watanzania hatuko siriaz kudai haki kenya walim mishahara juu kama sikosei ni asilimia mia
   
Loading...