Kashindye J.J
Member
- Oct 3, 2011
- 8
- 2
Madaktari wanagoma sasa, wanagoma wakiwa na madai ya msingi mikononi mwao. Lakini wakati mgomo unapamba moto, roho za raia na wananchi ziko mashakani.
Juhudi za serikali kutatua mgogoro huo na kumaliza tatizo zinakwenda taratibu kwa mwendo wa kinyonga mlemavu. Mgomo wa madaktari ni hatari kuliko aina zote za migomo kwa sababu unagusa moja kwa moja uhai wa wananchi.
Suala hili linahitaji kiongozi mwenye maamuzi magumu. Wala siyo watu wenye dharau za kiutendaji kama JK na wasaidizi wake. Natamani sana kipindi hiki LOWASA Ndiyo angekuwa Rais au Waziri Mkuu. Bila ya shaka angechukua maamuzi magumu na tatizo hili lingekuwa mfano wa chai ya baridi kwake. Nani mwingine?
Nani mwingine mwenye uthubutu na roho ngumu ya maamuzi kati ya waliopo CCM sasa zaidi ya mchapakazi LOWASA anayetetea maslahi ya wanyonge? Huu ndiyo ukweli japo wenye akili zilizopiga sarakasi watapinga na kudai nimevuta bahasha kama kawaida yao.
Hapa tu ndo mnaniboaga mkianza kampeni zenu za kuwapigia debe wanasiasa. Bila shaka umepewa ka-mkate kufanya hiyo kazi. Haya bhana endeleeni kumsafisha tunasubiri kuona