Mgomo wa madaktari na kiburi cha watawala wetu, nani anaumia?

Nachelea kuamini kama kweli serikali imetoa kauli kama hiyo kupitia PM. Ila kama ni kweli basi mwanzo wa mwisho wa utawala huu unabisha hodi. Hakuna serikali inayopata mamlaka kutoka mbinguni bali kwa wananchi, sasa usipowasikiliza wenye serikali yao (wananchi) nini wanataka utamsikiliza nani na kwa ajili ya manufaa ya nani. Serikali ingelifikiria hili suala kwa umakini. Ni kweli kwamba haiwezekani wananchi wakaamka na kusema fulani hatumtaki kisha serikali ikatekeleza lakini serikali ilipaswa kuangali kwa nini wanasema hawamtaki na kama hakuna sababu basi wananchi wajulishwe kwamba tuhuma zao dhidi ya mtuhumiwa hazijabainika kuwa za kweli huku serikali ikitoa vielelezo kuliko kukalia ubabe ikidhani inawatisha wananchi.
 
In principle nakubaliana na madai ya madaktari juu ya maslahi yao.
Hata hivyo wamejiingiza katika mtego wa kisiasa, kwa kutaka kushinikiza kujiuzulu wanasiasa.
Thats dangerous.
Mwanasiasa anaishi kwa kupiga domo, na juhudi zozote za kumuondoa kwa domo ni lazima zitapata upinzani mkubwa sana.
Mbaya zaidi ni precedence ambayo madaktari wanataka kuiweka.
Nawashauri waachane na wanasiasa na waendelee kudai maslahi yao.
Kwa hapa saga lilipofikia, madaktari lazima washikilie hapohapo.....wakifanya vinginevyo, consequences zitakuwa kubwa mno na hakuna atakayekuja kuwasikiliza asilani....
na kuna watu watatolewa "kafara".

Madaktari shikilieni hapohapo.
 
ha ha ha ha ha ha ha ha safi tu ngoja tuone itakuwaje teh teh teh teh teh labda pinda atavaa gloves akaoshe vidonda muhimbili
 
Hilo likitokea basi mjue kuna mawili;

(1) Wananchi kuwasusa hao madaktari wa nje kwa ajili ya kutaka fedha kidogo za nchi yetu zitumike kizalendo na zikabaki hapa hapa nchini, na vile vile;

(2) itakua ni mbinu dhaifu ya kujaribu kuzima moto kwa kutumia petroli - kuna uwezekano mkubw tena sana mgomo sasa ukasambaa zaidi kwa ma-kada mengi ya watumishi wetu ili kutaka kujua kwamba sasa serikali itafanya nini hasa nao wakigoma.


kuna tetesi serikali imeomba madakitari 350 kutoka india na 300 kutoka china wanaweza wakaingia muda wowote kuanzia kesho.
 
Hilo likitokea basi mjue kuna mawili;

(1) Wananchi kuwasusa hao madaktari wa nje kwa ajili ya kutaka fedha kidogo za nchi yetu zitumike kizalendo na zikabaki hapa hapa nchini, na vile vile;

(2) itakua ni mbinu dhaifu ya kujaribu kuzima moto kwa kutumia petroli - kuna uwezekano mkubw tena sana mgomo sasa ukasambaa zaidi kwa ma-kada mengi ya watumishi wetu ili kutaka kujua kwamba sasa serikali itafanya nini hasa nao wakigoma.
wasisahau kuleta manesi na wafamasia wa kichina
 
Mlisema serikali haifanyi maamuzi magumu haya sasa wameamua kuacha madaktari wagome.

Lete Wachina na wa Cuba hapa mtu 200 zinapiga kazi ya watu 1000.
Realistic?
.....and quality of the service...!?

Kumbuka, ukarabati wa mwili wa binadamu si ukarabati wa majengo au barabara!
 
Pinda atakuwa anamatatizo ya akili kwa kweli,sijawahi kuona kiongozi bomu kama Pinda,kweli mwehu huwa anamchagua mwehu mwenzake.
 
umempa nyingi sana 2 tu zinamtosha
Pinda, Pinda, Pinda!How many times did I called your name? Be carefulooh! Don't play with those Doctooo!
Yaani Pinda amekosa ubinaadam kabisa! Yaani amekuwa sawa na mtu ambaye anayeweza kumtuliza muuaji aliyeshika Sime asiue mateka wake, anaacha kutekeleza mahitaji ya muuaji mpaka aone muuaji ameanza kuua wa kwanza, yeye anaweka moyo mgumu, anaona wa pili akiuwawa, yeye bado anaweka moyo mgumu mpaka anaona wa tano na wa sita ameuawa ndipo anapotaka kutimiza matakwa ya muuaji, simply because si yeye wala mkewe wala mwanae miongoni mwa mateka wanaouawa. Eti mtoto wa mkulima!
 
Pinda akumbuke wananchi wanauwezo wakumfukuza rais licha ya waziri eg egypt,tunisia,libya
 
Huu mgomo ni wa kisiasa zaidi kuliko kudai masilahi. Nina waomba vijana wetu madktari, achaneni na mambo ya kisiasa kabisa. Taaluma yenu si siasa bali ni kutibu. Msikubali kabisa kutumiwa na wanasiasa.
 
hawa madaktari ni wajinga wanataka kuanzisha mchezo mbaya leo wao shinikizo lao likipitshwa kesho walimu pia watakuja na shinikizo lao sasa serikali gani? Mwisho utasikia na rais asipojiuzulu tunagoma bora wawapotezee tu

Mkuu kwani Serikali ni nani? Au PM anaposema Serikali haiwezi kufanya kazi kwa shinikizo ka Madaktari kuwafukuza kazi hao Mawaziri, hiyo Serikali ndiyo ipi? Ni mtu mmoja au ni Baraza la Mawaziri au ni Rais au ni PM? Ni nini hiki kinachoitwa Serikali? Je ni kweli Serikali nzima ndiyo inakuwa na kigugumizi ktk suala hili la Madaktari? Labda nikukumbushe kitu kidogo, tu kwa uelewawangu mdogo, Serikali ni Wananchi, kwa hiyo wakiamua leo Serikali itoke madarakani wanaweza kufanya hivyo. Kuna mifano mingi ambayo haihitaji hata kuitaja. Hembu fungueni macho na akili zenu.
 
Jamani....huyu mpondwa naona anahamu ya kujiuzulu sema tuu anapotezewa na baba mwanaasha...
 
Ndio tatizo la kuongozwa na viongoz waliokufa na kuoza mana anachosema pinda ni uvundo mtupu..! Yaani inahuzunisha sana kuona kiongoz... cjui niseme anaongea au anaropoka maneno kama hayo. Hi ni aibu sana...
 
Hawa viongozi wamechoka, hawana mbinu mpya za kuiongoza nchi, wanataka watolewe madarakani lakini ndiyo hivyo wananchi hawataki kuwatoa. Wito wangu kwa madaktari, waendelee na msimamo wao, hawa viongozi tutawapandisha kizimbani hata wakiwa wagonjwa au wazee wa kupindukia.
 
Serikali haiwezi kuinuka dhidi ya wananchi wake ikabakia kuwa serikali halali.

Unajaribu kusema nini MM? Ni vyema ukatambua kuwa kuna pande tatu katika sakata hili; wafanyakazi wa sekta ya afya, serikali na watumiaji wa huduma hizi. Ni vyema tusiwasahau watumiaji wa huduma.
 
Back
Top Bottom