Mgomo wa madaktari na uongozi wa nchi

Leo ni siku ya juma3 tar 25/06/12 ambapo wananchi wengi walisubiria kujua hatima ya mgomo wa madaktari. Taarifa ya habari ITV, STAR TV NA CHANEL TEN wameripoti kuwa hali ni mbaya Bugando , Mhimbili, MOI, OCEAN ROAD, MBEYA Kwani madaktari wengi wameunga mkono mgomo hali inayo wafanya wananch weng kuhaha huku walio na uwezo wakipeleka wagonjwa private. Kwa upande mwingine TBC1 Wameendelea na mgomo wa kutotangaza mgomo wa madaktari. Wa Tz kwakwel hali ni mbaya

tbc wao wanaangaliwa na nani????,nadhan hata wafanyakaz wa tbc hawaangalii taarifa za tbc
 
Serikali yetu ya Jmahuri ya Muungano Tanzania imekuwa na camouflage behavior katika kutekeleza makubaliano mbalimbali kufikia muuafaka kubaliwa.Utakumbuka serikali kupitia kiongozi mkuu wa nchi waliwaita madaktari na kuwasihi kuacha mgomo kwa makubaliano yao kutekelezwa.Walifika mbali zaidi madaktari kwa kusema wana imani na rais hatawaangusha.Lakini leo hii serikali hii hii inakimbia kivuli chake ama kwa makusudi au kutumia mbinu chafu za kubambika tuhuma ambazo madaktari hawakuweka katika madai yao ya awali.

Ifike hatua serikali iwe sikivu kimkakati zaidi kuliko kimaneno,namaanisha kwamba rais wetu amekuwa akisisitiza majadiliano ndiyo njia muafaka ya kutatua matatizo yanayoikabili jamii lakini anasahau kuwa amekuwa bingwa mara zote kwa kushindwa kutembea ndani ya maneno yake ama kwa kupuuza madai waliyoyafikisha kwake au staili yake ya funika kombe mwanaharamu apite.

Mgomo wa madaktari ni hatari kwa afya yetu,ikitokea serikali ikashindwa kuwahudumia wananchi wake kwa kushindwa kupata muafaka wa madai ya madaktari jua kuwa taifa linaingia kwenye janga kubwa la kitaifa kwa mustakabali wa afya ya jamii.Serikali isiogope kivuli chake,itekeleze makubaliano waliyoafikiana ili taifa liweze kukabiliana na changamoto mbalimbali huku taifa likwa na afya njema.
 
tujuzeni wakuu... hii ishu nakumbuka ilinifanya nkapigwa ban... siihitaji kua upande wowote leo.
 
Tatizo mna waamini mno viogozi wenu, wenye apetaiti kuliko viwavi

Tatizo si kuamini tu,bali mfumo wea kulindana ndiyo uliotufikisha hapa,tukisema kiongozi dhaifu watu wanabeba bango ooh,matusi hayo,matokeo yake nini afya ya wananchi mashakani
 
tatizo la wanasiasa ni kudhania kuwa wao tu ndio wenye kujua siasa.

Wanasiasa ndiyo waharibifu na wavuruga amani wa nchi hii,nasema hivyo nikimaanisha kuwa wao ndio chanzo cha kuleta mparanganyiko ndani ya nchi yetu kwa watu achache kutumia fursa waliyoipata kisiasa kutekeleza maazimio yao binafsi kwa matakwa yao binafsi.Wanasiasa hao wanaamini kuwa wao ndio source ya maendeleo kwa upande mwingine.Cha muhimu wananchi tujiepushe tunapopata fursa ya kuwaweka madarakani wanasiasa hao huku tukijua nia yao hasa kwani tunawajua kwa kuwa tunaishi nao mitaani
 
FRESH NEWS: UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI.
Leo ningependa turudijamvini kujadili kidogo kuhusu huu mgomo wetu, awali katika sehemu ya kwanza yamada hii, nilijaribu kuainisha madaiyetu, makubaliano na kuacha kwako mwanya wa kufikiri utendaji wa serikali yetu“SIKIVU” ilivyo na inavyofanya hadi sasa (kamahukubahatika kusoma hebu itafute facebook na Jamii forum ili upitishe machoKIDOGO TU ikiwa na thread title UKWELI KUHUSU MGOMO WA MADAKTARI)..leonilifikiri si vibaya tukijadili kuhusu madhara ya mgomo huu.
HALI HALISI HOSPITALINI:
Hospitali ya Taifa Muhimbili, Ocean Road Institute, Temeke,Mwananyamala, Amana, Bugando, Mbeya, KCMC, ST.Francis, Haydom, Dodoma n.k. huku kote hakuna kinachoendelea..madakatarikwa maana ya General practitioner na Specialist, sio Assistant Medical Officer,AMO(KWANI KUNA UTOFAUTI KATI YA NGAZI ZAUDAKTARI KUTOKANA NA KISOMO/ELIMU-nisingependa kwenda katika hili) .. Hii ni TOTAL TOOLS DOWN,(TTD), episode III..
Kama tulivyosema awali hatudai posho, na ongezeko la mishaharatu(hii si priority hata katika madai), ila eti kulingana na majibu ya serikali,tutegemee madai hayo katika next next fiscal year(2013/2014) lakini hebu jiulize
1. Madai ya madaktari yalianza lini?
2. Madiwani waligoma ama kudai mshahara/posho lini??!
3. Priority ya Taifa ni wananchi(kupitia madai ya madaktari) au viongozi(kupitia poshompya za madiwani zilizotangazwa Bungeni)?
4. Nyongeza ya posho ya madiwani imetokea wapi?? ilipangwakatika bajeti?
5. Viongozi au wananchi hamuoni haya??

