Mgomo Wa Madaktari: Jee, Serikali Kuwafukuza Kazi Kwa Summary Dismissal kwa "Insubordination"?

Mfano mzuri kweli - tatizo mwanajeshi wa Tanzania akigoma sasa hivi unafikiria Kenya au Rwanda watatuvamia? au Uganda? Umuhimu wa mwanajeshi unakuja wakati wa vita! Nje ya vita mwanajeshi ni tishio la watawala siyo wananchi.
Mkuu umesahau ya Nyerere mwaka 1964 ya kina Sokoine?..Hivi mzee huyu yuko wapi unajua he can be a very good President!

Leo hii Syria anapumua kwa nguvu ya Jeshi tu..Hawa jamaa wakigoma, acha Kenya wala Uganda machinga wenyewe wataingia barabarani barabarani wanajua JK hana walinzi..
 
Nimefuatilia thread nyingi na kuna baadhi yetu wanasema mgomo wa Daktari unaumiza wananchi. Ni kweli kwa mtazamo wa haraka, ukweli unabaki pale pale wananchi wanaumizwa na serikali kila siku. Hivi kwanini tuone mgomo wa madaktari unaumiza wananchi na tusahau kuwa jitihada zao zina lengo la kutusaidia pia! Kipi bora kugoma ili huduma ziimarishwe au kukaa kimya na kuona Wabunge 320 wakilipwa milioni 64 kwa posho tu kwa siku kwa kukaa eneo lao la kazi Dodoma.

Bajeti ya Hospitali moja ya wilaya ni chini ya milioni 500, sawa na posho tu za wabunge waliokaa katika viti vyao vya kazi kwa siku 9 tu. Kwanini tusione serikali inaumiza wananchi kila siku tuone leo. Hivi kufa kwa kukosa huduma muhimu na kufa kwa kukosa Daktari aliyegoma vina tofauti!! Maana watu wanakufa kila siku kwa kukosa dawa, utaalamu au vipimo na hilo hatulioni kama uuaji.

Kwa vile serikali inaamini katika demokrasia, basi upana wake unafikia katika vyama vya wafanyakazi na halali ya migomo kama silaha ya mwisho ya mfanyakazi. Ndivyo ilivyo duniani kote kwenye unions n.k.

Mkapa aliwahi kuwafukuza Madaktari na kuweka wa Jeshi. Pengine hili linawezekana kwa Muhimbili kwa siku mbili tatu, swali ni je huko wilayani na mikoani kuna madakatari wangapi wa kuziba mapengo yatakayobaki? Kwa taarifa tu jeshi linahitaji wataalam wa fani ya udaktari, hatua zozote zitakuwa za zima moto na si ufumbuzi wa tatizo.
Tatizo limejirudia kwasababu hakuna aliyewahi kulitibu, kila mtu alikuwa anatoa dawa ya kupunguza maumivu.

Kinachowasukuma madakari kugoma si kukosa uzalendo, ni kitu kinaitwa 'class warfare' yaani vita vya madaraja ya jamii. Sijui kwanini yeye awe na uzalendo wa kucheza na mazingira hatari wakati anajua nchi ina uwezo wa kuweka mazingira bora. Anajua kwasababu haiwezekani mbunge mmoja akikaa kwenye kiti chake kwa siku 3 ni mshahara wa daktari. Naye kama mwanadamu anajiuliza uzalendo unaanzia wapi na unaishia wapi na akina nani wanapaswa kuwa wazalendo.

Nitashangaa kama Rais ataingilia kati. Nashangaa kwasababu wakati tunalalama kuhusu ulafi wa wabunge na umasikini unaotusakata yeye kasukuma faili kwa Pinda ili asaini posho ya laki 200 kwa kuingia mjengoni tu achilia mbali mshahara na mafao mengine.

Wananchi, tatizo si madakatari wanaotaka mboga za watoto bali daraja teule la serikali linalofanya kazi pamoja na daraja teule la wabunge wanaodhani wana matumbo bora na haki ya kula hadi kukomba mwiko.

Hawa akina Blandina, Mtasiwa ni wafanyakazi wa matabaka teule,tatizo lipo kwa waliopewa dhamana ya nchi na hawa ndio wanaobeba roho zinazoteketea na damu ya wasio na hatia.Tusipofanya maamuzi ya kuwaambia sisi ndio waajiri wao, basi tutaendelea kunyanyasika na kupoteza uhai kila siku.
 
Mkuu wangu serikali inatuumiza wote hilo halina Ubishi lakini unapotaka kupambana na serikali unapeleka mapambano kwa serikali sio raia ambao hawana hatia kabisa, sasa kuumizwa kule kwa serikali kunachanganya na kuumizwa na madaktari huoni kama hapo wanafanya yale ya 9/11, only fools can support that even though kweli iliwapagaisha Marekani..Mkuu Daktari ni mwajiriwa utapinga tu kufanya kazi ikiwa inahatarisha hata maisha yako lakini kinyume cha pale acha kazi una uhuru wa kufanya hivyo sio kumlazimisha mwajiri wako ktk vitu ambavyo huna haki navyo kama mwajiriwa..

Sasa sawa wamegoma ili wafanikishe madai yao ndio warudi kazini haya nambie hayomadai wewe unafikiri yatachukua muda gani kama serikali itataka kuyatimiza maana yapo ya zaidi ya mwaka kutimizwa hata ktk hali nzuri ya kiuchumi.. Na tunaporudi nyuma na kutazama na kuilaumu serikali tunakuta zipo Taasisi husika wengine hapa tukisema mnatuita wadini... Je tunailaumu serikali kwa makosa gani ikiwa serikali imeunda chombo cha kushughulikia maswala haya lakini hatutaki kiguswe?.. Hao mawaziri mnawaonea bure maana nje ya sheria imeshandikwa na wao mbali na bajeti wanaoandika hupelekewa maagizo ya matakwa ya chombo kinachoshughulika na maswala haya.

