Mgomo wa madaktari: Kigwangwalla kufukuzwa CCM?

Ghasia mwenyewe alilazimisha ushindi,mtwara vijijin,na mana hataki tena kugombea vijijin,anataka mtwara mjin.5

Hili ninalijua sana, mpaka nashangaa nguvu za kumsulubu mwenzake anazitoa wapi. Ghasia alikataliwa kwao tangu 2005, nashangaa anashindaje chaguzi hizo
 
Hapa ndio kipimo chake cha uongozi, yuko upande wa wananchi au upande wa mafisadi? Fanya Maamuzi MAGUMU!

[h=6]Hamisi Kigwangalla
[/h][h=6]Natafakari yaliyonisibu! Uamuzi ninao, nasubiri kitu kimoja tu kabla sijachukua hatua yoyote ile![/h]
 
Kigwa nipo nyuma yako maana chama chako hakina mashiko na kimepoteza mwelekeo, ccm kama ni gari basi halina taa na hivyo haliwezi kutembea usiku.
 
kwa hiyo wanapenda wabunge wote wawe upande wa serikali haka ktk maovu hivi kazi za bunge ni nini Adam lazima ajui kuwa mbunge anachaguliwa na wananchi ili aisimamie serikali kutiza wajibu wake kwa wananchi na siyo mbunge anakuwa sehemu ya serikali kama waziri asiye na wizara

Big Up HK komaa hadi kieleweke Ila uwe makini sana
 
ccm na serikali yake wanadhan hii ni ya kwao peke yao.kama kuikosoa serikali ni kutolelewa vizuri, basi sisi wapiganaji na wakosoa serikali hatukulelewa vizuri,ila siku tukishika dola ndo watajua tulilelewa vizuri zaidi.wakae mkao wa kuliwa hasa ghasia.kigwangwala namsuport.
 
Wanabodi, hii imetoka jikoni kabisa:

Jana jioni majira ya saa 10, kikao cha kamati ya wabunge wa chama cha mapinduzi ilikutana Dodoma kujadili mambo mbalimbali na hapo ndipo suala la mjadala wa sakata la madaktari ililipoibuliwa na Mbunge wa Nzega kuhusishwa na mgomo huo.

Mhe. Hawa Ghasia ambaye alimtukana Kingwangallah kuwa ni mbishi, jeuri na hakufunzwa na wazazi wake na kwamba CCM hawatomuweza. Alisema Kingwangallah afukuzwe chamani na yeye (Ghasia) yuko tayari kwenda kupiga kampeni Nzega kuhakikisha jimbo linarudi CCM.

Kikao kiliazimia kupeleka mapendekezo ya kumfukuza kwenye kamati ya uongozi. Kikao hicho kimekaa leo jioni kuanzia saa 10. Bado hatujajua wameazimia nini mpaka sasa. Je akifukuzwa ataenda Chama gani? Bado hiyo haijajulikana...ila taarifa kutoka kwa watu walio karibu naye zinasema kwamba ameamua kujiuzulu kabla ya kusubiri kufukuzwa.

'Tayari ameishaanda barua na anasubiri tu kuitwa ili aiwasilishe' kilisema chanzo cha habari.

Source: ndani kwa ndani - Dodoma

Silaha pekee ya kumuokoa Kigwangala ni kutishia kutoa barua ya kujiuzulu. CCM wanajua kuwa watapoteza uchaguzi mdogo huko Arumeru, hawako tayari kuona jimbo la Nzega wakiliachia hivihivi ukizingatia na majeraha waliyopata kwenye kura za maoni nzega 2010. Ghasia asifikiri kampeni ya kushinda jimbo ni sawa na kuinua mguu kitandani.
 
Walidhani kumwondoa Selelii wametibu donda la Ubishi na usulubishi wa Serikali. Hata kama watamfukuza atatokea mwingine tu. Fukuzeni basi na mzee Sitta.
 
Dr . Ondoka huko, hawatakuchelewesha angalia mpambanaji Mwakyembe hana nywele zimepukutika zote. Those guys are ready to do anything to keep rulling this Country.

Anaondoka kweli, kasema anajipa muda kutafakari ili aone ni nini cha kufanya
 
Walidhani kumwondoa Selelii wametibu donda la Ubishi na usulubishi wa Serikali. Hata kama watamfukuza atatokea mwingine tu. Fukuzeni basi na mzee Sitta.
Subutuuu!!!...............CCM hawafukuzi mwanachama yeyote, hata awe jambazi au mnyang'anyi....actually, hao ndio wanaopendwa zaidi ndani ya chama.

Tunazoziona hizi ni mbinu za kuwaziba wengine wote midomo ili issue ikiibukia bungeni leo, wasithubut kunyanyua midomo yao kuwatetea madaktari.
 
hiyo habari tayari imekwishawekwa humu jamvini na tena imeeleza nini kilichojiri kwenye kikao cha ccm.sasa wewe nawe umeweka habari isiyojitosheleza badala ya kumwaga kila kitu ili ambao hawajaona ule uzi mwingine waweze kuchangia huku.funguka mkuu!
 
Habari za ndani kabisa mpango wa kuvua gamba kigwangalla upo katika hatua za mwisho ndani ya chama, kama unabisha subiri uone!

Inaama hawa jamaa wa sisiem wanapenda sana watu wanaosema uongo. Ukisema ukweli si mwenzao na kwa hiyo watafurahi nyimbo lingine kuwa wazi eti kwa sababu Dr. Kingwangala kawaunga mkono madakitari wenzenke? Hizo gharama za uchaguzi si wangewape madaktari na ili wamalize mgomo wao? Wakifikia uamuazi tutajua kuwa sisiem hawapo kwa ajili ya kutetea maslahi wa wananchi ...
Tunasubiri tuoni ...
 
Back
Top Bottom