Mgomo wa Madaktari uungwe mkono na wote wenye akili. Tuachane na kuwaamini wanasiasa. Soma haya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Madaktari uungwe mkono na wote wenye akili. Tuachane na kuwaamini wanasiasa. Soma haya.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mangifera, Jun 24, 2012.

 1. m

  mangifera Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii ni sehemu ndogo tu ya wodi mojawapo za Muhimbili. Kama hapa ndo Hospitali ya Taifa, huko kwingine kukoje?

  Kama ilivyo katika sehemu nyingi zinazotoa huduma za afya hapa nchini na hospitali ya taifa Muhimbili kwa ujumla, hali ya utoaji wa huduma za afya ni mbaya.
  Haya ni baadhi ya mapungufu utakayoshuhudia ukienda Muhimbili kulazwa!
  1. Msongamano wa wagonjwa wodini

  Msongamano ni wa hali ya juu sana hadi kupelekea wagonjwa wengi wenye maradhi mbalimbali na mengi ya kuambukiza kama kifua kikuu na hepatitis kurundikana wodi moja.

  Mfano wodi moja ina uwezo wa kulaza wagonjwa/vitanda 33. Lakini wagonjwa kwa siku ni 40 hadi 100 katika wodi moja. Hii hupelekea wagonjwa kulala chini kuambukizana magonjwa na utoaji wa huduma uko chini ya kiwango.

  2. Uhaba wa manesi
  Kwa kawaida wastani wa nesi kwa mgonjwa unatakiwa kuwa 1:6
  Lakini kwa sasa kila shifti wanaingia manesi wawili tu. Yaani ratio ni 2:40-100(1:20-50)
  Imeadhiri sana utoaji wa huduma. Wagonjwa hawapati dawa kwa wakati na wakati mwingine hukosa kabisa.
  Kwa sababu hiyo wagonjwa wanakaa sana wodini na wengine wanakufa bila uangalizi (unattended deaths). Yaani unaweza kupita raundi na kufanya kazi ya kugundua maiti za watu waliokufa bila taarifa!! Unyama gani huu kwa binadamu. Na hili linahitaji mahakama ya kazi?!!

  3. Uhaba wa madawa
  - Kuna uhaba mkubwa wa madawa ya dharura kama Junior ASA, Lasix, Clopidogrel, aldactone na nyingine nyingi kwa ajili ya dharura za magonjwa ya moyo na mapafu.
  - Uhba wa dawa za kutibu magonjwa nyemelezi kwa wenye Ukimwi kama fluconazole nk.
  - Madawa mengine mengi muhimu hayapo mf. Tramadol, lactulose, madawa ya magonjwa ya mishipa ya fahamu nk.
  Madawa muhimu kwa magonjwa hatari ya mapafu kama nebulizers na steroids mara nyingi hakuna. Wagonjwa hufa bila sababu.

  4. Uhaba wa vitendea kazi
  Mashuka- Yanatakiwa mashuka 8 kwa kila kitanda kwa siku. Lakini Muhimbili inatoa shuka moja tu kwa kila kitanda kwa siku. Hii hupelekea uchafu na kuambukizana maradhi

  Vifaa vingine kama infusion pumps, nebulizing machines (kwa wagonjwa wa
  pumu hatarishi) nk hakuna

  Hakuna hata mipira na mifuko ya mikojo haipo. Kila kitu hakuna. Wananchi wanateseka.

  Kukosekana kwa vitendea kazi clinic kama BP machine, stethoscope nk.nk

  5. Ukosekanaji na ucheleweshaji wa vipimo muhimu
  - Mfano CT scan ambayo tangu mwaka jana haifanyi kazi
  - OGD tangu mwaka jana November haifanyi kazi
  - Vipimo huchukua muda mrefu hivyo wagonjwa hufa au huondoka hospitali bila magonjwa yao kufahamika. Mfano USS booking hadi wiki mbili (sababu hakuna mashine na wataalamu wa kutosha kufanya vipimo), ECHO n.k,

  6. Magonjwa ya kuambukizwa na chanjo
  - Madaktari na manesi wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa magonjwa hatari kama ukimwi, Hepatitis, nk.
  - Pamoja na hatari hii, hakuna motisha wala chanjo inayotolewa kuwakinga na wala hakuna fidia inayoeleweka
  Matatizo yaliyotajwa ni machache. Yapo mengi mengine ambayo yanahitaji pia kutatuliwa kwa haraka.
  Madaktari wetu wameshasema. Serikali inakimbilia propaganda za posho na mishahara kwenye vyombo vya habari! Mazingira mazuri ya kazi, wagonjwa kupona ndiyo ahueni(satisfaction) ya daktari.
   
