Mgomo wa Madaktari (Leo): Kiburi cha Blandina Nyoni

Kwani aliwapeleka nani hapo? Na uhalali ama sio halali kuwepo hapo kwanini uje mda huu ambao wanadai maslahi yao?

Yani unajibu hoja pasipo hata kuelewa madaktari wanadai nini! Wewe hujui kuwa wanadai maslahi zaidi na pia intern warudi Muhimbili! Wasimame kwenye hoja za msingi, malipo yanayoendana na nature ya kazi na kuboreshwa kwa mazingira ya kazi, period! Hayo mengine wanajichanganya tu na jamii haiwezi kuwaelewa. Kama unafahamu aliyewapeleka hapo basi pia fahamu ana uwezo wa kuwatoa hapo, tatizo liko wapi!
 
Kwa akili hii nadhani tuna hatua kubwa sana ya kupiga hadi kupata maendeleo na ukombozi halisi wa kifikra!
Kwa hiyo bosi wako akiwa kazini na wewe lazima uwe kazini?!
samahani naomba nikuulize swali!? wewe ni mfanyakazi au mwanafunzi?

Kufanya kazi mpaka usiku ni dalili za inefficiency. Sio sifa. Pia sio nzuri kwa afya. Kama siyo tatizo la muundo wa taasisi basi ni tatizo la idadi ya watumishi au planning siyo nzuri. Pia kuna uzembe na kukosa kuwajibika - unacheza karata na kusoma JF asubuhi hadi saa tisa ndo unaanza kazi. Kwa ujumla siyo kitu cha kujisifia kutoka kazini usiku.
 
Mazee usichanganganye habari, kilichotokea MOI ni uzembe wa hali ya juu na usiosameheka kwani taratibu na mlolongo uliouelezea ndivyo inavyotakiwa, kwahili 100% wote waliohusika walitakiwa kufutiwa leseni zao milele na serikali yao kulipa mamilioni ya fidia kwa waathirika, cha msingi Madaktari wanatakiwa washikamane na wabomoe urasimu wa serikali yetu kulipa kiduchu kwa watendaji na kulipa rundo la fedha kwa watu wa juu, fikiria katika hili dai lenu Maprofesa wamo? na kama hawamo sababu kuu ni kwamba wametengewa marupurupu kibao ambayo yanawatosheleza kama wabunge kuliko nyie na hapo ndipo mnapogawanywa kuleta udhaifu kwenye fani yenu,Chukulia mfano Waziri wenu ni daktari au Prof Mwafongo atakutetea nini wewe wakati kila siku anashindana na JK kukata mawingu? SAFARI HII SHIKAMANENI MPAKA KIELEWEKE NA HAWAWEZI KUKUFUKUZENI WOTE

kaka nimesema hapo kwamba hilo suala sio justfiable kabisa wala sijasapoti ila hata kama hutaki matatizo haya kutokea yanatokea na yatatokea cha kufanya ni juhudi za kuyapunguza au "kuyamaliza"
 
Wewe huelewi hata maana ya intern ni nini, na kama ni intern hujui uko wapi wala wajibu wako ni nini. Daktari anafundishwa miaka 5, yule asiye na uwepo anachujwa mapemaa wanabaki wale wenye uwezo na fani husika. By the time anagraduate, daktari huyu ana skills na knowledge za kutosha, kilichobaki ni kumpa exposure ya kazi with MINIMUM SUPERVISION, marudia kwa kiswahili, na usimamizi mdogo. Lengo ni kumjengea uwezo wa kujiamini kufanya kazi na maamuzi pasipo kusimamiwa, anapoona anashindwa ndio hapo senior anamsaidia kidogo, na imani ni kuwa hatarudia kuuliza kitu hicho tena. Hiyo ndio maana ya internship. Waende vijijini humo hamna umeme na operation zinafanyika kwa mwanga wa vibatari ndio watajifunza vizuri kufanya kazi na kutoa
maamuzi in real world, sio kusema ati wapo mafunzoni. Mafunzo yalishakwisha, sasa ni wakati wa kufanya kazi, sio kulialia oooh Muhimbili ndio penye specialists, kwani si waliwafundisha mkiwa wanafunzi.