Twende mbele na tuzirudishe nafsi zetu katika Uzalendo kwanza na kama mnataka kui punish serikali basi wahusika na maendeleo ya AFYA na ELIMU nchini ndio wawajibishwe sio kugoma na kuwaumiza wananchi kwa madai ambayo wao sii sababu ila waathirika kabla hata ya kufikishwa Hospitalini. Nimetembelea Hospital Bongo hata hizo za binafsi ni hatari tupu yaani huwezi hata kufananisha na Health care ya mtaani kwangu.

Leo hii hata dawa za kumwagilia kuua mbu ni feki, nenda hata Shoppers au Mlimani utakuta diaper na kinga za wanawake picha na muundo sawa kabisa na Original za Ulaya, lakini ni FEKI watoto na kina mama wanatoka hadi mapele ya chini..Kila mtu tapeli na nasema tena madaktari wanachotaka ni kujionyesha wao muhimu kuliko kila kitu kwa madai ya posho tu, hayo mengine yameongezwa kuchamsha baraza, ebu JK akubali mengine yote aache posho tuone kama watarudi kazini..

Sasa nambieni wakuu zangu hata Supermarket zetu zinauza madawa feki, vipimo vya malaria na HIV feki na wamepewa mamlaka wataalam wetu kukagua na hata kupitisha vifaa hivi. Toka mbegu hadi chakula tunachokula Bongo siku hizi ni maradhi matupu tunabambikiwa..Wanawake wajawazito kubebwa na Bajaj haya yote ni matusi makubwa kwa wananchi na kama kweli kuna watu waliotakiwa kuandamana basi ni sisi wananchi pamoja na hao wagonjwa wa Muhimbili kisha hao madaktari wangejitetea kwamba sii makosa yao..

lakini kwa njia hii inaonyesha wazi kabisa kwamba wanachokitaka haswa ni posho na hasa baada ya Pinda kupitisha posho za Wabunge.. Hawa Madaktari na sisi wananchi kwa ujumla wetu tulitakiwa kuungana na kufanya maandamanoi kupinga hali halisi iliyopo na JK angeweza kutazama maswala yote kwa picha kubwa zaidi, lakini haya ya Ushindani one on one yanampa JK kichwa na kufikiria ni madaktari tu ndio wenye matatizo lakini wananchi wanamkubali..Lakini tufanyeje ikiwa wananchi wenyewe hatukuungana kila mtu kabeba msalaba wake?.

Binafsi siwezi kabisa kuwatetea madaktari ktk hili, madai yao yanaweza kuwa mazuri lakini maamuzi ya kugoma kuwatibu wananchi hapo wamevuka mpaka. Na nasema tena ni sawa na mwanajeshi alokataa kwenda vitani maana daktari akiwa kazini ni sawa kabisa na mwanajeshi unapoponyesha roho moja ni fahari kubwa na aibu ktk sekta hiyo kwa kila mtu anayekufa..Hivyo kutumia njia za makusudi kabisa watu wafe ili kuikomoa serikali sidhani ni maamuzi ya busara na kama ningekuwa mimi JK ningefukuza watu kazi, na sababu kubwa ni kitendo cha kukosa Uzalendo maana unapogoma ina maana hutaki mazungumzo sasa mbona wanakutana na Pinda, kumbe uwezekano wa mazungumzo upo..
 
Mkuu Mkandara, ni kwa maslahi ya nani kwa madaktari kurudi na kufanya kazi katika mazingira yaleyale yaliyowafikisha hapa?
 
kwa nini? fukuza tu, na tunaweka unique policy ya afya. madaktari mtaripoti kwa manesi, na manesi wataandika dawa. operation zenyewe zinawashinda, vichwa na miguu-wapi na wapi?
 
Mkuu Mkandara unasema kweli sawa, ila hata mi nltamani mgomo huu ushikwe na umma kwa namna flani hvi...!
Lakini kama tunakubaliana kuwa tuna umma "uliolala" tena usingizi mkali, hyo maana yake nini? Madaktari walitakiwa wafanye nini? Ndio ishu ni posho ie pesa, hyo sio aibu wala... Kudai pesa kwenye mfumo wa maisha ya pesa sio aibu!
Namna ya uchumi wa dunia kuwa "kila kitu ni pesa"
acha kila mtu adai pesa.
Kuna madhara hayakwepeki, ni kweli tutakufa sana na kuteseka sana kwa mgomo ila ukiangalia tena ndio maisha yetu yamekuwa hvyo siku zote,
mwaka juzi nimempoteza Baba yangu mzazi pale Muhimbili, wakati tunasubiri taratibu tu za kuruhusu kwenda nje ya nchi kwa matibabu zaidi... Hivyo ni tunakufa hata bila mgomo, mfumo tu unatosha kutuua!
 
Mkandara;3220301]Mkuu wangu serikali inatuumiza wote hilo halina Ubishi lakini unapotaka kupambana na serikali unapeleka mapambano kwa serikali sio raia ambao hawana hatia kabisa, sasa kuumizwa kule kwa serikali kunachanganya na kuumizwa na madaktari huoni kama hapo wanafanya yale ya 9/11, only fools can support that even though kweli iliwapagaisha Marekani..Mkuu Daktari ni mwajiriwa utapinga tu kufanya kazi ikiwa inahatarisha hata maisha yako lakini kinyume cha pale acha kazi una uhuru wa kufanya hivyo sio kumlazimisha mwajiri wako ktk vitu ambavyo huna haki navyo kama mwajiriwa
Mkuu Mkandara, nina uhakika kuwa unafahamu vema chimbuko la vyama vya wafanyakazi. Hata katika nchi zenye ubepari ambapo kazi humilikiwa na mtu bado kuna vyama hivyo na vimepewa haki ya kisheria kugoma na mwajiri wao kuwasikiliza. Wachezaji wa NBA waligoma wakidai masilahi zaidi kutokana na mapato ya mabosi wao.
Kilichofanyika ni majadiliano kwa njia za kisheria ili kulinda haki za pande zote.

Nashukuru umetambua kuwa katika mazingira hatarishi wanapaswa kugoma, na ni ukweli kuwa mazingira wanayofanyia kazi ni hatarishi.
Fikria operesheni ya kumuokoa mzazi kwa kutumia taa ya fanusi! fikiria daktari anaacha mgonjwa na kukimbia kununu kifaa cha sh 1000/= duka la dawa baridi. Kwamba mmiliki wa kaduka hako ana uwezo kuliko hospitali ya serikali ya Temeke.

Nikukumbushe kuwa serikali hiyo hiyo imekiri kuwa kuna madaktari wengi sana wamekimbilia nchi za nje, sasa unapo encourage hao wazalendo wachache watimke unakaribisha madaktari wa Nigeria na Cuba ambao watalipwa dollar 8000/= kwa mwezi.

Kama hali ikiwa ngumu mtu anapaswa kuacha kazi, mbona wabunge wenye donge nono na marupu rupu yenye kafara na karaha hatuwaambii hayo badala yake waziri mkuu ana saini 200,000/= kwa wao kukaa kwenye kiti cha kazini.
Mkuu hawa kama wanaona hawawezi ubunge wa mshahara wa kawaida si waache kazi kama tunavyowashauri madaktari.
Leo hii hata dawa za kumwagilia kuua mbu ni feki, nenda hata Shoppers au Mlimani utakuta diaper na kinga za wanawake picha na muundo sawa kabisa na Original za Ulaya, lakini ni FEKI watoto na kina mama wanatoka hadi mapele ya chini..Kila mtu tapeli na nasema tena madaktari wanachotaka ni kujionyesha wao muhimu kuliko kila kitu kwa madai ya posho tu, hayo mengine yameongezwa kuchamsha baraza, ebu JK akubali mengine yote aache posho tuone kama watarudi kazini
Mkandara, kwani wakidai posho kuna kosa gani? Kama mtu anapokea mshahara wa sh Milioni 12 kwa mwezi na bado anadai aongezewe posho ya 200,000 kwa kuhudhuria kazini kwake,iweje tuone kioja mtu wa sh 600,000 akidai posho yake halali na makazi ili atoe huduma
Sasa nambieni wakuu zangu hata Supermarket zetu zinauza madawa feki, vipimo vya malaria na HIV feki na wamepewa mamlaka wataalam wetu kukagua na hata kupitisha vifaa hivi. Toka mbegu hadi chakula tunachokula Bongo siku hizi ni maradhi matupu tunabambikiwa..Wanawake wajawazito kubebwa na Bajaj haya yote ni matusi makubwa kwa wananchi na kama kweli kuna watu waliotakiwa kuandamana basi ni sisi wananchi pamoja na hao wagonjwa wa Muhimbili kisha hao madaktari wangejitetea kwamba sii makosa yao
Nakubaliana na wewe kabisa, sisi tulitakiwa tuandamane ili pia wapewe haki na stahiki zao ikiwa ni pamoja na makazi, halafu tuwageukie na kuwauliza kwanini huduma ni mbaya, kwanini wanaruhusu utapeli wa dawa za mbu, dawa za wagonjwa n.k. Tunapowataka watimize wajibu wao bila sisi kuwatimizia wetu ni kumkamua ng'ombe mwenye njaa tukitegemea maziwa.

Hili la wanawake kubebwa kwa Bajaji sio madaktari walioshauri, ni serikali tuliyoichagua kwa kura. Tena kuna wakati madaktari walilamika kuhusu hilo lakini hao hao wanaokataa kutoa posho hawakuwasikiliza wakaalika kamera na sisi wananchi hutukuhoji wataalam wanasemaje
lakini kwa njia hii inaonyesha wazi kabisa kwamba wanachokitaka haswa ni posho na hasa baada ya Pinda kupitisha posho za Wabunge.. Hawa Madaktari na sisi wananchi kwa ujumla wetu tulitakiwa kuungana na kufanya maandamano kupinga hali halisi iliyopo na JK angeweza kutazama maswala yote kwa picha kubwa zaidi, lakini haya ya Ushindani one on one yanampa JK kichwa na kufikiria ni madaktari tu ndio wenye matatizo lakini wananchi wanamkubali..Lakini tufanyeje ikiwa wananchi wenyewe hatukuungana kila mtu kabeba msalaba wake
Nakubaliana pia inafika wakati kila mtu abebe msalaba wake. Nasema hivyo kwasababu sisi wananchi wa Tanzania ni wepesi wa kuangalia tunmeangukiwa wapi na si tumejikwaa wapi. Leo tunalalama tumeangukia muhimbili, tumesahau huko nyuma tumejikwaa sana.
Wananchi wamekaa kimya mtu mmoja alipwe bilioni 100 za utapeli.

Wananchi wamekaa kimya umeme ukipandishwa bei hata kama tulijua mipango iliyotajwa bungeni ya trilioni moja ililenga kutumaliza.
Wananchi wamekaa kimya makontena yanapita bila kodi na wao wanakamuliwa kodi katika laki 2 wanazopata.

Wabunge wamejiunga na kupata posho zao tena bila kujali upinzani.
Mkapa na Sumaye walishapeleka mswada wa kulinda posho zao leo akina Lowassa wanakula 80% ya mshahara wa PM kwa kuliingiza taifa katika hasara ya kihistoria.

Sasa madaktari ambao kila siku wanabeba roho zetu wakigombea masilahi yao kidogo sana kuna shida gani? Hivi huu si ndio muda muafaka wa sisi kuungana nao ili kesho tuwaambie waungane nasi kudai vitanda hospitalini.

Madai yao yapo siku nyingi lakini yaliyoshughulikiwa ni yale ya wateule wabunge. Sidhani kama ni haki Daktari afanye kazi miezi 3 bila mshahara tukijua ana mahitaji sawa na mbunge, katibu mkuu au mkulima mwingine. Kama serikali ingetaka kuwasaidia wananchi,ingeanza mapema kuonyesha nia ya kutatua tatizo lao. Hata pale walipotoa nafasi hiyo Blandina aliwahamisha vituo vya kazi kama sehemu ya 'ushugulikia'madai yao.

Labda Mkuu Mkandara utufahamishe, silaha gani wangeitumia ili kukabiliana na jeuri ya akina Blandina na Mtasiwa kama si JK ili wapate ufumbuzi wa tatizo lao.
 
Politics.
Hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo wanarefer wagonjwa ambao wana matatizo ambayo yangeweza kutibiwa mwananyamala, wanawaleta Muhimbili.
Ajali zinatokea huko porini wanawaleta askari waliumia MOI kufanyiwa opereshen halaf wanarudishwa Lugalo Hosp kufunga vidonda.
Ni Jeshi gani unaloliongelea Tanzania?
Acha siasa.

Jeshi lina graduate wachache sana katika fani ya udaktari. Wao wana clinical officers na AMO kwa uchache.
 
Kwa kiburi cha watu wachache tumeingia katika janga ambalo litaendelea kuwa kubwa zaidi kwa kiburi hicho hicho cha wachache hao. Madaktari mna madai ya msingi: solidarity forever!
 
Pasco hizi directives unazipata toka kwa nani? pm, waziri husika au naibu waziri au katibu mkuu au wote kwa pamoja?
Mkuu August, soma mwanzo wa thread hii ni opinionated questions!.

Maswali nimeyaunda mwenyewe na kusuggest posible answers. Jana nilisema watalazimishwa kurejea kazini na watakao kataa will face the music. Nilifikiri Iron Lady ataitia kiburi serikali isiwafate madaktari mahali walipo, jana serikali imewapigia magoti kupitia mawaziri wake 3!. Madaktari wakagoma wanamtaja Pinda!. Sasa leo Pinda watampata na atawaambia yale yale ya jana "madai yenu ni genuine, serikali imeyapokea na kwa vile yanahusu sekta mtambuka, uwezo wa nchi kulipa/ hazina ya taifa/ wizara ya fedha/wizara ya Afya/ Wizara ya Utumishi etc etc, its obvious it will take time". Mtoto wa Mkulima atatoa chozi kidogo kuwalilia wagonjwa waliokufa jana na wale wanaokufa leo, atakuwa pia ameshika magazeti kuonyesha ripoti za mateso Watanzania walala hoi wanavyoteseka, then atamalizia " Chonde Chonde ndugu zangu madakitari, nawaombeni sana muwaonee huruma Watanzania wenzetu wanaoteseka na msiba huu!. Nawaombeni sana mrejee kazini wakati serikali ikishughulikia madai yenu". Mimi na serikali yangu, tuko chini ya miguu yenu!".

Pia Mtoto wa Mkulima atawapa madakitari hao salaam zao kutoka Davos!.

Kama na leo wataendelea kugoma, yale masaa 48 yanamalizika Jumatatu asubuhi!. Sikilizieni kitakachofuatia.
 
  • Thanks
Reactions: ral
This saga has all elements of poor administration at the ministerial level. You can't communicate with professions like they are your children. The principal secretary and chief medical officer have created this situation which is causing suffering to common citizens. The way the minister and deputy minister have acted have revealed the weakness in political appointments in this country. It is a shame for the deputy who happens to be a doctor of medicine
 
Jeshi lina graduate wachache sana katika fani ya udaktari. Wao wana clinical officers na AMO kwa uchache.
Ozzie kwa level ya Tanzania mpaka nesi ndio daktari mkuu wa kijiji itakuwa hao AMO?. Ma RMO ndio wamekuwa wakiendesha hospitali zetu miaka nenda rudi leo ndio washindwe nini?.
Subirieni baada ya mkutano wa Pinda leo muone kitakachotokea Jumatatu asubuhi!.
 
Naombea mpango huo wakuwafukuza serikali iutekeleze iliwatu sasa wakae barabarani kuiondoa serikali ya ccm baada ya watu wengi kufa na hapa tunakaza hakuna kurudi nyuma wakuu.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Its just a matter of time subiri tamko hilo within the next 48hrs!, unless madaktari wakomaji wamekubali kuitikia mwito wa serikali kuifuata ilipo, wakishikilia msimamo wao, kuwa lazima serikali ndio iwafuate walipo, serikali haitawafuata and they will be fired!.

Na baada ya tamko la kuwafukuza kazi hiyo next Monday, Tuesday mtaona Tangazo la ajira za madaktari equal na number ya waliotimuliwa jana yake, na tangazo hilo litasema, madaktari waliotimuliwa ruksa kuomba kazi upya, na belive me, wataomba, kwa masharti yale yale waliyoyagomea!, na this time masharti yao ya ajira mpya yatatamka 'expresisly' not 'impliedly' ni marufuku kugoma, na ukigoma tuu jihesabu you have lost your job!.

Siyo raisin kiivoooooooooo, unakumbuka mow aka 1994, walifukuza kikatokea nini? Wooooooote walirudishwa bila mashirti hebu tuwe tunaangalia historia kuona mambo yalishughulikiwaje, "UONGOZI NI UWAJIBIKAJI KWA RAIA NA SI UBABE" J .K NYERERE RIP
 
Politics.
Hospitali kuu ya Jeshi, Lugalo wanarefer wagonjwa ambao wana matatizo ambayo yangeweza kutibiwa mwananyamala, wanawaleta Muhimbili.
Ajali zinatokea huko porini wanawaleta askari waliumia MOI kufanyiwa opereshen halaf wanarudishwa Lugalo Hosp kufunga vidonda.
Ni Jeshi gani unaloliongelea Tanzania?
Acha siasa.

Nimeandika facts siyo siasa. Ina maana Brigadier general Dr. Balele hakuwahi kuongoza kikosi cha wanajeshii kwenda Muhimbili wakati madaktari wamegoma? Siasa niliyoiandika iko wapi? Soma post kwa makini usikimbie kuandika kabla vidole havijaagana na ubongo! Tofautisha fact na siasa. Sijasema jeshi liende nasema lilishawahi kwenda.
 
Mkuu wangu serikali inatuumiza wote hilo halina Ubishi lakini unapotaka kupambana na serikali unapeleka mapambano kwa serikali sio raia ambao hawana hatia kabisa, sasa kuumizwa kule kwa serikali kunachanganya na kuumizwa na madaktari huoni kama hapo wanafanya yale ya 9/11, only fools can support that even though kweli iliwapagaisha Marekani..Mkuu Daktari ni mwajiriwa utapinga tu kufanya kazi ikiwa inahatarisha hata maisha yako lakini kinyume cha pale acha kazi una uhuru wa kufanya hivyo sio kumlazimisha mwajiri wako ktk vitu ambavyo huna haki navyo kama mwajiriwa..

Sasa sawa wamegoma ili wafanikishe madai yao ndio warudi kazini haya nambie hayomadai wewe unafikiri yatachukua muda gani kama serikali itataka kuyatimiza maana yapo ya zaidi ya mwaka kutimizwa hata ktk hali nzuri ya kiuchumi.. Na tunaporudi nyuma na kutazama na kuilaumu serikali tunakuta zipo Taasisi husika wengine hapa tukisema mnatuita wadini... Je tunailaumu serikali kwa makosa gani ikiwa serikali imeunda chombo cha kushughulikia maswala haya lakini hatutaki kiguswe?.. Hao mawaziri mnawaonea bure maana nje ya sheria imeshandikwa na wao mbali na bajeti wanaoandika hupelekewa maagizo ya matakwa ya chombo kinachoshughulika na maswala haya.

Twende mbele na tuzirudishe nafsi zetu katika Uzalendo kwanza na kama mnataka kui punish serikali basi wahusika na maendeleo ya AFYA na ELIMU nchini ndio wawajibishwe sio kugoma na kuwaumiza wananchi kwa madai ambayo wao sii sababu ila waathirika kabla hata ya kufikishwa Hospitalini. Nimetembelea Hospital Bongo hata hizo za binafsi ni hatari tupu yaani huwezi hata kufananisha na Health care ya mtaani kwangu.

Leo hii hata dawa za kumwagilia kuua mbu ni feki, nenda hata Shoppers au Mlimani utakuta diaper na kinga za wanawake picha na muundo sawa kabisa na Original za Ulaya, lakini ni FEKI watoto na kina mama wanatoka hadi mapele ya chini..Kila mtu tapeli na nasema tena madaktari wanachotaka ni kujionyesha wao muhimu kuliko kila kitu kwa madai ya posho tu, hayo mengine yameongezwa kuchamsha baraza, ebu JK akubali mengine yote aache posho tuone kama watarudi kazini..

Sasa nambieni wakuu zangu hata Supermarket zetu zinauza madawa feki, vipimo vya malaria na HIV feki na wamepewa mamlaka wataalam wetu kukagua na hata kupitisha vifaa hivi. Toka mbegu hadi chakula tunachokula Bongo siku hizi ni maradhi matupu tunabambikiwa..Wanawake wajawazito kubebwa na Bajaj haya yote ni matusi makubwa kwa wananchi na kama kweli kuna watu waliotakiwa kuandamana basi ni sisi wananchi pamoja na hao wagonjwa wa Muhimbili kisha hao madaktari wangejitetea kwamba sii makosa yao..

lakini kwa njia hii inaonyesha wazi kabisa kwamba wanachokitaka haswa ni posho na hasa baada ya Pinda kupitisha posho za Wabunge.. Hawa Madaktari na sisi wananchi kwa ujumla wetu tulitakiwa kuungana na kufanya maandamanoi kupinga hali halisi iliyopo na JK angeweza kutazama maswala yote kwa picha kubwa zaidi, lakini haya ya Ushindani one on one yanampa JK kichwa na kufikiria ni madaktari tu ndio wenye matatizo lakini wananchi wanamkubali..Lakini tufanyeje ikiwa wananchi wenyewe hatukuungana kila mtu kabeba msalaba wake?.

Binafsi siwezi kabisa kuwatetea madaktari ktk hili, madai yao yanaweza kuwa mazuri lakini maamuzi ya kugoma kuwatibu wananchi hapo wamevuka mpaka. Na nasema tena ni sawa na mwanajeshi alokataa kwenda vitani maana daktari akiwa kazini ni sawa kabisa na mwanajeshi unapoponyesha roho moja ni fahari kubwa na aibu ktk sekta hiyo kwa kila mtu anayekufa..Hivyo kutumia njia za makusudi kabisa watu wafe ili kuikomoa serikali sidhani ni maamuzi ya busara na kama ningekuwa mimi JK ningefukuza watu kazi, na sababu kubwa ni kitendo cha kukosa Uzalendo maana unapogoma ina maana hutaki mazungumzo sasa mbona wanakutana na Pinda, kumbe uwezekano wa mazungumzo upo..
Mkuu Mkandara, mimi naunga mkono madai ya madakitari ni genuine ila mgomo sio halali na hilo la kutunisha misuli kupitiliza linaninatatiza kidogo!. Lets hope hiyo deadlock itaisha leo!.
 