 2. LOWE89

  LOWE89 Senior Member

  #2
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Wanaosema mgomo ni haramu wasome hiyo habari
   
 3. Scofied

  Scofied JF-Expert Member

  #3
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 2,017
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  naumga mkono mgomo wa madaktari dhidi ya serikali DHAIFU ya jk....
   
 4. msnajo

  msnajo JF-Expert Member

  #4
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 2,458
  Likes Received: 331
  Trophy Points: 180
  Sitaki na sitopenda kuwasikiliza wanasiasa wa Tanzania. Kila mwenye pumzi awalaani hawa wanasiasa, ambao umaskini wa watanzania ni mtaji wao. Majuzi nimesoma hapa kuna tsh 330bl ziko Switzerland Central Bank, wameficha tuliowapa mamlaka ya kutuongoza! Vitu kama hivi ndio vina amsha hasira ya Watanzania. Hii makala inamuuma kita mtu mwenye utu! Raisi ikiitwa dhaifu na serikali yake goigoi watu wanabisha. Kwa hali hii, serikali ni "DHAIFU" sana.
   
 5. jingalao

  jingalao JF-Expert Member

  #5
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 19,263
  Likes Received: 10,455
  Trophy Points: 280
  ni heri wananchi wayajue!


  KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
   
 6. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #6
  Jun 24, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,497
  Likes Received: 1,060
  Trophy Points: 280
  Wao ndio haram. Tunawaunga mkono ma Dr wetu.
   
 7. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #7
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Siungi Mkono mgomo wa Madaktari wa Muhimbili ambao uko kiSiasa zaidi kwingwneko kote kazi zinaendelea
  Uzalendo hawana bora JKT irudi hivi kweli Dr unataka Gari na nyongeza % 120
  Nyie sio watoto wa wakulima mlipokuwa wadogo mliwaamrisha wazazi wenu wanunue Treni au gari
  Subirini Bajeti tta Afya ikipita mwambieni Waziri wenu ajiuzulu
  Uhaba wa madawa TC Scan nk mnaviingiza ktk Siasa? Mbona Polisi hawagomi wakati wanapambana na mjambazi wenye AK47 wao wana SMG
  Angalieni na ubinadamu wanaokufa ni ndugu zako
  Ningekuwa Rais anayedhubutu Muhimbili nungeweka maDR wa Jeshi halafu maDokta mliogoma JKT mgomo quishney
   
 8. j

  jigoku JF-Expert Member

  #8
  Jun 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Kweli wewe ni UKWAJU,tena nadhani ni ukwaju hybrid.hivi wewe ulishawahi kuguliwa au kuuguwa na ukalazwa?hivi unaijua hali ya muhimbili? na je unaijua hali ya mahospitali hata huko mikoani?unayajua mazingira ya kazi yalivyo mahospitalini?watu kama nyinyi sijui huwa mmezaliwa wapi na katika familia gani,na sijui mnamuabudu Mungu yupi au sijui ni shetani gani.
  Na siku zote akili fupi huwa zinalazimisha kutatua matokeoya taitizo na sio chanzo cha tatizo,laikini kwa kuwa umenisikitisha kwa uelewa wako mdogo juu ya sakata la madaktari sintoendelea kukujuza kitu,ila kwa taarifa ni kwamba WAKO WENGI TU PIA WANAOUNGA MKONO MGOMO WA MADAKTARI NIKIWEMO NA MIMI,NATOA RAI KWA MADAKTARI YA KUWA MSIOGOPE KUNA WANANCHI WENYE AKILI ZAO TIMAMU WANAUNGA MKONO MGOMO WAENU BILA KUJALI HATA SISI TUNAOUNGA MKONO TUNAWEZA KUUGUA.KAZENI BUTI WALA MSIHOFU.
  Ni wafahamishe wanabodi,mkitaka kujua ukweli wa mgomo tafuta jamaa yako ambaye ni daktari ili akuhabarishe jinsi whali ya mgomo ilivyo,wanawasiliana kupitia mfumo wao wa masiliano unaohusu walioko MART tu,kama sio member huwezi kupata access.Ukwaju unawaongopea watu,mgomo upo na tutahakikisha unaendelea na unafanikiwa
   
 9. H

  Hute JF-Expert Member

  #9
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,045
  Likes Received: 3,918
  Trophy Points: 280
  kati ya vitu ambavyo nimesikitika kuvisikia ni kuwa vipimo vya T scan havipatikani nyanda za juu kusini yaani iringa mbeya etc, wanatakiwa waje dsm, alisema dr. ulimboka kwenye tv kwa waliosikia...sijui garama ya icho kitu ni sh. ngapi, mafisadi wamekula sh ngapi, epa walirudisha sh ngapi na priority ilienda wapi kama sio kupunguza maafa ya watu hawa wa nyanda za juu kusini....afadhali hata kaskazini utakuwa kuna bugando, kuna kcmc etc.....
   
 10. Dr Klinton

  Dr Klinton Senior Member

  #10
  Jun 24, 2012
  Joined: Jan 21, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona kushirikisha ubongo wako vizuri au wewe ni mmoja wa wale mnaokula mkate huu wa tz kwa sasa

  Unajua watu wa kwenye mashirika ya amma wanajilipaje au wao pesa wanalipa si ya kodi za watz ewura,epz, tanroads, tcra, tanapa, mengine taja wewe si mishahara tu na miposho PIA... Wanayojilipa am sorry mnayojilipa......

  Daktari bila vitendea kazi tofauti yake na sangoma ni Nini, mazingira yenyewe hovyo
  Tatizo watz wengi ni wajinga na hawajui haki zao sijui nani atawaamsha maana wewe na wenzako mnataka waendelee tu kulala nyie mmpeleke hiyo mijipesa uswisi
   
 11. H

  Hute JF-Expert Member

  #11
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,045
  Likes Received: 3,918
  Trophy Points: 280
  madaktari gomeni sisi wananchi tuko upande wenu...wengi wetu hata mimi ule mgomo wa kwanza sikuunga mkono niliwapinga sana madaktari, lakini ni kwasababu nilikuwa sijaelewa, nafikiri wananchi wakieleweshwa vizuri kuhusu issue hizi wanaweza kuwaunga mkono sana madaktari.
   
 12. a

  adolay JF-Expert Member

  #12
  Jun 24, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  kama serikali haitaki madakitari wagome si iboreshe mazingira ya kazi na vitendea kazai.

  Wanauwezo wa kubeba wanachama kutoka pembe zote za jiji la Dar es salaam kuenda kuwaaminisha ujinga kwenye mikutano yao.

  Je hiyo mikutano na afya zetu kipi bora? Tunahitaji matibabu bora na si bora matibabu.
   
 13. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #13
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mgomo sawa kama njia ya kushinikiza suala fulani kutekelezwa, kwa uzoefu wa migomo ya Tanzania si dhani kama inafanywa kitaalam kwa maana ya kujipanga kwa kuweka malengo na baadaye kufanya tathmini kama umefanikiwa ua la, tathmini itasaidia kuona matokeo na kutoa mwanya wa njia mbadala pale tunapobaini kuwa njia ya wali haikufanikiwa.

  Kukosekana kwa tathmini na mikakati madhubuti ya kuendesha migomo, kwa sasa wanaoumi ni raia wasikuwa na hatia. Madktari waliogomo siku chahche zilizopita, madhara makubwa yaliyotokea ni watu kupoteza maisha hasa wale ambao hawanauwezo wa kupeleka wagonjwa wao mahali pengine kupata huduma. Viongozi wa madaktari walipata audience ya kutosha na viongozi wote wa kitaifa na kuwasilisha madai yao.

  Leo wameanza mgomo kwa mtindo ule ule, matumaini yangu ni kuwa madhara yatakuwa yale yale, walalahoi watapoteza maisha, baadaye viongozi watasimama majukwaani na kulaani mgomo na pole kwa wote waliopoteza ndugu zao. Swali la msingi ni je madaktari wamefanya tathmini na kubaini kama njia wanayoitumia kugoma/kuendesha mgomo/kusukuma madai yao? hasa kwa kuchukua matokeo ya mgomo uliomalizika mwanzoni mwa mwaka huu. Kinachoonekana hivi sasa ni ubabe kati ya serikali na wadaktari. Wakati serikali ikisema this time hakuna kuwasikiliza wadaktari wanaamini kuwa watafanikiwa kwa kutumia mbinu ile ile. Ni kweli madai yao ni ya msingi kabisa na nawapongeza kwa kudai masuala mengi kwa niaba ya wananchi, lakini nawashauri wakae chini na kubuni mbinu mbadala kushinikiza madai yao kuliko kutumia njia ile ile ambayo kimsingi imeshindwa kuzaa matunda.
   
 14. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #14
  Jun 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Wakati hospitali zetu zipo hivyo, Kikwete anapanga kujenga kumbi za kustarehe zaidi, Mbowe anapanga kununua toleo jipya la gari yake ya kutembele, Mkapa anapanga kwenda kupumnzika ng'ambo, Ndesamburo na Nkono wao wanapanga kununua Hoteli Nairobi na Dubai, Lowasa na Rostam wanashindana kuingiza hela kwenye akaunti zao za nje, Dr. Slaa anapanga kwenda Ujerumani kutembelea marafiki zake, Sugu anapanga kwenda kufanya show Dar Live na Jubilee na Mnyika na Mdee wanapanga kumsindikiza, Riz 1 anapanga kwenda kupunga upepo fukwe za Brazil na kimada wake, Lipumba anapanga kwenda kupewa sifa nje ya nchi, Lema anapanga wapi pa kupata pesa akuze jina, mawaziri wanapanga kuiba wake za watu, shehe na askofu wanapanga kwenda kuhiji Mashariki ya Kati, wabunge wanapanga kwenda kustarehe viwanja gani. Masikini mkulima na Mfanyakazi, nguvu zao ndizo zinavyoliwa hivyo. Wamejikunyata kama kuku aliyenyeshewa na mvua, wanaimbishwa wimbo wa ukombozi na hao hapo juu! Ningekuwa macho nisingependa kuona.
  MUNGU wetu anaita sasa!
   
 15. m

  mangifera Member

  #15
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 15, 2011
  Messages: 47
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama topiki inavyosema ni kuwa watu wenye akili ndo wanaweza kuona na kuunga mkono mgomo huu!
  Lakini kuna wajinga wengi kama huyo Ukwaju hapo juu (ndo maana una ugwadu ugwadu). Hawataona na wala hawasikii!! Na hawa ndiyo mtaji wa mafisadi na magamba maana wanajua kuna mabwege wengi wanawasapoti, ndo maana wanatufanyia hvyo!!!
   
 16. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #16
  Jun 24, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Binafsi naunga mkono mgomo wa madaktari kwa vile nimeelewa vizuri sababu za madaktari hao kugoma. Kuongezewa posho ni sehemu ndogo sana ya malalamiko ya madaktari. Sehemu kubwa ya malalamiko ya madaktari ni kufanya kazi katika mazingira ambayo yanawazuia kufanya kazi yao vizuri. Mimi sio daktari wa wagonjwa, lakini nina marafiki zangu wengi madaktari ambao wamekuwa wakihuzunika sana pale mgonjwa anapofariki, hasa kutokana na na sababu ambazo zingewezwa kuzuiliwa. Mara nyingi, kisaikolojia, madaktari hawa wanaishi katika hali ya mahuzuniko kila siku. Jifikirie kama ni wewe ungekua unaishi katika hali hiyo kila siku!

  Nasema kuwa vifo vingi vingeweza kuzuilika kama serikali ingekuwa na nia thabiti ya kudumisha sekta ya afya, badala ya kuzingatia matumizi makubwa ya serikali katika mambo ambayo si ya muhimu na ya anasa. Hakuna haja ya kuandika hapa ni mambo yepi maana hata asiye kipofu anaona. Viongozi wetu pamoja na familia zao wanaishi maisha ya anasa kupita kiasi, huku wakija kwenye majukwaa wanawaambia wananchi kwamba wako pamoja na wananchi. Wakiugua wanakuwa haraka sana kukimbilia kutibiwa nje wakati mwananchi wa kawaida ni shida sana kwake kufika katika hospitali ya rufaa ambayo hata akifika, itakuwa ni shida sana kupata matibabu ya kuaminika.