SISEMI TUNAHITAJI MISHAHARA YETU ILINGANE NA WABUNGE, MAWAZIRI, WAFANYAKAZI WATRA, BOT, n.k..LA HASHA!! ILA UNAPODAI MAZINGIRA BORA YA KAZI, NYONGEZA YAMSHAHARA,POSHO NA UNAPEWA MAJIBU YA DHARAU,.. NA WENGINE KAMA VIONGOZIKUJIONGEZEA(duringthe same period of our claims), HAPO NDIPO COMPARISON INAPOTOKEA, NAKULAZIMISHA TUFANANE NA NYIE!!
Katika hospitali tajwa hapo juu, Wakurugenzi, wakuu wa idarawamekuwa wakifanya vikao na kulipwa 50,000/=TSHS@SIKU toka mgomo kuanza23.06.2012.., Je, wananchi mnayajua haya? Jiulize kuna idara ngapi katikahospitali hizi? Nani anayetoa pesa hizi? Zitatoka hadi lini? Lengo kuu nikushawishi, kushurutisha madaktari turudi kazini… !!

VYOMBO VYA HABARI:
Katika “episode” mbili za “series” yetu hii ya Mgomo waMadaktari, vyombo vya habari vilianza kuripoti kuwa hakuna migomo, hadi palewatu wa HAKI ZA BINADAMU walipoingilia kati!!
Nasikititishwa sana na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC),kutotoa taarifa halisi wakati watu wanazidi kupoteza maisha, kweli hawaoni? Hawajuiau wanapuuzia?
Halafu mnatuitamadaktari si wazalendo? KWELI?? Napata shida sana kuelewa inakuwaje watanzaniawanaumia na viongozi kutotilia maanani madai yetu, ni kweli uhai wa mtuhauwekwi rehani lakini hatukuingiakatika mgomo huu kwa kuweka maisha ya watanzania wenzetu katika mizani, na ndiomaana muda wa mazungumzo ulikuwepo nahata kabla ya mgomo, muda wa wiki mbili ulitosha kujipanga, kwamba kama Serikaliikishindwa kutekeleza madai, AU kuonyesha njia mbadala ya kuyatatua basiijipange kuhudumia wananchi.
Kama leo hii tunaangalia luninga(TV-mfano Mh. W/Afya paleStar TV kukimbia), tunasikiliza redio lakini mambo yanayofanya na serikali nihaya, umekwisha jiuliza ingekuwaje, ama Serikali yetu ingetutendea nini kamatungekuwa hatuwaoni wanachofanya pale Bungeni(Mfano Takwimu za uongo), nakwingineko? Hali hii itaendelea hadi lini?
MKAKATI:
Usalama wa taifa wako kila hospitali, swali ni hili
1. Ni usalama wa Taifa au wa chama tawala?
2. Wanatumia pesa ya nani?
3. Last‘episode” walileta wanajeshi,
KAMA MADAI YAMADAKTARI SI YA MSINGI NA SERIKALI IKOSAHIHI KWANINI WANAJESHI HAWAJATOA HUDUMA KAMA WALIVYOTOA HAPO MWANZO??
KWANINI HAWAKUWA TAYARI HATA WALIPOOMBWA KUFANYA KAZIMNAYYOIITA KAZI YA WITO????

MAKOLIGI (colleague)??
Ni lini wananchi waliingia mkataba na sisi juu ya afyazao??sasa mbona wanatulalamikia na kutushambulia??..nadhani wananchi mnakoseakidogo, dhamana ya afya zenu ni kwa hiyo serikali “sikivu”, hivyo lawama, maombi, na hisia zotepelekeni huko….ila sisi kurudi ni hadi pale madai yataposikilizwa, this time sikwenda kazini halafu yafanyiwe kazi? HAPANA..HII IELEWEKEVIZURI..HATUDANGANYIKI… hadi yafanyiwe kazi na kuthibitishwa au njia mbadala.
Najua wanasema when you get in a fight you should dig, twograves but I guess you should not fightwith someone who has NOTHING to loose,..We either overestimated the power of Government’s responsibility orThey(Government) underestimated our power, and I really doubt of the latter because they KNOW they cant stopus.. you cant stop what you cant catch,because the more they will push us the worse this is going to get…
..Solidarityforever..
 
Tunamsubiri akurupuke tena kuhutubia wazee wa Dar es salaam! Maana ndizo zake hizo!!
 
Back
Top Bottom