Bado tunawasubiri na maaskari waunge azimio!!! Matatizo si kwa madaktari tu!! nanyi askari amkeni!! Tokeni usingizini!! Someni kwa haraka waraka huu KISHA muwaunge mkono madaktari!!!

Waraka maalum kwa Askari wote

MAKALA hii ilikuwa itoke Jumatano ya wiki iliyopita lakini kwa sababu za kiufundi ikashindikana. Imekuwa ni bahati nzuri kwamba inapotoka leo, ijibu swali la askari polisi dereva wa gari la maji ya kuwasha.

Askari huyo alimweleza Mwalimu Mkuu wa watu jinsi roho inavyomuuma pale anapowamwagia Watanzania wenzake maji hayo ya kuwasha wakati wakidai haki yao. Askari uliyeuliza na wenzako wote someni makala hii kwa utulivu. Huu ni waraka maalumu kwa askari wote wa majeshi yote vikosi vyote Tanzania Bara na Visiwani.

Kwa lugha ya wazi zaidi nazungumza na askari wa Jeshi la Polisi Tanzania, Askari wa Jeshi la Kujenga Taifa, askari wa Kikosi Maalumu cha Kuzuia Magendo (KMKM), askari wa Jeshi la Magereza na wale wa Jeshi la Wananchi (JWTZ).
Kuwa mwanajeshi lolote kati ya hayo niliyoyataja si dhambi na si kweli kwamba kuwa mwanajeshi kunakuondolea uwezo wa kufikiri na badala yake ukawa unafikiriwa na watu wengine.

Wala haimaanishi kuwa askari kuwa kama robot ndio nidhamu bora kuliko zote duniani. La hasha! Mimi nilikataa utumwa huo!

Mwaka 1999 nilihitimu elimu ya cheti cha ufundi mchundo, yaani Full Technician Certificate (FTC) katika uhandisi wa Elektroniki na Mawasiliano ya Anga, yaani Electronics & Telecommunications Engineering kutoka Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam (DIT).

Nikiwa bado sijapata kazi ya maana, mwezi Aprili mwaka 2000 niliona tangazo la kazi ya Radio Technician katika Jeshi la Magereza. Nikatuma maombi na kuitwa kwenye usaili uliofanyika Chuo cha Maofisa wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es Salaam mwezi Juni 2000.

Wote tuliofaulu usaili tulipangiwa siku ya kuripoti Chuo cha Magereza Kiwira kule Tukuyu, Mbeya.

Kufika kule nilishuhudia mambo ya ajabu. Ingawa wao hufurahia na kusema eti wanakutoa uraiani na kuwa mwanajeshi lakini baadhi ya matendo yanayofanyika wakati wa mafunzo ya jeshi ni ya kuwapumbaza askari wetu ili baadaye wakiwa kazini, watawala wawatumie watakavyo.

Nilishindwa kuvumilia kaulimbiu ya wakufunzi wa jeshi pale walipoelekeza kwamba chochote kruta (askari mpya mafunzoni) unachoambiwa lazima uitikie “ndiyo afande”. Nilishindwa kuitikia kwa mfano pale mkufunzi mmoja mwenye cheo cha koplo alipotutamkia mfululizo wa sentensi zifuatazo:
Mkufunzi: Nyinyi makruta mbona wote hamkuja na majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Hamkuambiwa makao makuu ya jeshi kwamba lazima mje na majembe?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Kwa hiyo kwa kuwa hamkuambiwa na nyinyi hamkuyabeba?
Makruta: Ndiyo afande!
Mkufunzi: Wote ni wapumbavu pamoja na mama zenu waliowazaa.
Makruta: Ndiyo afande!

Ni hayo pamoja na mambo mengine ya kulazimishwa kwenda kwenye kile kinachoitwa disko, ambapo pamoja na uchovu wa kutwa nzima wa kazi ngumu na nyingi bado ni lazima ukae hapo mpaka saa 4 usiku tena ukinyooshewa kidole tu na mwenzako lazima usimame na kuimbisha wimbo tena kwa tabasamu, wimbo mmoja wapo ukisema “Magereza ninavyokupenda nitakunywa sumu juu yako”, ndiyo yaliyonifanya nikakataa kazi ya jeshi baada ya wiki moja tu ya mafunzo.

Siku niliyokataa jeshi ilikuwa ni Jumatano asubuhi ambapo sikwenda mchakamchaka na wakati wenzako wanatawanyika kufanya usafi wa nje maeneo mbalimbali, mimi nilibeba begi langu na kuanza kuondoka chuoni majira ya saa moja na nusu hivi asubuhi.

Nilikamatwa na mkufunzi mmoja wa jeshi na kupelekwa pamoja na begi langu kwa Ofisa Mafunzo wa chuo. Aliponiuliza sababu nilimtajia mbili, kwanza kwamba sifurahii mambo ya jeshi na kubwa zaidi kwamba mimi ni Msabato na nimeambiwa na wenzangu kwamba hapa hakuna kwenda kusali, siku zote za juma ni kazi.

Kitu ambacho sitaweza maana Sabato takatifu lazima nipumzike! Bila kuuliza zaidi aliconclude kwa kuniambia kwamba, “Sijawahi kuona mtu anaacha kazi kwa ajili ya mambo ya dini.

