Mgomo wa madaktari: Kigwangwalla kufukuzwa CCM?

Massenberg

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
1,173
1,370
Wanabodi, hii imetoka jikoni kabisa:

Jana jioni majira ya saa 10, kikao cha kamati ya wabunge wa chama cha mapinduzi ilikutana Dodoma kujadili mambo mbalimbali na hapo ndipo suala la mjadala wa sakata la madaktari ililipoibuliwa na Mbunge wa Nzega kuhusishwa na mgomo huo.

Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zinasema wabunge wa CCM ambao ni mawaziri walipata nafasi ya kumsulubu Kingwangallah kama wanavyotaka ukizingatia kuwa amekuwa akiwabana sana mara kwa mara akiwa bungeni kutokana na misimamo yake ya kutetea haki na ukweli.

Mhe. Adam Kighoma Malima alikuwa wa mwanzo kuongea na aliutumia muda wake wote kumshambulia Kigwangallah akidai ndiye aliyefadhili mgomo wa madaktari na ndiye aliyeendesha harakati za mgomo huo mwanzo hadi mwisho. pia aligusia kuwa Kingwangallah hakuongoza kura za maoni, alikuwa nafasi ya tatu nyuma ya Bashe na Selelii, lakini chama kilimpendelea na kumpa nafasi yeye. Malima alimtaka Mwenyekiti wa kikao hicho, ambaye ni Waziri Mkuu, amtake Kingwangallah kupanda mbele ya podium na aeleze uhalali wake wa kuwa kwenye kikao cha mgomo wa madaktari na kushawishi wagome na aseme kama yuko CCM ama la! Na kama yuko CCM kwa nini hakuisaidia serikali? Baada yake alikuja Mhe. Hawa Ghasia ambaye alimtukana Kingwangallah kuwa ni mbishi, jeuri na hakufunzwa na wazazi wake na kwamba CCM hawatomuweza. Alisema Kingwangallah afukuzwe chamani na yeye (Ghasia) yuko tayari kwenda kupiga kampeni Nzega kuhakikisha jimbo linarudi CCM.

Wabunge wengine waliunga mkono hoja hiyo huku wakionesha kusikitishwa na hatua ya Mbunge huyu kushiriki kwenye mgomo wa madaktari na kuwahamasisha kuibana serikali mpaka kieleweke! Mbunge Kingwamngallah alionekana kukosa support ya wabunge kabisa na hata wale walioonekana kumuonea huruma walinyamaza na hawakutaka kuonekana wazi wazi kabisa kuwa wako na Kingwangallah. Mawaziri walimshambulia mpaka basi tu.

Kikao kiliazimia kupeleka mapendekezo ya kumfukuza kwenye kamati ya uongozi. Kikao hicho kimekaa leo jioni kuanzia saa 10. Bado hatujajua wameazimia nini mpaka sasa. Je akifukuzwa ataenda Chama gani? Bado hiyo haijajulikana...ila taarifa kutoka kwa watu walio karibu naye zinasema kwamba ameamua kujiuzulu kabla ya kusubiri kufukuzwa.

'Tayari ameishaanda barua na anasubiri tu kuitwa ili aiwasilishe' kilisema chanzo cha habari.

Source: ndani kwa ndani - Dodoma
 
Kuwa CCM haina maana kusapoti vitu vyote hata kama ni hovyo. Dhana ya chama kwanza ilashakufa, kama kuna kitu kizuri alikifanya wala asitishike. Kuna watu wanafikiri nchi hii ni yao. that is fallacy.
 
Dr.Kigwangala karibu CDM wewe ni jasiri, kuwa mwana ccm si kukubaliana na kila jambo lifanywalo na serikali achana nao naamini nzega watakusaport mtetezi wao.
 
Huko ndiko kufilisika kwa CCM, Acha wamfukuze tu, kwani CCM ndio wazazi wake?? Kwani sie tunaopeta mitaani mbona hatuna mahusiano na CCM na Serikali yake kwa lolote? Huko ni kuishiwa hoja na ndio anguko lao. Dr achana nao, amua kukitosa chama halafu tuone wanasemea wapi. Tatizo la Serikali hii linasahau kitu kimoja muhimu kuwa, Hakijagundua kina deal na society ya namna gani.Na hilo ni kosa kubwa.
 
CC! hawana uwezo wa kufukuza mbunge/kumvua mtu uanachama, si sera yao, hao wanaandaa mazingira ya kuwatisha wabunge ili kesho hili suala likiibuka bungeni wawe wameshafungwa midomo.

Naomba waelewe kuwa wananchi wanafuatilia hili suala hatua kwa hatua, hii nchi si ya CCM wala CHADEMA au vyama vya siasa, ni ya wananchi ambao ndiyo wengi kushinda hao wanachama wa vyama.
 
Hahahaahaaa! Waziri kanichekesha eti dr hakufunzwa na wazazi wake! Kwa hiyo kuitetea 'sirikali' hata kwa kile usichoamini au uonacho ni makosa ndio unaonekama umefunzwa na wazazi! Lol! Kweli akili ni nywele...!

Hata hivyo hawana ubavu wa kumfukuza! Wameshindwa kufukuza mafisadi walogoma kujivua gamba wamfukuze dr kwa kushiriki kikao? Labda!

Ndio wataujua utamu wa "UJIRA WA MWIHA"! Raaaha kweli kweli! 'Senema' imenoga!
 
Homeboy Kigwangalla kwa hili kama ni kweli, una support yangu mia kwa moja bila wala kuuliza.

Kila mpigania wanyonge na HAKI, basi mie nipo naye bila kujali chama.

Simamia unachokiamini na Mungu atakulipa, kama si leo basi kesho.

TUPO NANYI MADAKTARI WETU. Kufanikiwa kwenu ni kufanikiwa kwetu. KITAELEWEKA.
 
Dr . Ondoka huko, hawatakuchelewesha angalia mpambanaji Mwakyembe hana nywele zimepukutika zote. Those guys are ready to do anything to keep rulling this Country.
 
Ghasia mwenyewe alilazimisha ushindi,mtwara vijijin,na mana hataki tena kugombea vijijin,anataka mtwara mjin.5
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom