Mgomo wa Waalim: Nani sasa atapelekwa Mabwepande? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Waalim: Nani sasa atapelekwa Mabwepande?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mdakuzi, Jul 30, 2012.

 1. Mdakuzi

  Mdakuzi JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,748
  Likes Received: 526
  Trophy Points: 280
  Inawezekana kuna aina fulani ya maisha tunaanza kuzoeshwa Watanzania, ni aina ya hakuna itakachowezekana bila migomo na maandamano. Maisha ya sasa yamekuwa hata wanafunzi wa chekechea huandamana kudai kuwekewa matuta kwenye barabara zilizo jirani na shule zao.
  Ndipo tulipo, na wapo waliofanya tuwe hapa, ambao ni viongozi wasiotaka kutimiza wajibu wao hadi wasukumwe na makamanda wa Chadema, kelele za Bunge na maandamano na migomo ya jamii.
  Hili lilisababisha madaktari kugoma, na matokeo yake kiongozi wa madaktari Dr. Steven Ulimboka aliishia kutekwa na kuteswa vibaya hadi kukaribia kifo, kisha kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande.
  Kwa kipindi kirefu waalimu wamekuwa na mgogoro na serikali, na kwa bahati mbaya kwa kipindi chote hicho hakukuwa na kiongozi yeyote wa serikali aliyeonesha nia ya dhati ya kumaliza mgogoro huo, na badala yake wakawa wakiuhairisha tu.
  Na ndio maana nimeanza kujiuliza ni nani itakuwa zamu yake sasa kwa kuteswa na kwenda kutupwa kwenye msitu wa Mabwepande kutokana na mgomo wa huu wa waalimu?


   
 2. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #2
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ni mwanahalisi magazine ameanzishiwa lakini yeye amepelekwa kifungoni,safari hii tutaambiwa hata wake zetu tusiongee nao maana mahakama haijaturuhusu.
   
 3. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Tusubiri tuone.

  Si ndio tarehe zenyewe hizi mzee wa mbayu wayu anashushaga verse!
   
 4. C

  Choi Member

  #4
  Jul 30, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  ha ha ha ha ha! umenichekeshaje?
   
 5. wamdawi

  wamdawi Member

  #5
  Jul 30, 2012
  Joined: Nov 7, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  kwani wagomapo lazima waseme chezea Msitu wa Pande wewe chezea TZ!!
   
 6. marejesho

  marejesho JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 6,539
  Likes Received: 830
  Trophy Points: 280
  Hivi speach kama ile ya Mbayuwayu inaweza kutolewa kesho? Wazee wa Dar es salaam hawajaalikwa?
   
Loading...