”Ni dhahiri wewe ulikuja kutupeleleza na hivyo kazi yako imeisha sasa unataka kurudi. Tutakuweka rumande, tena ile ya polisi kwa wiki mbili wakati tunafanya upelelezi juu yako.”

Askari aliyenileta alianza kunivuta ili kunipeleka rumande lakini nilikataa huku nikiendelea kujieleza kwa ofisa mafunzo ili ajue kwamba sikuwa na mpango huo aliousema.

Baada ya kuelemewa na hoja zangu alinipeleka kwa makamu mkuu wa chuo ambaye yeye alitumia zaidi Biblia kunihubiri kwamba nakaidi amri ya mamlaka wakati hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu.

Jibu langu lilikuwa fupi na lenye msimamo mzito kwamba ikiwa mamlaka ya wanadamu inafika mahali inanena tofauti na Mungu, Mtume Petro ametuandikia kwamba katika hali ya namna hiyo, “Imetupasa kumtii Mungu kuliko mwanadamu”.

Na yeye alinishindwa akanipeleka kwa mkuu wa chuo na wao wote wakiwapo. Ushauri waliokuwa wakimpa mkuu wa chuo ni kwamba mimi niwekwe rumande kwanza ili wafanye upelelezi. Lakini sikuyumba katika msimamo wangu.

Nilimweleza mkuu wa chuo kwamba mimi ni raia na si mpelelezi. Nilizirudia rudia sababu zangu za kuacha jeshi tena kwa ujasiri mkubwa na kumhakikishia mkuu wa chuo kwamba akinipa hayo ninayoyataka niko tayari kubaki jeshini.
Hatimaye kauli ya mwisho ya mkuu wa chuo ilikuwa ni hii: “Jeshi ni wito. Tunaweza kumlazimisha huyu kijana kuwa mwanajeshi lakini baadaye ikatuletea madhara makubwa sana.” Akamalizia kwa kusema, “chukueni maelezo yake kwa maandishi kisha arudishe vifaa vya jeshi.”

Wakati naondoka nilimsikia ofisa mafunzo akitoa maelekezo kwa walio chini yake kwamba mwanafunzi mwingine wa jeshi akija kuripoti na kwenye daftari akajaza kwamba ni Msabato, msimsajili kwanza mpaka aje kwangu! Sijui kama Wasabato wameendelea kupokewa kwenye hicho chuo cha magereza lakini ninachotaka askari wote wa majeshi yetu yote na vikosi vyote, ni kwamba askari unaweza kusimama kwa miguu yako na kufikiri kwa akili yako mwenyewe!
Ndugu zangu askari, nchi imefika mahali ambapo Waingereza hupenda kupaita ‘critical point’. Ni mahali ambapo wananchi wako tayari kwa mabadiliko na watawala wako tayari kwa mapambano ili kubaki madarakani.

Katika point hii askari wetu wanakuwa na nafasi kubwa ya aidha kuwezesha mabadiliko hayo kutokea kwa wakati wanaoutaka wananchi, tena kwa amani ama kuyachelewesha (si kuyazuia) na kusababisha yatokee baadaye kidogo kuliko wananchi walivyotaka, tena baada ya kumwaga damu nyingi ya Watanzania wasio na hatia!

Napenda kurudia kwamba hakuna jeshi lolote duniani hata kama tungekusanya majeshi yote ya dunia hii na kuyaleta Tanzania hawataweza kuizuia nguvu ya umma pale inapokuwa imeamua kufanya mabadiliko.

Napenda tena kurudia kwamba si lazima askari mfanye kile ambacho wakubwa wenu wanataka na kuwaamuru kufanya. Tunaweza kusimama imara na kutetea haki za Watanzania tukiwamo na sisi askari. Niliwahi kugoma kutii amri ya kukamatwa na kuwekwa rumande.
Lakini pia mifano ni mingi na nisingependa kuchukua mifano kutoka nchi za Ulaya kama Uingereza ambako tulishuhudia wananchi wakiandamana mitaani na askari wao hawakuwahi hata kumpiga kofi tu mwandamanaji hata mmoja.
Walipohojiwa na vyombo vya habari walisema dhahiri kwamba waandamanaji ni raia halali wenye haki ya kufanya kile wanachokifanya kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi yao. Katiba ya Tanzania na sheria za nchi hii zinatoa haki kama zile za Uingereza. Tofauti ni utekelezaji wa matakwa hayo ya kikatiba na kisheria. Watawala wa Uingereza wako tayari hata kung’oka madarakani ili kutekeleza matakwa ya nguvu ya umma.

Lakini wale wa Tanzania wako tayari kung’oa uhai wa raia wengi ili mradi kuzuia nguvu ya umma inayodai haki na wananya hivyo kwa sababu ya hofu ya kung’oka madarakani, jambo ambalo hawataki kabisa kulisikia. Na ndugu zangu askari napenda kuwaambia kwamba yote yanafanywa na watawala wetu kwa kuwategemea nyinyi.

Wanaminya haki zenu nyinyi wenyewe, haki za wazazi wenu, dada na ndugu zenu, marafiki zenu, jamaa zenu na majirani zenu. Chukulia mfano rafiki zangu Mtaki na Edwin. Tumesoma wote shule ya msingi pale Magu.

Nilichaguliwa kujiunga na Mazengo Sekondari, shule kubwa na ya muda mrefu ambayo sasa imegeuzwa kuwa chuo kikuu bila mabadiliko ya majengo.

Shule iliyokuwa na maabara nne kwa maana ya maabara ya baiolojia, kemia, fizikia na jiografia. Ilikuwa ni sekondari ya ufundi na hakuna karakana ambayo haikuwapo.

