Mgomo wa madaktari na dhana ya uwajibikaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari na dhana ya uwajibikaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sungurampole, Jul 14, 2012.

 1. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  [FONT=&quot]Ndugu zangu Watanzania nianze kwa kuwataka tuamke ili tudai haki zetu. Haki zinapatikana kwa kudai siyo kwa kuomba huruma dunia hiyo ya huruma haipo. Hakuna ubishi kuwa watanzania wanakufa kutokana na kukosa huduma za afya, ulinzi na usalama na kesho watoto watakosa masomo. Huduma zote hizi ni haki ya mtanzania na ni wajibu wa serikali kuzitoa. Hivi tunalielewa hili? Na kama tunalielewa tunashindwaje kukubaliana kuwa tumdai nani haki hii. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Najua wako wanaofikiri tuwadai madaktari kwa vile wamegoma. Kwa maoni wangu hapa ndipo tunapokosea. Sisi hatuna mkataba na hawa madaktari, mkataba wetu sisi tumefunga na serikali kuwa kwa kuwapa kura watawale. Halafu tukawapa kodi. Jukumu lao ni kuhakikisha tunapata huduma za afya, elimu, maji, ulinzi, usalama na nyinginezo. Iweje sasa serikali inatusukumia tatizo la mgomo wa madaktari kama vile hilo ni jukumu letu?[/FONT]
  [FONT=&quot]Serikali ndiyo wamewaweka kazini wakigoma sisi haituhusu wakae wayamalize sisi tunachotaka ni huduma.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ninachojiuliza hivi imekuaje TUKAKUBALI HUU MTEGO WA SERIKALI KUKWEPA WAJIBU WAKE NA BADALA YAKE TUNAISHIA KULALAMIKA TU? [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Ukweli hapa tumeingizwa mkenge na hii serikali isiyotaka kuwajibika kwa wananchi wake, wanataka tuwape madaraka ya kutawala basi, zikIja shida tusiwasumbue tuzitatue wenyewe-hii haikubaliki.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Sioni ni kwa vipi sisi wananchi tuwanaweza kuwafikia madaktari waliogoma kiutaratibu ukiondoa ile ya kuomba huruma yao. Tumeona hata taasisi nyingine kama zile za dini zikijaribu kutoa mchango wake ili kumaliza tatizo lakini tumeshuhudia wakiwekewa vigingi. Tatizo ni lile tuliloliongelea hapo juu kuwa kwa kufuata sheria na taratibu hakuna anayeweza kuwasukuma madaktari isipokuwa serikali. Naona kuna jaribio la Mahakama kujaribu kutenda ule wajibu wa serikali lakini sioni wakifanikiwa (labda mimi ni myopic) ila mbele ya njia hii naona giza. Hivi tunatarajia kutibiwa na 'madaktari wa mahakama' - tukikubali hili tuwe tayari kusikia hukumu zitakazomuagiza daktari akudunge sindano. [/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Tafakari hii imenipeleka kuangalia dhana nzima ya uwajibikaji. Namkumbuka mwalimu wetu wahesabu ambaye tulimbatiza jina la ‘mtaalam’ kutokana na umahiri wake katika hesabu. Alitufundisha kanuni moja ya muhimu sana kuwa ukiona heasbu inakusumbua ‘go back and derive it from first principles’ mara zote nimeitumia na imenisaidia. Hivyo nilivyofanya tafakari ya dhana hii ya uwajibikaji ikanikumbusha hadithi ya Kalumekenge aliyekataa kwenda shule. Ilitokea kuwa kijana kwa jina Kalumekenge alitakiwa kwenda shule, Kalumekenge akakataa kwenda shule, Fimbo ikaombwa imchape Kalumekenge ili Kalumekenge aende shule, fimbo ikakataa moto ukaombwa uichome fimbo ili fimbo imchape Kalumekenge ili Kalumekenge aende shule moto ukakataa. Yakaombwa maji yauzime moto ili moto uichome fimbo ili fimbo imchape Kalumekenge ili Kalumekenge aende shule... (wengi tunakumbuka ilivyoendelea). Kwa hili la leo mnyororo huu unaishia kwa sisi kama MAJI tunatakiwa tuuzime MOTO ambalo ni BUNGE ili moto uichome FIMBO ambayo ni SERIKALI ili fimbo imchape Kalumekenge ambao ni MADAKTARI ili watoa huduma ya afya. Dhana hii ya kuwajibishana inajengwa katika mnyororo huu ambao kila mmoja anafanya wajibu wake na kumbana mwingine naye atimize wajibu wake. imejengwa katika msingi kuwa unapomwambie Kalumekenge aende shule unabidi pia umjengee mazingira ya kusomea likiwepo darasa tena lenye dawati, mwalimu na kitabu n.k.[/FONT]
  [FONT=&quot] [/FONT]
  [FONT=&quot]Muhimu nilitaka tu kutoa tafsiri yangu ya hali tuliyofikia na dhana ya UWJIBIKAJI inavyoweza kutoa ufumbuzi wa kudumu wa hili na matitizo mengine yanayofanana na hili. [/FONT]
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Migogoro na migongano ya kazini ni ukosefu wa nidhamu.

  Viongozi pia wajibu wetu mkubwa ni kulinda nidhamu ya kazi.
   
 3. D

  Dr Gustav Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  unapozungumzia nidhamu cjakuelewa unamaanisha upande upi kati ya mwajiri na mwajiriwa,huwezi kuniambia niwe na nidhamu ya uwoga.fikria wewe ndo daktari mama amejifungua kitoto kiko salama
  mara wakati unajiandaa kumruhusu mama aende nyumbani unabaini mtoto kapata magonjwa mapya kutokana na mazingira ya hospitali harafu tena kitoto kinakufa unamruhusu mama kuondoka na maiti ya mwanae,wakati huo huo unaona kila cku watu wanakufa kwa uzembe hivyo hivyounategemea nidhamu gani?
   
 4. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Wimbo Uliouchagua ni mzuri. Mantiki ya wimbo imetekwa na Uongozi Magumashi usioamini katika uwajibikaji na dhamana ulionao...hakuna nidhamu bila taratibu na sheria zinazoongoza WATU wote na kukata Kama msumeno.
   
 5. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Madaktari wangekuwa serious kugoma kushindikiza serikali kuboresha mazingira basi leo hii nina hakika Muhimbili, Mwananyamala, Temeke, Ilala zingekuwa kama Agha Khan. Tatizo misingi ya mgomo yenyewe ni 3.5M
   
 6. Sungurampole

  Sungurampole JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2012
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 987
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hesabu ambayo ni dhambi kwa madaktari lakini halali kwa wengine siyo
   
Loading...