Ishaka
Member
- Nov 1, 2011
- 74
- 12
Mwalimu Nyerere wakati akihutubia mkutano wa wafanya kazi siku ya mei mosi kule Mbeya, aliwambia unganeni katika kudai haki zenu kwani hakuna mtakachopoteza bali minyororo yenu, sawasawa na walivyofanya madaktari wetu katika baadhi ya hospitali hapa nchini. Na kawaida migomo duniani kote huwa ni hatua ya mwisho ya mfanya kazi katika kudai haki yake anayodhulumiwa endapo njia nyingine zote zimegonga mwamba. wahenga walisema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Sasa watanzania tunashuhudia sakata ambalo wasomi wetu waliopewa dhamana ya roho za watu mahospitalini wamesitisha huduma na serikali iliyopewa dhamana ya maisha bora ya watanzania inakosa ufumbuzi wa tatizo hili kwa takribani zaidi ya wiki sasa! hii ni ajabu na aibu ya karne miaka 50 ya uhuru. wagonjwa wanakufa mahospitalini kwa kukosa huduma, hii si haki kabisa kwa serikali iliyokula kiapo cha kuwalinda na kuwatumikia watu wake. Hivi kweli tatizo la msingi liko wapi, nani anastahili asulubiwe katika hili; serikali au madaktari? Kwanini tunafika mahali hapo kama nchi, serikali na madaktari kutunishiana msuri maana mwisho wa siku watanzania wanyonge wasioweza kujighalamia matibabu katika hospitali za binafsi za madaktari hao wenyewe ndio tunaoumia. Kwanini serikali hilo hamlioni! Ni wazi kwamba kazi za madaktari na wauguzi ni ngumu zinazohitaji wito, moyo na kujituma lakini pia siyo kazi ya utawa ile. Hospitali si kanisa wala msikiti. Kama madai yao yanalenga kuboresha huduma wanazozitoa kwanini wasisikilizwe mapema katika hatua za mwanzo kwa ngazi ya uongozi wa chuo ikizidi sana basi wizara husika. Tatizo la nchi yetu ni umangi meza unaotokana zaidi na uteuzi wa viongozi ktk nafasi ambazo si za taaluma zao. Hii nayo ni issue! Lakini kama nchi, tumeutumia wapi msamaha wa madeni ya nchi hisani. Kila siku serikali inalia haina pesa, ni lini basi itakuwa nazo ili watanzania tupumue maana maisha tunayoishi sasa katika uongozi wa awamu ya nne ni kama tupo ICU. Awamu ya tatu pia wimbo ulikuwa uleule, serikali haina pesa! sawa.. lakini Radar ikanunuliwa kwa mabavu, na pia ndege ya rais mtarajiwa ikanunuliwa hata kama haikujulikana kama huyo rais ajaye angekuwa ni kutoka chama gani lakini ilinunuliwa pamoja na kwamba manunuzi hayo yalipingwa vikali sababu kulikuwapo na mahitaji mengine muhimu ya kitaifa likiwamo la huduma ya afya na elimu ambaya kwa kiongozi mwenye uzalendo, ndege ya rais isingekuwa kipaumbele cha taifa! Kumbuka pia katika lile sakata la serikali na chama cha...wafanyakazi nafikiri (serikali vs Mgaya - maarufu kama mbayuwayu), serikali ilipigilia msumari kabisa kwamba haikuwa na uwezo wa kulipa nyongeza ya mishahara hivyo kwamba anayekusudia kugoma ni bora aache kazi kabisa maana isingesaidia sababu pato la taifa halikutosha kufanya hivyo. Sasa ajabu ikawa kwamba wakati wa karibia na uchaguzi pesa zilipatikana nje ya lile pato la taifa na kuingizwa ki-aina katika akaunti za wafanyakazi! zilitoka wapi - fuatilia mwenyewe ni haki yako kujua sababu ni mlipa kodi. Sasa hii inatufundisha nini! Tukija ktk habari ya posho za wabunge, hiyo haina wabunge kugoma ili waipate maana hata mawaziri wote ni wabunge. Ila inapokuja kwa walimu, madaktari na wauguzi hapo ndipo huwa na tatizo miaka nenda rudi. Sasa hii ndio wanaita kula na kipofu kisha ukamgusa mkono. Watanzania tunashuhudia mengi lakini tunafumbia macho ili siku ipite wasiojua magumu tuliyobeba mioyoni waendelee kutuita nchi ya amani na utulivu. amani iko wapi wakati mioyo ya watanzania wengi imegubikwa na hofu ya maisha? mfumuko wa bei utafikiri upo kwenye promotion, bei za vyakula tishio, mafuta na umeme sasa ni anasa. EWURA hii kwa maoni yangu haitusaidii watanzania, kwanza ni mzigo kwetu sababu tunalazimika kumlipa sisi kwa kila manunuzi ya umeme kwa mwezi wakati mwajiri ni serikali. kwa maana nyingine ombi lolote la Tanesco la kutaka kupandisha garama za umeme kwake ewura ni ulaji hivyo akipelekewa atapunguza tu kiwango lakini kukataa ni ngumu. Nchi yetu sasa inahitaji viongozi makini na wabunifu wenye mtazamo wa mbali ili wanusuru kizazi hiki vinginevyo, nahofu tunaweza kuwa kama Rwanda kwanza ili baadae kupata viongozi wenye akili kama Rais Kagame. Huyu sasa ndiye Rais anayefunika marais wote barani Afrika kwa uongozi makini which is a determinant of his I.Q. Kiongozi mwadilifu na mzalendo anatakiwa aione Tanzania ya miaka 35 inayokuja jinsi inavyofanana ikiwa jangwa tupu bila uoto wake wa asili, bila misitu wala maji ya mito, wala wanyama na ndege tunaojivunia sababu mafuta na umeme kila vikipanda bei tunaegemea nishati ya kuni na mkaa maadamu vibali vinatolewa vya kuangamiza misitu, maisha yanaenda! mkaa wa mawe tunao tele ungeweza kuokoa mazingira kwa kuhamasisha biashara ya usambazaji wake katika miji yote nchini kwa msamaha wa kodi lakini kama yupo mwenye wazo hilo basi tayari ni mradi wa fisadi wa kuuza nje ya nchi. Tanzania itajengwa na wenye moyo safi. Madaktari wasikilizwe bila vitisho ili watutumikie sisi tusiotibiwa nje ya nchi. Lakini ombi langu kwa watanzania wote mtakaopata bahati ya kutoa maoni juu ya mswada wa katiba mpya ni muhimu kufuta fursa ya viongozi kutibiwa nje ya nchi. wote tutibiwe hapahapa na watoto wao wasome shule hizihizi ili twende sawa ndio itakuwa suluhisho la migomo. Jambo lingine muhimu, pingeni kwa garama yoyote sheria ya uraia wa nchi mbili. Haina faida yoyote kwa mtanzania wa kawaida bali nahisi inalenga kutoa mwanya wa mafisadi waliokwisha limbikiza nje utajiri wa nchi yetu kwa uficho, sasa waende kuhalalisha na hivyo tushindwe kuwabana kisheria pindi tutakapopata serikali makini. Kumbuka sio jambo rahisi kupatiwa uraia nchi yoyote ughaibuni bila wewe kuwa milionea au kuwa umeishi kule miaka mingi au lah, uwe mkimbizi wa kisiasa. Sasa nambie ni watanzania wangapi wa kawaida wenye uwezo huo kama sio deal la wachache wenye nazo.