Mgomo wa Madaktari: Serikali yalazimishwa kutoa maelezo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa Madaktari: Serikali yalazimishwa kutoa maelezo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 3, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,076
  Trophy Points: 280
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE]
  [TR]
  [TD]Madaktari watikisa Bunge
  • Serikali yalazimishwa kutoa maelezo

  na Waandishi wetu
  Tanzania Daima  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #ffffff"] [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE]
  [TR]
  [TD]MGOMO wa madaktari umelitikisa Bunge ambapo sasa limetishia kutoendelea na shughuli zake endapo serikali haitotoa hatima ya mgomo huo leo.
  Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, kabla ya kuahirisha shughuli za Bunge jana.

  Ndugai alisema anashangazwa na ukimya wa serikali kwani iliahidi tangu juzi kutolea kauli, lakini hadi jana haijasema chochote huku mgomo huo ukiendelea kushika kasi na hali za wagonjwa zikizidi kuwa mbaya.(What do you expect from Serikali taahira!?)

  “Ninaiagiza serikali kesho iwe imeleta maelezo yake bungeni, vinginevyo shughuli za Bunge zitavurugika kwa wabunge kutaka kujadili hali hiyo,” alisema Naibu Spika huyo.

  Huku akiungwa mkono na wabunge wengi kwa kupiga piga meza zao, Ndugai alisisitiza kuwa jambo hilo ni la dharura, hivyo linapaswa kuwa na ufumbuzi wa haraka badala ya kuendelea kuchelewa kulishughulikia.
  Akitolea mfano alisema juzi nchini Misri, zaidi ya watu 78 walifariki katika uwanja wa mpira na Bunge la nchi hiyo ambalo lilikuwa likizo kwa wakati huo, liliitwa kwa dharura kujadili hali hiyo.

  “Mgomo wa madaktari wetu una zaidi ya wiki mbili sasa na hatujui umesababisha vifo vya watu wangapi, lakini serikali iko kimya kabisa. Tunaitaka serikali leo ije na kauli yake juu ya hatma ya mgomo huo,” alisema Ndungai.(Duh!!! Aibu kubwa kwa Kikwete)

  Awali kabla ya kutoa kauli hiyo, Ndugai alizima mwongozo wa Spika uliotolewa na Mbunge wa Kigamboni, Dk. Faustine Ndungulile (CCM), na John Mnyika (Ubungo), ambao kwa nyakati tofauti walisimama kutaka kujua kauli ya serikali na pia Bunge kuvunja shughuli zake za jana kwa ajili ya kujadili hoja ya mgomo wa madaktari.

  Mnyika alisema kwa kuwa jambo hilo ni la dharura na tayari limeshaleta madhara makubwa, aliliomba Bunge kuvunja shughuli zake ili kujadili hatma ya mgomo huo wa madaktari.

  Akitoa mwongozo wa hoja za wabunge hao, Ndugai alisema kuwa wabunge hao wako sahihi, lakini wakitoa hoja hiyo, wabunge wanaounga mkono walipaswa kusimama kwa mujibu wa kanuni ili kuiunga mkono.

  “Wabunge hao wako sahihi, wametumia kanuni vizuri, tatizo ni moja tu wakati wanatoa hoja hiyo, wabunge wanaounga mkono kutaka shughuli za Bunge leo zivunjwe kutoa nafasi kujadili hoja hiyo, walipaswa wote wasimame, hivyo naitupa hoja hiyo kwa sasa,” alisema Ndugai.

  Madaktari watoa tamko
  KAMATI ya Jumuiya ya ya Madaktari imetoa tamko na kukataa mpango wa madaktari bingwa wa kuonana na Waziri Mkuu Mizngo Pinda, wakisema kuwa jumuiya hiyo imepewa mamlaka kuratibu madai ya madaktari.

  Alisema jumuiya hiyo pia inaratibu madai ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Taifa Mhimbili ambao juzi waliunda kamati ya watu watano kwenda kumuona Pinda kwa ajili ya kutafuta suluhu ya mgomo uliodumu kwa takriban wiki mbili sasa.

  Akizungumza na waandishi habari jana, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Dk.Stephen Ulimboka, alisema kuwa uamuzi huo umetokana na kikao kati ya madaktari bingwa na kamati ya jumuiya ya madaktari.

  Alisema kuwa mpango mkakati wa madaktari bingwa hauna jukumu la upatanishi na hata siku moja madaktari hawakuwahi kukaa na kuteua kikodi kazi cha upatanishi.

  Dk. Ulimboka alisema kuwa jukumu pekee la kikosi kazi kilichoundwa Muhimbili ni kuishinikiza serikali itoe majibu kwa tuhuma zilizo mbele yake na si kwa jumuiya ya madaktari.

  Hali bado tete Muhimbili
  HALI imeendelea kuwa tete katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kutokana na mgomo wa madaktari unaoendelea hospitalini hapo.

