MGOMO WA MADAKATI BMC: DR GILYOMA asema WAGONJWA WALOKOSA HUDUMA MUHIMBILI WAJE BUGANDO

tonnyalmeida

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
226
46
Katika hali ya kushangaza imesikika katika vyombo vya habari daktari mmoja wa bugando aliyetajwa kwa jina la Dr Gilyoma amesikika akisema eti wagonjwa walokosa huduma katika hospitali ya Muhumbili waje Bugando kwa sababu kunahuduma wakati huduma tangu jana zimesitishwa tangu jana na wametoa matangazo hata humu JF tumeyaona na taarifa za ndani znasema mgomo unaendelea.

Huyu Dr Gilyoma ni nani? wadau mnaomjua mtujuze tafadhali.
Na anafanya haya ili iweje?


NAOMBA KUWASILISHA.
 
Labda hukumuelewa vizuri, ni sis walalahoi tusiothaminiwa na hii serikali yetu, ama ni hawa wenzetu wanaambiwa waende BUGANDO kupata Referal ya kwenda APOLO India. Hebu msikilize tena vizuri.
 
yani wagonjwa watoke MNH, waende Bugando?
Kwa nini wao wapo wengi, si waje MNH?

ukenge mwingine tabu kweli!!
 
gilyoma ni director wa clinical services bugando. ki profession ni ENT surgeon, na kwa sasa anakaimu u director wa hospitali kwa kuwa director wa hosp hayupo nafkiri atakuwa amekwenda dar kwenye kamati ya majadiliano/usuluhishi. nafikiri hizi zitakuwa ni propaganda za serikali kuwapoza wananchi kwa kuwa jana gari la mkuu wa mkoa lilionekana ndani ya hospitali. madaktari wameendelea na mgomo
 
mwanza??? kwa flight (300k +) mhh hizo gharama za kwenda si nisawa nakupata matibabu TMJ,DAR GROUP , plus other private hospital, they cant afford, au mabasi ya Rzzzzzz yatawapeleka bure???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom