Mgomo wa madaktari haukuongeza vifo: Dr. Nkya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa madaktari haukuongeza vifo: Dr. Nkya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tume ya Katiba, Apr 11, 2012.

 1. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Haya wadau tuisikilize serikali yetu, mwenye ushahidi wa vifo vilivyosababishwa na mgomo alete kwa sasa hii ndio kauli ya serikali yetu sikivu;

  SERIKALI imesema hakukuwa na ongezeko la vifo ambavyo vinahusishwa moja kwa moja na mgomo wa madaktari uliotokea hivi karibuni.

  Naibu Waziri wa Afya Ustawi wa Jamii, Dk. Lucy Nkya aliliambia Bunge jana mjini hapa wakati akijibu maswali ya Mbunge wa Gando, Khalifa Suleiman Khalifa (CUF), ambaye katika swali la nyongeza, alisema yupo kijana wake alifariki katika mgomo huo huku akihoji ni namna gani Serikali itawapoza walioathirika.

  Aidha, katika swali la msingi, Khalifa alitaka kufahamu ni namna gani mgomo uliathiri jamii ya Watanzania, watu wangapi walikufa kwa kukosa huduma na ni maeneo gani ya nchi yaliathirika zaidi.

  Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri alisema hospitali nyingi zilizokumbwa na mgomo huo zimetoa taarifa kuwa hakukuwa na ongezeko la vifo ambavyo vinahusishwa moja kwa moja na mgomo.

  Alitoa mfano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwamba kabla ya mgomo, Novemba mwaka huu, kulikuwa na vifo 457, Desemba vifo vilikuwa 537 wakati wa mgomo, Januari vifo vilikuwa 475 na wiki ya kwanza ya Februari vilikuwa 95.

  Alisema mgomo wa madaktari ulitokea katika hospitali 13 na maeneo yaliyoathirika zaidi ni Hospitali ya Taifa Muhimbili na Taasisi yake ya Mifupa (MOI) pamoja na hospitali za Manispaa za Dar es Salaam ambazo ni Amana, Temeke na Mwananyamala.

  Kwa mujibu wa Naibu Waziri, hospitali nyingine zilizokumbwa na mgomo ni Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Hospitali za Rufaa-Bugando, Mbeya na KCMC. Pia Hospitali za mikoa ya Tanga, Morogoro, Dodoma na Arusha.

  Akieleza ni namna gani mgomo uliathiri jamii, Naibu Waziri alisema uliwaathiri wananchi kisaikolojia kutokana na wagonjwa kukosa huduma kwenye maeneo ya hospitali walizotarajia.

  Athari nyingine ni ya kiuchumi ambapo baadhi ya wagonjwa ilibidi wapate huduma za malipo kupitia hospitali za watu binafsi. Aidha, alisema wapo watumishi wa afya waliokuwa wakiendelea na kazi wakati wa mgomo ambao walipata usumbufu mkubwa kutoka kwa waendesha mgomo.

  Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Pauline Gekul (Chadema) aliyetaka kufahamu ni namna gani Serikali imeshughulikia uhaba wa vifaa uliochangia mgomo huo, Dk. Nkya alisema chanzo kikubwa kilikuwa ni maslahi binafsi ya madaktari. Hata hivyo, alisema Serikali imejitahidi kupeleka vitendea kazi

  Source: HabariLeo | Mgomo wa madaktari haukuongeza vifo
   
 2. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,019
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  kumbe arusha kulikuwa na mgomo?
  Nina wasiwasi na hii taarifa.
  Je kamati ya bunge ya huduma za jamii iligundua nini?kwa sababu ilitamka hali ni mbaya sana pale muhimbili.
   
 3. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Katika Hospitali za serikali wagonjwa wengi walihamishwa, hivyo serikali haiwezi ona ongezeko kubwa. Wengi walijifia majumbani kwa kutegemea kupata huduma na ushauri toka wauguzi wasaidizi (manesi) tunaoishi nao mitaani.
   
 4. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Ubongo wa huyu mama Nkya umeshakuwa na makorongo kama uwanja wa kia
   
 5. Mtoto Wa Mbale

  Mtoto Wa Mbale JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2012
  Joined: May 15, 2011
  Messages: 458
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nilimsikiliza Dr.Nkya kwa makini sana, niliishia kujiuliza kama hiyo taaluma ya U-Dr inamsaidia au imempumbaza.

  Ina maana alishindwa kuelewa kuwa idadi ya vifo vilivyoripotiwa katika takwimu za Muhimbili kwa vyovyote ingekuwa ndogo wakati wa mgomo kutokana na wagonjwa wengi kuondoka hospitali? Ina maana alikuwa hafuatilii taarifa za watu kuhamishiwa hospitali binafsi? In maana hajui kuwa wapo waliofia majumbani kwa kukosa huduma mahospitali?

  Kama kawaida serikali hutoa majibu mepesi kwa masuala nyeti. Sishangai, Rais Muongo, Waziri Mkuu Muongo, Mawaziri wengine waongo, Manaibu waziri Waongo; kila aliyeko katika serikali ya ccm ni muongo. Wakumbuke njia ya muongo ni fupi, wanaumbuka sasa.
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,817
  Likes Received: 10,107
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli basi hatuhitaji kuwa na waganga maaana wakifika tu hosp watapona wenyewe bila dokta
   
 7. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Ni mambo ya ajabu lakini hutokea Duniani ambapo watawala wanakua wamejitenga na watawaliwa kimawazo na kimatendo. Ilitokea Ufaransa ambapo malikia aliwataka wasio na chakula kwa kukosa mkate wale keki. Wakati watu wengi wakipoteza maisha kwakutopokelewa hospitali anachkua takwimu za siku hizo na kulinganisha na siku ambazo maelfu ya watu walipokelewa hospitali. Niliwahi kuambiwa kwamba kuna uongo na kuna takwimu. Hapa kwa matamko ya waziri tena daktari kwa taaluma nauna uongo kwa kutumia takwimu. Naamini ilibidi atumie takwimu kuigiribu jamii ya wajinga waliwao kwenye jamii yetu kwasababu yeye binafsi ni sehemu kubwa ya chanzo na asili ya mgomo wenyewe. Aibu tupu na kujidhalilisha mbele ya watu.
   
