Mgomo wa madaktari-madaktari na serikali ndiyo wa kulaumiwa pekee? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari-madaktari na serikali ndiyo wa kulaumiwa pekee?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanajamii, Feb 3, 2012.

 1. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #1
  Feb 3, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Wiki mbili tangu mgomo wa Madaktari uanze, lawama nyingi zimekuwa zikirushwa kwa Madaktari wenyewe na zaidi kwa Serikali. Swali langu ni je kama ni dhambi ya kuua wataipata Madaktari na Serikali!

  Nauliza hivyo kwa makusudi na kwa kurejea maandiko toka vitabu vitakatifu vya mungu kuwa "MANENO HUUMBA", nikiwa na maana kwamba mogomo huyo umepokelewa kwa namna mbalimbali toka makundi mbalimbali wakiwemo wanasiasa , wanaharakati na hata mtu mmoja mmoja. Nawapongeza sana wale walinaokesha wakiomba suluhu katika Madaktari na Serikali ipatikane ili wagonjwa wetu wasiendelee kuteseka.

  Nirudi sasa kwa wale walionisukuma ni post Thread hii, wale ambao wanafurahishwa sana na mvutano kati ya Madaktari na Serikali na kuwa mavuvuzela mazuri ya kutoa maneno ya ajabi, "mara Serikali imegwaya", "mara Serikali imeshikwa pabaya", "mara Madaktari mshikilie uzi huohuo", ili iweje?

  Ni faida gani tutaipata kwa kuendelea kuona Madaktari na Serikali wanaendelea kusigishana?. Ni sisi hawa hawa ndiyo tunafanya mgomo uendelee, badala ya kuomba suluhu ipatikane, tunashabikia ili mgomo uendelee. Kamwe hatutakwepa dhambi hiyo ya kuua.

  Nalenga makundi matatu ambayo ni kioo cha jamii ambayo kama yangesimama imara yote haya yasingetokea. Waandishi wa habari, wanasiasa na Wanaharakati, siyo siri makundi haya yameteka mgomo huu umekuwa wa kwao na waathirika wakuu ( wagonjwa na Madaktari ) wamekuwa kama wamebaki wanaogelea tu.

  Hata kama ni Demokkrasia na uhuru siyo katika masuala nyeti kama hayo. Waandishi wa habari na Wanasiasa wamechangia kwa kiasi kikubwa muda wa mgomo wa Madaktari kuwa mrefu tofauti na hata Madaktari wenyewe walivyotegemea manake tunao huku mitaani tunawsikia wakisema wenyewe.

  Kama Serikali imeua, au kama Madaktari wameua, hakika sisi tutakuwa tumeua zaidi kutokana ushabiki wetu katika mgomo huo.
   
Loading...