Shule iliyokuwa na walimu wa kutosha, vyumba vya kutosha vya madarasa na vya kulala mabwenini.
Katika bweni la Ujamaa kwa mfano, nilikokuwa naishi mimi, kuna vyumba kadhaa havikuwa na watu. Darasa la Form IVA ambalo nilikuwamo lilikuwa na wanafunzi 21 tu darasani.

Na mazingira mengine mengi ambayo sitaweza kuyataja hapa ambayo yanafanya wanafunzi wa leo wa Chuo Kikuu cha Mt. John wajiulize kama kweli ile ilikuwa ni shule ambayo haina maktaba wala vitabu vya kutosha, na mengineyo mengi mnayoyafahmu.

Nikafaulu kwa kiwango cha daraja la juu lililoniwezesha kuendelea mpaka chuo kikuu na kupata kazi nzuri kwenye Umoja wa Mataiifa.

Rafiki zangu nakumbuka mlivyoamua kujiunga na Jeshi la Polisi si kwa sababu mlipenda kazi hiyo ama kwamba mlikuwa na wito wa kuwa polisi kama mnavyodanganywa kwamba jeshi ni wito.

Nakumbuka mlijiunga huku mkilalamika kwamba mnalazimika kujiunga huko kwa sababu kiwango chenu cha ufaulu hakiwapi fursa ya kazi bora zaidi ya hiyo. Lakini mimi nawafahamu vizuri. Najua uwezo wenu wa darasani. Mliathiriwa na mazingira ya hovyo ya shule mlizosoma.

Rafiki zangu nyinyi wote leo ni wakuu wa vituo vikuu vya polisi vya wilaya katika wilaya za Mbozi na Igunga.
Leo hii mimi nimeacha kazi ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kushiriki vema katika mapambano ya kutafuta ukombozi wa taifa hili.

Wadogo zenu na wadogo zangu mnawajua wako katika juhudi za kutafuta maisha lakini ni magumu. Wengine walikosa kabisa nafasi ya kujiunga hata na hiyo Magu Day.

Wakaishia Bulima na Kinango, ambako hali ilikuwa mbaya zaidi. Wakafeli kabisa na leo wanahangaika hapa na pale lakini watawala wanawawekea mazingira magumu mno ya kuendesha maisha.

Na sasa chukulia nao wametambua hali yao duni inasababishwa na watawala walafi na walaghai. Wamejaribu kutumia njia za kidiplomasia kudai haki zao wanakutana na watu wanaitwa wakuu wa wilaya na mikoa.

Wanaamua kuandamana, mnashiriki kuamrisha askari walio chini yenu kuwapiga na kuwaweka rumande na hatimaye kuwafungulia kesi za kubumba!

Askari wetu igeni mfano wa askari wa Misri! Pale wananchi walipoamua kuandamana kukomesha utawala wa kidhalimu wa miaka 30 chini ya Hosni Mubarak, askari waliwalinda badala ya kuwapiga.

Walikataa kwa sababu hata wao walikuwa wakiumizwa na Mubarak lakini zaidi ya hayo, waliokuwa wakiandamana walikuwa ni dada zao na ndugu zao na marafiki zao.

Hivi sasa nchi iko njia panda. Ugumu wa maisha umeongezeka mara nne na zaidi. Watawala hawalioni hilo wala hawajishughulishi kurekebisha hali ya mambo hususan hali ya uchumi.

Wako busy na kujiandaa kwa uchaguzi wa 2015. Mawaziri wako busy na kampeni za kuteuliwa kuwa wagombea wa urais kupitia chama tawala hapo 2015 na rais naye yuko busy kuandaa mtu wake ambaye anadhani akimrithisha jumba jeupe la pale Magogoni atasema mwacheni Ndugu Kikwete apumzike kwa amani.

Taifa limeamua kuandika katiba mpya, rais na serikali yake na chama chake wameamua kuuteka mchakato ingawa haikuwemo kwenye ilani yao ya uchaguzi ili tu waturudishie katiba ya mwaka 1977 na kuipa jina juu ya jalada KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA YA MWAKA 2014.

Natambua juhudi zinazoendelea hasa zikiongozwa na CHADEMA kujaribu kumkumbusha rais kwamba katiba iko juu yake na katiba ni mali ya wananchi na yeye anaajiriwa kwa katiba hiyo na si yeye kujiandalia katiba ili atawale kwa ulaini.

Lakini juhudi za kidiplomasia zikishindikana hapo ndipo itabidi haki ya watu idaiwe kwa maandamano na hapo askari wote tuungane na kuwa kama Misri, kwa kuwa Katiba mpya ni kwa masilahi yenu pia! Jaribuni kutafakari!
 
Jibu langu la haraka ni kuwa serikali haiwezi kufanya hivyo, haiwezi kuombea iweze kufanya hivyo na ikidhania kuwa inaweza kufanya hivyo haitoweza kufanya hivyo kwa sababu ikifanya hivyo itakuwa imepoteza uhalali wa kuwa serikali! Unless wafukuze madaktari wote, wauguzi wote! na wakiweza wagunge na mahospitali yote!

Ila kwa vile naamaini naweza kuwa nimekosea naombea serikali ifanye hivyo mapema zaidi kutangaza kuwa madaktari wote waliogoma wamefukuzwa kazi!!!

Banafsi naona serikali ifanye hilo jaribio ili walau watu waamini kwamba kweli si legelege!!

Hata hivyo nimekerwa sana na hii thread ya Pasco kwani ukiiangalia kwa jicho la mbali, ni kama vile ametumwa kutoa vitisho kwa madakatari. Hawa watu wanadai vitu ambavyo ni very genuine ila serilaki inawapuuza. Sina hata jina linalofaa kuipa hii serikali yetu ya ajabu sana!!
 
Back
Top Bottom