Mgomo wa madaktari wa tanzania na haja ya kuusuka upya mfumo wa afya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari wa tanzania na haja ya kuusuka upya mfumo wa afya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kebepa, Jul 8, 2012.

 1. kebepa

  kebepa Senior Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 134
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mambo ambayo yamepelekea madaktari kugoma yamejikita katika mfumo mzima wa utoaji huduma za afya katika nchi yetu.
  Mfumo wa afya unatakiwa kuwa na nguzo sita ( kwa kadri ya Shirika la Afya duniani) ambazo ni
  i)utoaji wa huduma za matibabu
  ii)Rasilimali watu
  iii)Mfumo wa taarifa za afya
  iv)Madawa, vifaa tiba na teknolojia za tiba
  v)Rasilimali fedha
  vi) uongozi, será na uratibu
  Nguzo hizi kwa kufanya kazi kwa ushirikiano ndipo mfumo wa utoaji huduma za afya huimarika. Madai ya madaktari yamegusa kila kipengele na yanaashiria kuwa mfumo mzima wa afya katika nchi yetu unatakiwa kufumuliwa na kusukwa upya.Hadi sasa serikali (executive) imeshindwa kusimamia ufanisi wa uratibu wa nguzo zote sita.Kwa kupeleka suala hili mahakamani inaonyesha wazi kabisa kuwa limewashinda na wanahitaji msaada wa muhimili mwingine(mahakama) , lakini hili siyo suluhisho la kutatua matatizo ya kimfumo, ila linachochea tatizo kuwa kubwa zaidi. Kama muhimili wa tatu ( bunge) halitaingilia, baadala ya serikali kutoa huduma za afya kwa wananchi, watakuwa wapo busy kufuatilia mgogoro huu mahakamani wakati wananchi wakiendelea kufa.
  Katika mazingira haya, bunge lilitakiwa lije na mswada wa dharura ( au suluhisho lolote) ambao utaweza kutatua matatizo yaliyopo kwenye mfumo wa utoaji huduma za afya katika nchi. Inashangaza kuona hadi sasa bunge lipo kimya wakati wananchi wanaendelea kufa na wengine kukosa huduma za matibabu au kama wakipata wanapata kwa bei kubwa kana kwamba hawana wawakilishi wanaoweza kuwasemea na kuhakikisha kuwa huduma za afya zinapatikana.Wabunge hawa wanasahau wajibu wao kuwa wao ndio waliopewa dhamana ya kutunga sheria na kurekebisha zile zinazokuwa na utata na kuleta migogoro isiyo ya lazima katika nchi yetu.Wapo wapi sasa, ina maana kuwa katika bunge letu hakuna watu makini wanaoweza kufikiria na kutatua mgogoro huu? Nachelea kufikiria hivyo, nadhani wamesahau kuwa wanatakiwa kusimamia maslahi ya wananchi kwanza kuliko vyama vilivyowasimamisha ( eti wale wa chama tawala hawataki kuonesha kuwa serikali imechemsha, na wale wa upinzani hawaeleweki…hapa ndipo ilitakiwa hata kugomea mjadala unaendelea sasa bungeni na kutoka nje kama walivyowahi kutuaminisha siku za nyuma kwamba wapo kwa ajili ya wananchi).
  Hii inaonyesha wazi jinsi ambavyo bunge letu limekuwa linausikiliza muhimili mwingine ( executive) baadala ya kuusimamia kwa manufaa ya wananchi ambao ndio wanaowapeleka hawa wabunge mjengoni. Kama ni watu makini, wanatakiwa wasisubiri kuletewa miswaada na serikali na wao kuchangia tu badala ya wao kuhusika moja kwa moja kwenye utengenezaji wa miswaada.
  Umefikia wakati wa kila Mwananchi kumuuliza mbunge wake kuwa kama hasimamii upatikanaji wa huduma za afya na huduma nyingine za kijamii, anafanya nini bungeni?na kumwambia wazi kuwa sisi wananchi hatutaki kusikia eti suala la mgomo wa madaktari upo mahakamani wakati tunaendelea kufa.
  Asasi za kiraia na viongozi mbalimbali wa kijamii wanatakiwa wasikae kimya kwa suala hili.
   
 2. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #2
  Jul 8, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  i)utoaji wa huduma za matibabu
  ii)Rasilimali watu
  iii)Mfumo wa taarifa za afya
  iv)Madawa, vifaa tiba na teknolojia za tiba
  v)Rasilimali fedha
  vi) uongozi, será na uratibu
  VYOTE HAKUNA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 3. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Lazima pia juhudi ziende sambamba na kuchoma moto msitu wa MabwePande.
   
 4. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Ccm na serikali yake washaanza kuondosha dhima nzima ya mgomo na kuhusisha na siasa rejea mazungumzo ya mama Stella Manyanya,ktk mazingira kama hayo usitegemee maboresho yoyote
   
 5. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,015
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hivi ni nature imeamua mbumbumbu wote wawe CCM?
   
 6. K

  Kabachubya Member

  #6
  Jul 9, 2012
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 88
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Nakupongeza sana kaka kwa ufafanuzi wako mzuri, unajua hawa wabunge wanafanya hivyo kwa kujua cha cha CCM ndio kimewameka hapo na sio WANANCHI. Kwanini nasema hivyo, ukiangalia kama ni mbunge wa wananchi hata akienda chama kingine wananchi watamchagua. lakini wa CCM wabunge wake wengi wamechaguliwa na chama na sio wananchi. Hilo ndio tatizo la kwanza.

  tatizo la pili ni kwamba wananchi wamelala sana, yani wananchi hawajui haki zao kabisa, mfana sisi ni watoto mapacha kulwa ndio wananchi na doto ndio maDr. baba yetu serikali sasa tumekosa chakula kulwa anaanza kumlalamikia doto anamuacha baba ambaye ni jukumu lake. Ndio kinachotokea Tanzania sasa.

  Sijapenda na sito penda mwananchi yeyote kuwasema na kuwalaumu maDr. coz wewe si una mbunge unayemwamini ukamchagua akuwakiliche? sasa ndio tunaanza kuona jinsi gani wabunge wanavyochaguliwa na vyama na kuwakilisha chama na sio wananchi wanaojifanya wanawatumikia.
   
 7. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Uchambuzi mzuri sana. Hata hivyo katika kuaddress sekeseke zinazoendelea hivi sasa, uchunguzi huu uko biased. 1. Katika utatuzi wa tatizo lolote la kimfumo, MUDA ni factor muhimu sana. Uchambuzi ulipaswa kugusia jinsi madaktari walivyoitumia rasilimali MUDA katika kulitambua tatizo na jinsi ya kulitatua. 2.Kwa vile washauri na watendaji katika kuboresha mfumo wa afya ni haohao madaktari, uchambuzi ulipaswa kuelezea jinsi madaktari walivyokuwa sehemu ya failure ya mfumo ya afya nchini. 3. Uchambuzi umeshindwa kutofautisha kati ya makundi makubwa matatu ya madaktari nchini ambayo yana mtazamo na mahitaji tofauti yaani a) madaktari walioajiriwa kama clinicians b) madaktari watawala c) madaktari wanaomiliki vituo binafsi vya huduma za afya.
   
 8. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2012
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Sasa Sol.ution ni nini mimi niliandika topic hapa nikatoa mawazo yangu ya kubadilisha mfumo je wewe una mawazo gani badala ya kulaumu tu. Watanzania wengi hawana solution na hilo ndilo tatizo kubwa.
   
 9. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Kwa aina ya watawala tulionao sasa hivyo vyote siyo vipaumbele!
   
Loading...