Chipukizi
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 3,949
- 5,979
Ccm on the way to damascus
nimeisikiliza hotuba ya waziri mkuu kuhusu mgomo wa madaktari kama mtiririko wa matukio ni ule aliyoeleza waziri mkuu, waziri mkuu amemissimage mgogoro huo.
kasoro ya 1: yalikuwa ni makosa makubwa kukubali kuongea na madaktari zaidi ya mia nne (400) kwa sababu sio rahisi kupata suluhu ya mvutano katika mkusanyiko wa watu mia nne, yeye angekubali kuongea na wawakilishi.
kasoro ya 2: ni kutoa majibu ya mkato tuu kuwa madai ya nyongeza ya tshs3,000,000/= hayawezekani. Nakubaliana na madai ya nyongeza ya mshahara toka tshs.900,000/= hadi tshs.3,000,000/= ni unrealistic lakini angewauliza hao madaktari wametumia vigezo vipi kufikia ongezeko la madai ya zaidi ya 300%, inawezekana madaktari walijiropokea tu, angewauliza vigezo wangejiona hawana hoja. Pia angewaeleza financial implications za madai yao kitaifa , madaktari ni watu wenye vipaji vya akili ya juu na ni waelewa wangemwelewa. Majibu yaliyotelewa ya mkato hayakuwa ya kutafuta mwanzo wa mazungumzo ya kutafuta mwafaka. Hapa pia ni upungufu wa kutafuta mwafaka.
kasoro ya 3: madaktari pia walitaka walipwe risk allowance, hili lingeweza kutolewa ufumbuzi, wangeambiwa wa classify hizo risks kwa sababu siyo wote wana risk zinazofanana, kukubali hili lingewapa muda wa kutafakari na pia lingeweza kuwagawa na kupunguza makali, hapa sielewi ilipataje kigugumizi . Madaktari pia walitaka walipwe hardship allowance hili pia halina utata, mbona wafanyakazi wengine wanaopelekwa mfano kasulu, kibondo n.k wanalipwa kwanini isiwe madaktari? Hapo waziri mkuu amewapotosha wananchi.
kasoro 4: madaktari walitaka wapewe au wakopeshwe magari, hapa sioni utata. Serikali ingewakopesha kwa awamu na wengine wangelipwa transport allowance, kuna mashirika ya umma karibu yote hapa nchini yanatoa transport allowance kwa wafanyakazi wao kufuatana na vigezo mbali mbali.
kasoro ya 5: waziri mkuu ameshindwa kutoa majibu ya madai ya nyumba kwa madaktari. Naamini madaktari sio vichaa, siamini wangetegemea wapewe nyumba siku ya pili yake. Wangepewa housing allowance ambazo mashirika mengi ya umma hapa nchini wanatoa kwa wafanyakazi wao. Sidhani km ingekuwa mgogoro.
kasoro ya 6. Kwamba madaktari walitaka madai yao yatekelezwe mara moja. Hii tafsiri kwa waziri mkuu ni kama amri au dharau, madaktari walitaka makubaliano sio utekelezaji ufanyike siku hiyohiyo moja, au wajenge nyumba siku hiyo hiyo, hili lingeweza kuongelewa bila viongozi kujiona wamedhalilishwa.
kasoro ya 7: waziri mkuu kugusia maslahi binafsi ya madktari kama yalivyoainishwa kwenye madai yao bila hata kugusa mazingira ya kazi na vitendea kazi kama walivyoainisha kwenye madai yao, hapo waziri mkuu alikuwa na lengo la kuwagombanisha madaktari na wananchi.
mwisho kabisa ni kuwapiga marufuku wasikutane popote. Serikali imewafukuza kazi hii inatosha, wasikutane popote hii inatoka wapi na kwenye katiba ipi, huu ni ufashist.