 8. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  ndo maana tuliwakataa hawa wapuuzi. Mpaka leo anaendele kulidanganya bunge na wabunge wanakubali.
   
 9. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #9
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,351
  Trophy Points: 280
  Yupo mbunge mmoja aliuliza kwanini data ni za muhimbili tuu?Kajitahidi jibu ...kwani jibu simply hapa ni kuwa hawawezi establish idadi kamili.
   
 10. luhala

  luhala JF-Expert Member

  #10
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 25, 2012
  Messages: 412
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Shame to Kikwete, CCM and his government as these lies will go down in history and will be remembered for centuries to come. This woman is a liar, a killer and displays the kind of government we are having - a shameful government full of liars, thieves and the like. Can someone in this rotten government tell the public what happened to the many women who were to deliver by Caesarian section and who could not get the service due to the Doctors strike? And what about that who failed to meet their Doctors appointments in time due to the strike, can they tell us what happened to all these? It is very unfortunate that we Tanzanians have no culture of suing our government and ministries for the misdeeds done to us and the public at large.
  It is apathetic to see the government playing with peoples lives, it has palyed with our country's economy and embezzled, swindled and stole the resources and money intended for the improvement of the common man's welfare, the government is now unable even to pay the small pensions for our retired fathers and mothers, unable even to seat our children on desks and is now dilly dallying with our lives. Is there any justification for those thugs to be left in power come year 2015?

   
 11. tikatika

  tikatika JF-Expert Member

  #11
  Apr 12, 2012
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 1,669
  Likes Received: 2,198
  Trophy Points: 280
  ninaposoma kauli za viongoz naona matusi matupu kwa watanzania!
  Watafieje hospital wakat zimefungwa?
  Kwan kuna time kuchunguza mitaan ni wangap wamekufa?
  Kama idadi wakat doctors wapo iko juu kweli inaweza kupungua wakat hawapo?
  Basi haina haha kuwa na hospital!
  balaza lots la mawazir ng'ombe kabisa!
  Maana akija mkulo atakwambia uchumi umepanda mnoooo huku raia Mia kupata tabu.
  Ngeleja mgao ni history kwa sasa ! !!!!!!
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Apr 12, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Halafu Eti Nikipende Chama anachotoka huyu Mama LoL My Foot
   
 13. M

  Msendekwa JF-Expert Member

  #13
  Apr 12, 2012
  Joined: Mar 11, 2012
  Messages: 440
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kumbe mgomo ht haukuwa na madhara.
  Sasa ilikuwaje Pinda awachimbe mkwara warudi kazini wkt mchango wao ni negligible?
  Ilikuwaje govt ikimbilie Kortini kuzuia mgomo wa 2?
  Ilikuwaje Rais awaite viongozi wa Madaktari ikulu na kuwasihi wasimuumbue km mgomo wenyewe ht haukuwa tishio?
   
 14. M

  MONTESQUIEU JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 847
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mh kila kitu wanafanya siasa.

  Huyu mama atakuwa si mzima kabaisa!
   
 15. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Usichukie chama kaka kwa kutoridhishwa kwako na mtu mmoja! CCM ina sera nzuri sema tatizo kuwa watendaji wasiozidi 1% sio watendaji wazuri.
  Tujitahidi kuwarekebisha mkuu! sio kwa jazba.
   
 16. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Serekali hii jamani inasikitisha. Mama wa rafiki yangu hapa ofisini kwetu alifariki kwa kukosa matibabu na kupigwa danadana kipindi cha mgomo leo Nkya anasema vifo havikutokea kwa sababu ya mgomo! Amefanya utafiti gani? Na huo utafiti aliutumiaje? Kwani watu wote wanaokufa wanafia hospitalini?
   
 17. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwanza pole kwa msiba, usimlaumu Waziri haoteshwi isipokuwa natoa taarifa kulingana na jinsi alivyopokea kutoka kwa watendaji wake.
   
 18. g

  gabi Member

  #18
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  chagueni chadema huenda wao hakajitahidi kuyafanya yale mnayotaka, lakini kumbukeni yeyote aingiae madarakani hatowaridhisha kwa kila jambo coz mengine yanakuwa njee ya uwezo wake na wa tz tuwe na mshikamano kama vile kenya wafanyavyo, sukari ikipanda wanaingia barabarani lakini kwetu tunabaki kulalamikia humu tu nani ajitoe muhanga? na virungu, maji washa, bunduki, mabomu ya machozi ya IGP nani anayataka?
   
 19. g

  gabi Member

  #19
  Apr 12, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo si Nkya bali anaelekezwa cha kufanya na mkulu wake ndio kawaida yao. Mungu atende miujiza tu
   
 20. popiexo

  popiexo JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 743
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sera za chama ndio zinazokumbatia hao watendaji wabovu. Ingekuwa chama makini kingeisha watimua wajingawajinga wote.
   
Loading...