MGOMO WA MADAKTARI: Waziri wa Afya kitanzini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MGOMO WA MADAKTARI: Waziri wa Afya kitanzini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by 2mbaku, Feb 11, 2012.

 1. 2mbaku

  2mbaku JF-Expert Member

  #1
  Feb 11, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 317
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  JINAMIZI la mgomo wa madaktari bado linaendelea kuitafuna serikali baada ya jana, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na wanaharakati kutoa matamko mawili tofauti wakitaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Haji Mponda na naibu wake Dk. Lucy Nkya kujiuzulu nyadhifa zao au kuwajibishwa.

  Wanaharakati pia wamempa wiki moja Waziri Mkuu Mizengo Pinda, awe ametangaza hasara na madhara ambayo wananchi na taifa wamepata kutokana na mgomo wa madaktari uliosababisha vifo kadhaa.

  Aidha wamemtaka Spika wa Bunge Anne Makinda kuuomba radhi umma wa Watanzania kutokana na hatua na kauli zake walizodai ni za kibabe ndani ya Bunge za kuzima hoja za wabunge katika kutafakari mgogoro huo.

  CHADEMA katika tamko lao mbali ya kuwataka viongozi hao wawili wa kisiasa kuwajibika, walieleza kushangazwa na ukimya ulioonyeshwa na Rais Jakaya Kikwete katika kipindi chote cha wiki tatu cha mgomo huo wa madaktari uliosababisha kuzorota kwa huduma katika hospitali zote kuu za serikali.

  Mbali ya hilo, chama hicho pia kilielekeza lawama zake kwa Pinda kwa kuchelewa kuchukua hatua za haraka za kuzima mgomo huo hata kusababisha madhara makubwa ya kibinadamu.
   
 2. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #2
  Feb 11, 2012
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hapa ndipo ninapochoka mimi! Yaani madhara na hasara zilizotokana na mgomo wa madaktari mpaka atangaze Waziri Mkuu?! Watafiti na hao wana harakati wanashindwa kulishughulikia hili na kuwajuza wananchi? Huyo waziri mkuu akitangaza uongo?!
   
 3. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Kweli mkuu wasitegemee atatangaza ukweli labda na wao wafanye uchunguzi alafu pindi atapo danganya umma wamweleze ukwali wa uongo wake
   
 4. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mwenyewe nimejaribu kulifikiria suala la jk kuwa kimya kipindi chote hicho nimeshindwa kupata jawabu maana atakuwa ndiye rais pekee duniani anaweza kukaa kimya hivyo kwa mambo yanayoligusa taifa moja kwa moja pasipo hata kumwajibisha mtu
   
 5. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,602
  Likes Received: 2,458
  Trophy Points: 280
  Mkuu swala la kujiudhuru au kuwajibishwa halipo, rejea mifano miwili Ngeleja,Jairo na ukusanyaji wa pesa kufanikisha bajeti, pili Dr. Hussein Mwinyi na milipuko ya mabomu iliyoghalimu roho za watu na mali zao, na hii ni kwa uchache tu. Spika na ubabe wake ulilenga kutokuwapa fursa wabunge ya kujadili sakata la doctors kwa hofu kuwa moja madai ilikuwa ongezeko la posho za doctors na wakati huohuo wabunge nao wanapigia chapuo laki350,000/= hii ingileta mvutano hasa ukizingatia uwiano wa posho ni mkubwa. Kumbukumbuku zangu hazinioneshi wakati ambako mkulu alionyesha kuguswa na madhila ya wanachi wake, hivyo basi sikutarajia kitu hata ktk hili la mgomo wa doctors achilia mbali roho zilizoptea. Pinda nae ni mjinga kabisa alidhani kwa kuwatisha kuwa serikali itawafukuza angetatua tatizo, amesahau kuwa doctors wanamadai ya msingi kabisa, na akumbuke pia mtu mzima hatishwi bali huelekezwa ka njia stahiki. Swala la ripoti ya athari za mgomo nadhani members wa JF tunaweza kuindaa, Nawasilisha.
   
 6. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Rais hawezi kufanya maamuzi mepesi wala magumu.
   
 7. MTENGETI

  MTENGETI JF-Expert Member

  #7
  Feb 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 2,330
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Hata mimi ndipo ninapochokea hapo hao wanaharakati wakitangaza halafu mamlaka zikakanusha ? na kudai takwimu ni za uongo na uchochezi? waonee huruma kina Helen KIJO BADO ANA SHOMBO LA KIBENDERANI
   
Loading...