  Wagonjwa mbalimbali waliolazwa katika wodi ya Mwaisela, Kibasila na Sewa Haji wamewaambia waandishi wa habari waliotembelea wodi hizo jana kuwa wanaiomba serikali kukaa pamoja na madaktari ili kuweza kutatua mgogoro huo.

  Hata hivyo, meneja wa kitengo cha magonjwa ya dharura, Silanda Optatus, aliwaambia waandishi wa habari kuwa huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida ingawa kuna tofauti kubwa ya wagonjwa wanaoingia katika kitengo hicho.
  Alisema hapo awali kwa siku walikuwa wanapokea wagonjwa 80 hadi 100 lakini kwa sasa wanapokea wagonjwa 25 na wote wakipatiwa huduma.

  Wakati huohuo,Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia, aliyetembelea hospitalini hapo kwa ajili ya kuwapa pole wagonjwa, alisema hali ni mbaya na kwamba serikali isifanye mzaha na masiaha ya watu.

  Alisema kuwa alitembelea hospitali ya Amana na kijionea hali mbaya pia kama ilivyo Muhimbili kutokana na hivyo kuitaka serikali kuchukua hatua za makusudi kunusuru hali hiyo.

  Aidha alisema kuwa kama mgogoro huo hautasimamiwa na kupatiwa ufumbuzi ndio utakaoiondoa serikali madarakani.
  Aliwaomba madaktari watumie hekima kupitia kwa Waziri Mkuu Pinda ambaye hapo awali serikali ilimtumia katika kutoa kauli ambayo haijazaa matunda.

  Habari hii imeandaliwa na Martin Malera, Chalila Kibuda na Asha Bani

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #2
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Naye Ndugai aache kutuchezea akili. Anafikiri wote tunatoka huko kijijini kwao? Yeye mwenyewe ni sehemu ya tatizo la mgomo wa madaktari halafu anailazimisha serikali itatue. Basi aanze yeye kwa kurudisha Posho za bungeni anazo ng'ang'ania utafikiri ni haki yake. AAche kupenda sifa na ubinafsi.
   
 3. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #3
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ndugai hajatamka maneno kama Serikali Taahira, Aibu kwa kikwete, hivyo Thread yako imepoteza maana. Lakini pia tuna swali la kujiuliza, Ina maana Ndugai hajui juhudi ambazo SERIKALI imekuwa ikifanya kuhusiana na mgomo huo mpaka aseme imekaa kimya? au alitaka kuwafurahisha Wabunge? Mbona hajitafutii umaarufu kupitia sakata la posho zao? Tunashindwa pia kuelewa kuwa Serikali siyo Kikwete (Government is a system) sasa sijui unaposema aibu kwa Kikwete una maana gani ,labda ungefafanua, na kwa nini isiwe aibu kwa Madaktari ambao wanaidhalilisha taaluma yao kutokana na influence za kisiasa?
   
 4. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #4
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Let's wait and see.
   
 5. MachoMakavu

  MachoMakavu JF-Expert Member

  #5
  Feb 3, 2012
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Inawachukua siku zaidi ya tatu kuandaa tamko? Leo itabidi nisubiri kuona hilo tamko la siku tatu likoje
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mzushi tu huyu, anafikiri atakuwa maarufu kama Sitta kwa kufanya hivyo. Hajui Sitta ni miongoni mwa watu wanaopenda sifa sana lakini kiuhalisia ni watu ambao hawana mchango wowote katika kumsaidia mwananchi wa kawaida mbali na kuwatumia kama daraja la kujipatia nyadhifa. Kwa nini Ndughai anakuwa mkali pale tu wabunge wanapokuwa wamechachamaa. Nakumbuka hata issue ya Jairo, alitoa kauli ambazo siyo rahisi kutolewa na kiongozi wa ngazi ya juu kama Naibu Spika. Yaani unaona wazi kuwa anafanya hivyo ili mradi aonekana wa tofauti (kupenda sifa huko). Issue ya Madaktari huwezi kuilaumu Serikali pekee, wa kulaumiwa zaidi ni Madakari. Tangu mgomo uanze wamekutana na Serikali mara kibao, lakini kwa vile kisaikolojia walishaliweka katika hali ya kukataaa kila pendekezo la Serikali na siyo siri dhana hiyo ambayo sote tunajua kwamba imetokana na misukumo toka nje (Kisiasa na kijamii) wamesababisha maafa makubwa kwa wagonjwa. Ni vigumu sana mtoto ambaye anashikinizwa na Mama kupata kitu toka kwa baba yake amkubalie Baba kuwa atakipata muda mwingine, lazima atalazimisha tu na hata kuanza kumdharau baba yake. Lakini sasa swali ni je Baba sasa akigundua kuwa mwanae ambaye hakuwa na tabia hiyo, amebadilika kutokana na msukumo toka kwa Mama atafanya nini? Itabidi aache kwanza mtoto mwenyewe achambue pumba na mchele na kigungua kuwa Mama anampotosha basi itabidi arudi kwa Baba.