A medical intern is a term used in the United States for a physician in training who has completed medical school. An intern has a medical degree, but does not have a full license to practice medicine unsupervised.
So who will supervise this intern huko unakosuggest ....akawe supervised na Clinical officer maana huko unakokusema hata MD tu hawapo..acha ushabiki kuongelea kitu usichokijua na jua kuwa hapa we a talking of man's life nafikiri wewe labda ndio utapenda daktari wa namna hii aje kukuhudumia, daktari ambaye hajaiva!!!!!
 
Pia anapata mshiko kwa kuleta maktari kutoka appolo india kuja kuchagua wagonjwa wa kupeleka india wakati operation zinafanyika vema bongo. Anawalaza southern sun kwa kodi zetu. Hata kumwagilia maua muhimbili tenda kachukua yeye mama analindwa na nani?
 
A medical intern is a term used in the United States for a physician in training who has completed medical school. An intern has a medical degree, but does not have a full license to practice medicine unsupervised.
So who will supervise this intern huko unakosuggest ....akawe supervised na Clinical officer maana huko unakokusema hata MD tu hawapo..acha ushabiki kuongelea kitu usichokijua na jua kuwa hapa we a talking of man's life nafikiri wewe labda ndio utapenda daktari wa namna hii aje kukuhudumia, daktari ambaye hajaiva!!!!!

Wewe ndio usiyejua unachoongea, unalinganisha Tanzania na Marekani, huh! pole. Nchi zote zilizoendelea kila chuo cha udaktari kina teaching hospital. Wilayani kuna madaktari wanaoweza kutoa supervsion, nendeni huko mkafanye kazi, sio mpige kelele za kukaa mjini kwa kisingizio cha specialist. Kwanza hamuhitaji kusimamiwa na specialist maana mkimaliza intern mnakuwa GP-general practitioner tu. Kama ni maslahi mpo sawa, hayo mengine mnajidhalilisha tu.
 
Yeh hauwezi ndio Maana akaitwa surgeon... Kazi ya kuchukuwa history ni ya physicians... Yeye anakuja kupitia kilichoandikwa na na ku check ct au MRI kama zipo ..Na kuna watu ambao kazi Yao ni kumtayarisha mgonjwa ... Ma nurse wa chumba cha upasuaji ... Kuna ma anaesthesioligosts na hao wana tangulia kumuona mgonjwa . Surgeon yeye ni wa mwisho anafika pale mgonjwa yupo usingizini na kama ni operation ya kichwa basi amekuwa kesha funikwa usoni . Hapa na assume unajuwa mgonjwa anafunikwa vipi wakati wa surgery

Kwanini aje alaumiwe surgeon while WaPo wale ma nurse wa chumba cha upasuaji wa kutayarisha mgonjwa ..?

Sikujua kuwa surgeons hawana tofauti na wachinja ng'ombe machinjioni. Yaani anachotafuta yeye ni shingo ya ng'ombe tu apitishe kisu.
 
Wewe ndio usiyejua unachoongea, unalinganisha Tanzania na Marekani, huh! pole. Nchi zote zilizoendelea kila chuo cha udaktari kina teaching hospital. Wilayani kuna madaktari wanaoweza kutoa supervsion, nendeni huko mkafanye kazi, sio mpige kelele za kukaa mjini kwa kisingizio cha specialist. Kwanza hamuhitaji kusimamiwa na specialist maana mkimaliza intern mnakuwa GP-general practitioner tu. Kama ni maslahi mpo sawa, hayo mengine mnajidhalilisha tu.
mkuu kama hujui kitu usikurupuke na kujidhalilisha.huna hoja na unafoka bila kuelewa kinachoongelewa ni nini,kwa maneno mengine unafikiria kwa kutumia ugwe mgongo(spinal cord) na sio ubongo.
kwanza fahamu kuwa medicine ni universal, anachofundishwa daktari wa marekani ni sawasawa na anachofundishwa daktari wa rwanda au tanzania.hakuna chuo cha udaktari tanzania kisicho na teaching hospital hata IMTU na UDOM(vyuo vipya) wana utaratibu wa kutumia hospitali za mwananyamala na dodoma kwa ajili ya kufundishia.
ningependa unitajie wilaya moja tu yenye specialist wa kumsimamia intern.kwa taarifa yako hakuna wilaya tanzania hii yenye madaktari(M.D) zaidi ya watatu ambao kisheria hawaruhusiwi kumsimamia intern.general practioner sio daktari bali ni mtoa huduma ya kwanza kabla ya kumpeleka mgonjwa kwa daktari.msipende kukurupuka kama hamjui vitu.are u mentally retarded??
 
wanafahamu dhahiri hakuna wa kugoma pale,na hata wakigoma siku moja tu...lakini la zaidi watakufa watanzania na familia yake haitibiwi mwananyamala..
 
Wewe ndio usiyejua unachoongea, unalinganisha Tanzania na Marekani, huh! pole. Nchi zote zilizoendelea kila chuo cha udaktari kina teaching hospital. Wilayani kuna madaktari wanaoweza kutoa supervsion, nendeni huko mkafanye kazi, sio mpige kelele za kukaa mjini kwa kisingizio cha specialist. Kwanza hamuhitaji kusimamiwa na specialist maana mkimaliza intern mnakuwa GP-general practitioner tu. Kama ni maslahi mpo sawa, hayo mengine mnajidhalilisha tu.

Mfano aliokupa mazee ndugu yangu Pax ni valid sana kwa mazingira ya Tanzania huo ndio mfumo.
Na kwa taarifa yako pia daktari akigraduate anakuwa sio General practitioner(GP) as you try to imply here kwani haruhusiwi kupractice hadi pale atakapofanya mazoezi chini ya usimamizi(internship) wa Seniors wake(Mabingwa) ndipo apewe licence(Registered) na kuweza kuwashika wagonjwa, La afanye kazi za maofisini na madaktari wengi ambao hawajafanya interniship wanafanya kazi hizi za maofisini hapa Tanzania kwani wao hawahitaiji kupractice na hawatakuwa GP's hadi watakapofanya internship......
Huko mawilayani ukimpeleka huyo intern yeye ndie atakuwa senior kwa wengine pia hao madaktari siku hizi mtazamo umebadilika sana wengi wanakwenda sana huko vijijini wanapopata nafasi ila shida nyingine huko mawilayani hawaaombi madaktari kwenye vibali vya ajira kwani uatakuta mkuu wa idara ya afya si daktari hivyo wanaogopa kwamba kama wakiomba daktari basi akiripoti hap atakuja kuchukua nafasi yake naa hii ndio style iliyopo saizi ukiwa unaongea fanya utafiti kwa taarifa yako tu daktari anapokuwa shuleni anakuwa anaassist most of the time akiwa intern anatakiwa kufanya kazi under supervision mfumo una mlolongo mrefu i sana jaribu kufuatilia wewe mwenye kama una interest ya kujua lakini ila Mazee amejaribu kukufafanulia vizuri tu na wewe unaonekana huna uelewa wa hili........
 
Hapa sasa nimekubali hata nafasi ya katibu mkuu wa wizara ni ya kisiasa... LAZIMA TUNATUMIA MASABURI KUFIKIRI
 
Mkuu Karata, kwanza nakushukuru kwa kuweka hii organogram ya wizara ya afya, sikuwa naifamu kabla na sikufanya utafiti wa kutosha. Pamoja na structure hii, inavyoonekana ni kuwa vitengo au idara kama councils, boards, commisiion, directorate of planning, internal chief audit n.k n.k wanawajibika moja kwa moja kwa katibu mkuu na idara nyingine kama curative, au emmergence prepadness zinawajibika kwa mganga mkuu kama technical personnel. Karata, shida inakuja pale wale wa juu kama councils au boards au chief accountant kuwajibika kwake, hiyo ndiyo shida, kwa nini msajili wa madaktari au wauuguzi au maabara wawajibike kwake wakati structure haisemi hivyo???, mfano wakati interns wamerudishwa wizarani, nasikia waliokuwa wanaandaa kuwapost intern ni mabaraza lakini kwa maelekezo ya cmo, why?? maana nategemea baraza la madaktari ndio linajua wapi kuna specialist na wapi panafaa kupelekea interns, na ndio maana waliwapanga huko kulingana na uwezo wa hospitali husika, lakini cmo ndio alitoa maelekezo hayo, sasa hiyo structure ina mantiki??? nifafanulie karata. Na kama tatizo ati wamekuwa wengi, kwa nini katibu mkuu aliridhia wpelekwe huko, maana naambiwa msajili wa madaktari ndiye anyempanga intern doctor sehemu husika na kumwandikia katibu mkuu, ili malipo yaweze kufanywa kwa intern husika na katika hospitali husika.
Mkuu ww ni great thinker, usiandike kwa kusikia tu, fanya research. Katibu Mkuu, Blandina Nyoni ni mtendaji Mkuu wa Wizara, yy ndo Accounting officer wa Wizara yote na Mganga Mkuu, Deo Mtasiwa ni technical person wa Wizara, yaani kwa kifupi wao ndo Wizara. Waziri na Naibu Waziri ni Viongozi wa kisiasa tu.

Tazama Structure ya Wizara ya Afya hapo chini.

structure.jpg
 
Kinachogombaniwa sio kuhamishiwa mikoani kwa Interns but ni ubabe wa serikali, iweje udai haki yako then uhamishwe na kama adhabu vile wakarudie mwaka wote?!
Suala la kumhamisha specialist ni kichekesho! Hospitali ZOTE za mikoani ni hovyo mara mia kulinganisha na Muhimbili, sasa unamhamisha daktari bingwa wa upasuaji wa mifupa kwenda kwenye hospitali ambayo hata kisu cha kufanyia upasuaji hakipo, akafaye nini?
Wameshauriwa na wenye hekima, waache ufisadi ili waimarishe hospitali za mikoa kwa vifaa vya upasuaji, madawa, wodi na supporting staff then ndio wapeleke specialists, lakini kama kawaida yao wanasema "serikali haina hela" Hiyo wanayoifisadi sio hela ya serikali?!
 
Usisahau hili:
Alivyoingia Afya alimuua mtaalam mmoja anaitwa Manumbu. kisa cha kuuawa huyu mzee ni kuzuia Tshs. 400,000,000/= zisiibiwe na huyo mama!!!

Mama huyu aliwahi kuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali pale Hazina, akawa Katibu Mkuu Maliasili akawang'owa wakurugenzi waliokuwa visiki pale na sasa yuko Afya huko madaktari mtaipata
 
Hapa ndipo madaktari wanapokosea kama mtizamo wao ndio huu wa Zimmerman. Hapa unachotafuta ni Daktari awe na mshahara mkubwa kuliko watumishi wengine wote au maslahi yaendane na kazi? Hebu mfikirie rubani anayeongoza ndege yenye abiria 480, there is no room for error, hakuna cha kusema ati nurse alimix mafaili, one mistake half a thousand people are dead! mfikirie mtu anayetreat maji tunayotumia dar es Salaam kutoka mto Ruvu, no room for errors, mix-up of chemicals my dear the whole city is dead! Kwa hiyo hiyo arragance uliyo/mliyonayo is a grave mistake. Nchi nyingine zilizoendelea unazozitolea mifano, mishahara iko very close hamna tofauti kubwa kati ya dereva wa basi hata na daktari, wote wanatoa huduma muhimu kwa jamii. Sema mishahara inakidhi mahitaji. Madaktari wanayo baadhi ya madai ya msingi kabisa, suala la posho ni la msingi.

Kwa upande wa pili, madaktari nao wana matatizo makubwa sana na ndio maana naona baadhi ya watu wanaandika kwa hisia hapa. Nadhani kila mmoja wetu ameshatendwa in one way or another na wafanyakazi wa sekta ya afya. Na hii kwa kiasi kikubwa inatokana na arrogance waliyonayo kuwa they are the best, most important professionals, which is not true at all, kila mtu na fani yake ana umuhimu kwa jamii, you need to look it from the system perspective na sio kama units. Fani ya udaktari imeoza, purely rotten, wengi wana majina ya udaktari but ni wababaishaji wakubwa, hakuna kitu, empty headed enjoying being called with all sweet prefixes in the street, Dr, Dr! Madaktari wa leo hawana ethics, na mwili wa binadamu wanauchukulia kama wa mnyama tu, they dont care at all. Nasema wengi ni wababaishaji, lakini wapo wazuri na makini, wanaopenda kazi yao.

Mwisho, system nzima ya afya inahitaji complete overhaul, haiwezekani mgonjwa atoke Amana anafikishwa Muhimbili ati anapokelewa na Intern, ni upuuzi mtupu huu. Hospitali ya Rufaa inageuka ya kujifunzia tena? mgonjwa aliyezidiwa anaonwaje na daktari mwanafunzi kama sio uwendawazimu huu! nchi gani inafanya huu upuuzi? Hospitali za rufaa zinatakiwa 24 hours zina specialists, za kwetu ati zina interns. Akili za wapi hizi? Wagonjwa wengi naamini zaidi ya nusu wanafariki sio kwa maradhi yanayowasumbua, hapana wanakuwa mismanaged. Hili linajulikana, mara intern mara mwanafunzi wa masters mara nurse mara huyu, mpaka mtu anakata roho anafanyiwa mizaha tu.

Ungekuwa unajua maana ya teaching hospital na jinsi inavyofanya kazi zake usingeandika huu upupu hapa,mi sio daktari lakini inelekea hujui hata intern au resident ni mtu gani.
 
Mfano aliokupa mazee ndugu yangu Pax ni valid sana kwa mazingira ya Tanzania huo ndio mfumo.
Na kwa taarifa yako pia daktari akigraduate anakuwa sio General practitioner(GP) as you try to imply here kwani haruhusiwi kupractice hadi pale atakapofanya mazoezi chini ya usimamizi(internship) wa Seniors wake(Mabingwa) ndipo apewe licence(Registered) na kuweza kuwashika wagonjwa, La afanye kazi za maofisini na madaktari wengi ambao hawajafanya interniship wanafanya kazi hizi za maofisini hapa Tanzania kwani wao hawahitaiji kupractice na hawatakuwa GP's hadi watakapofanya internship......
Huko mawilayani ukimpeleka huyo intern yeye ndie atakuwa senior kwa wengine pia hao madaktari siku hizi mtazamo umebadilika sana wengi wanakwenda sana huko vijijini wanapopata nafasi ila shida nyingine huko mawilayani hawaaombi madaktari kwenye vibali vya ajira kwani uatakuta mkuu wa idara ya afya si daktari hivyo wanaogopa kwamba kama wakiomba daktari basi akiripoti hap atakuja kuchukua nafasi yake naa hii ndio style iliyopo saizi ukiwa unaongea fanya utafiti kwa taarifa yako tu daktari anapokuwa shuleni anakuwa anaassist most of the time akiwa intern anatakiwa kufanya kazi under supervision mfumo una mlolongo mrefu i sana jaribu kufuatilia wewe mwenye kama una interest ya kujua lakini ila Mazee amejaribu kukufafanulia vizuri tu na wewe unaonekana huna uelewa wa hili........

Unayejiita Dr Klinton acha kuongopea watu ukifikiri kuwa wote JF hawajui chochote, hapo penye red mbona umeandika kama vile unatumia masaburi?

Toka lini na wapi Intern anaweza kuwa Senior kwa DMO? Mfumo wa wizara ya Afya ipo wazi kwa nafasi za ma DMO kwamba ni lazima awe na MD/MPH au tu awe MD, sasa hapo intern aliyemaliza Muhimbili, KCMC, Bugando etc vipi kicheo au kwa kufuata seniority intern awe juu? yaelekea kweli hujawahi kufika mawilayani na kuona ndugu zenu (MDs) waliograduate zamani wanavyohenya kukimbizana na Posho huku wakiwaachia Hospitali AMOS waendelee na kazi na ndio maana unafikiri kuwa intern akienda wilayani anakuwa Super Guy ...Big No , Intern wilayani anabaki kuwa ni Dr tu na mbaya zaidi akienda huko na kumkuta Clinical officer wa mwaka 1980 frustration zitamzidi pale atakapogundua kuwa starting salary yake hamwiingii Junior wake ambaye ni huyo Clinical Officer
,

Pili unajaribu kudanganya watu kuwa Wilayani hawaombi MDs, Laiti ungelijua kwa undani usingesema hayo kwani ukweli ni kwamba wanaomba lakini Fedha wanazotengewa ni kidogo na hazitoshi kulingana na mahitaji halisi, serikali yenu HAINA PESA ndio maana mnagombana nayo kwa kuwa wao wanavimbiwa nyie mnapata Constipation kwa sababu ya kula Chips dume mtaani

Angalia hapa..http://www.moh.go.tz/waliopangwa vituo.pdf

Narudia kusema Mkuu wa Idara ya Afya wilayani Kinondoni ni MD, Namtumbo pia ni MD, Kilombero ni MD, Kasulu ni MD..NDIVYO ILIVYO KOTE ISIPOKUWA WILAYA CHACHE SANA ...MWISHO ACHA KUFIKIRI WOTE HATUJUI

Vipi kamgomo kamefikia wapi na Mtoto wa Mkulima? Je akikulilieni kama kawaida yake mtasitisha mgomo au mnataka kumuliza tu mtoto wa watu halafu mmumpotezee? Wenzenu enzi hizo walifanya kweli mpaka waziri Chiduo akang'oka wizarani na baadaye kupata peresha na kufa ....hii Prof Sarungi ndio alikuwa Think tank wa hii kitu na yeye ndio akaukwaa uwaziri kwa kuuma kotekote, kwa madaktari wenzie anasema hivi then akienda wizarani anasema vile, akitoka wizarani anakatisha pale Magogoni moja kwa moja anateta na mkuu wa kaya, Nyie Road map yenu ikoje? SIASA MCHEZO MCHAFU LAKINI WANG'ANG'ANIENI MPAKA MPATE HAKI YENU
 
Usisahau hili:
Alivyoingia Afya alimuua mtaalam mmoja anaitwa Manumbu. kisa cha kuuawa huyu mzee ni kuzuia Tshs. 400,000,000/= zisiibiwe na huyo mama!!!

Usitulishe nyamafu bwana, Manumbu alikuwa Director of Planning pale wizarani au ndio unamaanisha mtaalamu wa Planning?

Hivi Mtaalamu kwa kithungu inakuwaje vile?
 
Sikujua kuwa surgeons hawana tofauti na wachinja ng'ombe machinjioni. Yaani anachotafuta yeye ni shingo ya ng'ombe tu apitishe kisu.

mkuu medicine sio kama unavyoifikiria weye.. anyways ni ngumu kwa mtu wa kawaida kumuelewesha... au maybe kwa sytem za huko bongo surgeon anafanya kazi zote anyways :focus: sasa ...
 
wandugu ee hiVi kama kila mtu ata claim kima cha chini kiwe 3.5 tutafika?hawa madaktari nao wamezidi jamani dUuh
 
Back
Top Bottom