Kwakweli leo madakatari wote wamerejea kazini. Muhimbili leo asubuhi wakipishana kila mmoja kuwahi kutia sign daftari la mahudhurio.
Ni wazi wito wa Waziri Mkuu umeitikiwa kwa kasi ya ajabu.
Tatizo la viongozi wetu wengi bado wanafikiri wananchi kwenye zama za RTD! Sasa hivi huhitaji radio wala tv kujua nini kinaendelea duniani let alone hapa bongo! Hawa mabwana wameharibu kabisa TBC sasa hivi imegeuka kuwa national embarrassment. Tangu mgomo umeanza TBC imekuwa na mkakati wa ku-downplay hali halisi. Je, ni kweli watu hawana taarifa? Ukitaka kutatua tatizo sharti ukubali kwanza kuna tatizo.