  Nimeshauguza ndugu zangu na kuona adha ya hospitali zetu. Kimsingi ni kuwa hakuna huduma bora yeyote inayotolewa huko. Hakuna dawa wala vifaa vya kuhudumia waagonjwa. Vingi ilibidi tununue wenyewe na mara nyingine, kwa sababu vifaa vingine vilikuwa vya kitaaluma zaidi, vilikuwa havipatikani madukani, tuliuziwa kutoka hospitalini huko huko. Wakati wote viongozi wetu wanaishi katika maisha ya kupeta.

  Kutokana na hali hii ya huduma mbovu za afya, huduma ambazo zimeachwa kwa makusudi ziwe mbovu, watu wengi sana wamekwisha fariki mpaka leo. Wengine wamefia mahospitalini, lakini wengine wengi pia wamekufa bila kufika hospitalini au kwa kushindwa kufika huko, au kwa kukata tamaa kwamba wakienda hospitalini hawatapata huduma yeyote ile. Hali hii nayo imejitokeza katika kushamiri biashara ya waganga wengi wa kienyeji (wengi wao matapeli). Mfano mmojawapo ni pale tulipoona watu walivyofurika kwenda kwa Babu wa Loliondo. Tuliweza kuona mpaka hao hao viongozi wakifurika kupata kikombe. Pamoja na kwamba wanaweza kwenda kutibiwa nje, lakini mawazo ya kijamii ya kijumla (psyche) juu ya uponyaji wa kiaina pamoja na ushirikina, nao yameshawaathiri.

  Inabidi wananchi na sisi tudai haki zetu badala ya kuwalaumu madaktari amabao wameshaliona hilo na wanadai haki ya kupata afya kwa ajili yetu. Upatikanaji wa afya ni mojawapo ya misingi ya haki ya mwanadamu. Tusipofanya hivyo, wagonjwa (ambao ni sisi sote) wataendelea kufariki, iwapo madaktari watagoma au la.
   
 17. Duduwasha

  Duduwasha JF-Expert Member

  #17
  Jun 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 5,135
  Likes Received: 2,159
  Trophy Points: 280
  Dawa hazipatikani Mahospitalini hadi uende Pharmacy za Vigogo na Mawaziri Pembezoni mwa Hospital na Mitaani na Nchini India
   
 18. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #18
  Jun 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  hebu tufike hospitali zetu za serikali ili tujue mauzauza ya huduma.

  Ukienda hospitali utasikia x ray haifanyi kazi,hii dawa haipatikani,ambulance haina mafuta,daktari yuko kwenye kijiwe chake n.k
  serikali inawajibika kutafuta ufumbuzi wa maswala haya bila ubabaishaji.

  Leo hii tuna neurosurgions wasiozidi watatu tanzania,mmoja amefuata maslahi bora botswana.

  Tunatumia hela(mafuta) kumfuata daktari nyumbani kwake wakati tungeweza kumjengea nyumba karibu na hospitali,ukienda upanga utakuta wahindi ndio wakazi wa eneo hilo wakati madaktari wanakaa kimara uswahilini.je huu ni utawala bora?tumeweka malengo ya milenia katika afya je tutayafikia kwa kuwadharau wahudumu wa afya?

  Kigogo anachukua milioni kumi kwa mwezi wakati mkunga anapata laki mbili na ushee je hii ni sawa?

  Tunasema hatuna hela kwa nini tusiweke mikataba ya madini vizuri na kusema kila kipato cha madini asilimia moja itaenda kwenye afya!

  Serikali ionyeshe ujasiri na iache uzaifu.
   
 19. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #19
  Jun 24, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  "Insane means doing the same thing again and again and then somehow expect different results"
   
 20. 4

  4change JF-Expert Member

  #20
  Jun 24, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 535
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  funguka ndugu.utabaki na mawazo finyu namna hii hadi lini?ndo maana nchi yetu haiendelei!Kwa hiyo wewe unaona ni sawa askari mwenye smg apambane na jambazi mwenye ak47?unafiki hao 'madaktari' wa jeshi hawana kazi huko waliko?wakitoka huko nani atawareplace?na wakija muhimbili ndo vitanda madawa na vifaa vya kupimia wagonjwa vitapatikana?na kwenye hosp nyingine watawatoa wapi madr?na hii ndo itatatua matatizo yaliyoko kwenye sekta ya afya?THINK BIG
   
Loading...