  Jamani, Serikali ingewachapa viboko Madaktari waende kazini kwa lazima wakati hawataki kukubali lolote. NDUGHAI ajiulize kama angekuwa yeye angefanya nini?
   
 7. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #7
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  source: Tanzania daima ....gazeti lilile linalonukuu vibaya kwa faida ya kisiasa.
   
 8. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #8
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siasa chafu + gazeti chafu = chama kichafu
   
 9. f

  frontline1 Member

  #9
  Feb 3, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  wapambe wa serekali ni wengi sana, naomba tu ni wasihi wachangia mada waache kuwashambulia watu binafsi badala yake wachangie hoja kwa kutoa maoni yatakayotatua tatizo lililopo, ni kweli kuwa taifa letu linahitaji mabadiliko yakisera na mfumo, tuache ushabiki tuweke mbele uzalendo.
   
 10. Raia Mwema

  Raia Mwema JF-Expert Member

  #10
  Feb 3, 2012
  Joined: Jun 30, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania Daima lilikuwa gazeti pendwa sana sijui limepatwa na nini siku za karibuni halina tofauti na Ijumaa na Kiu. Au limenunuliwa na Erick Shigongo
   
 11. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #11
  Feb 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,159
  Likes Received: 1,248
  Trophy Points: 280
  Ama kweli Nyani haoni kundule
   
 12. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #12
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135

  KANUNI ZA KUDUMU ZA BUNGE, TOLEO LA 2007

  47.-(1) Baada ya Muda wa Maswali kwisha, Mbunge yeyote anaweza kutoa hoja kuwa Shughuli za Bunge kama zilivyooneshwa kwenye Orodha ya Shughuli ziahirishwe ili Bunge lijadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.

  (2) Hoja ya namna hiyo itakuwa ni maalumu na inaweza kutolewa wakati wowote hata kama majadiliano yatakuwa yanaendelea.
  (3) Hoja itatolewa na Mbunge kwa kusimama mahali pake na kuomba idhini ya Spika kutoa hoja ya kuahirisha Shughuli za Bunge
  kwa madhumuni ya kujadili jambo halisi la dharura na muhimu kwa umma.

  (4) Iwapo Spika ataridhika kwamba jambo hilo ni la dharura, halisi na lina maslahi kwa umma, basi ataruhusu hoja hiyo itolewe kwa
  muda usiozidi dakika tano na mjadala juu ya hoja hiyo utaendelea kwa muda ambao Spika ataona unafaa kwa kuzingatia mazingira ya suala linalojadiliwa

  Hapa ndipo ninpoamini kuwa JF ina mchango mkubwa sana katika good governance of this country, nina imani kuwaNaibu Spika Mhe Job Ndugai alitaka kuliburuza taifa lakini alipogundua ya kuwa wananchi kupitia JF tunafahamu Kanuni za bunge akajirekebisha.

  Wapi katika ibara alizotaja hapo juu wabunge wametakiwa kusimama kuunga mkono hoja, kanuni zinamtaka spika kuridhika na kuahirisha shughuli za bunge iwapo hoja iliyotolewa na mbunge ni ya dharura kitaifa tu.

  Alichofanya Ndugai ni kuipatia serikali nafsi ya kujipanga kwa hoja za uongo ndipo joni wakati wa kuahirisha bunge anataka maelezo ya serikali yatolewe kesho yake kinyume cha kanuni.
   
 13. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #13
  Feb 3, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  kwa kauli zako nahisi wew ni mmoja kati ya Mponda, Nyoni au Mtasiwa. Kwanini ajzungumza hoja ya madakatari kuchoshwa na vifo vya maelfu ya wagonjwa kutokana na ukosefu wa vifaa vya tiba ambyo ni moja ya madai yao, Wamechoka kufanya kazi katika mazingira duni huku wakishuhudia maelfu ya watanzania wenzao wakipoteza maisha kwa kukosekana vifaa vya tiba ambavyo vingeweza kupaikana kwa fedha kidogo kama serikali ingebana matumizi kidogo tu. Acha kuwa upande mmoja tu. Hivi ni haki mtumishi wa serikali alipwe Shs 200,000/ hadi 1,000,000/= kama posho ya kuhudhuria kikao ( mara nyingi hivizidi nusu sasa au wakati mwingine hawahudhurii kabisa ila huandika majina tu) ambacho ni sehemu ya ajira yake anayopokea mshahara halafu dkatari alipwe posho ya kazi za usika ya Shs 10,000/= huku akijiweka hatrini kupta maambukizi ya magonjwa mbali mbali toka kwa wagonjwa anaowahudumia k.m ukimwi n.k
   
Loading...