Mgomo wa daladala Morogoro: Mkuu wa Mkoa&Mkurugenzi wawajibishwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa daladala Morogoro: Mkuu wa Mkoa&Mkurugenzi wawajibishwe

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MWananyati, May 21, 2011.

 1. M

  MWananyati Senior Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 155
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Inasikitisha sana kuona serikali yetu imeshindwa kutatua suala la mgomo wa daladala mkoani Morogoro. Ni siku tatu tangu huduma hio muhimu katika ujenzi wa taifa ilipositishwa kwa madai ya kuwa kumekua na ukuikaji mkubwa wa makubaliano ya makusanyo ya mapato kwa daladala stendi kuu-mjini kuelekea sehemu zingine za manispaa. Ilikubali kuwa kwa siku kila daladala itakua inalipa shilingi mia tano (500) tu, kama ushuru hapo stendi. Lakini serikali kwa kupitia kampuni ya ukusanyaji mapato imeamua kutoza shilingi mia tatu (300) kwa kila trip ambayo gari linatoka stendi hio. Hii inamaanisha kila ukiingia hapo stendi unalipa sh.300 ambapo kwa siku waweza lipia zaidi ya sh 2000.

  Inasemekana kuwa suala hili limetiliwa ngumu na mkuu wa mkoa pamoja na mkurugenzi wa manispaa ambao wanataka malipo sasa yawe 2000 kwa siku. Hio ya mia tano hawataki kuisikia kabisa.

  • Mkuu wa mkoa na mkurugenzi wake watambue kuwa wanaoumia kwa kadhaa hii sio wao wala wake/waume zao, watoto au ndugu zao ambao hutumia magari ya serikali ambayo hutunzwa kwa fedha yetu ya kodi. Wala sio wenye daladala, ni wananchi wa kawaida tena wengine wagonjwa
  • Iweje mikoa yote ya tanzania ushuru uwe mia tano (500) na morogoro iwe zaidi ya hapo? morogoro kuna faida kubwa ambayo labda hawa wakubwa wanaifahamu? kuna mgogoro ama wa maslahi binafsi kwa mkuu wa mkoa na mkurugenzi
  • Mkuu wa mkoa na mkurugenzi watambue kuwa vifo vyote na majeruhi wote waliopatikana kipindi hiki cha mgomo kwa ajili ya kutumia pikipiki aka bodaboda, damu yao ipo juu ya vichwa vyao na familia zao m/mkoa na mkurugenzi
  • Kama ni njia ya kurudisha pesa kutokana na matumizi mabaya ya ofisi au kama ni agizo la Mkullo, tafadhali waache mara moja. Budget deficit haiwezi kufidiwa ndani ya mwezi huu mmoja uliobaki
  serikali kuu ipo wapi? mnauza tu dowans huko wakati wananchi wanahangaishwa na uongozi mmbovu wa mkuu wa mkoa na mkurugenzi wake. Ina maana ofisi husika ie usafirishaji, waziri mkuu, ikulu hamjasikia hii tabu tunayopata wakazi wa morogoro? au mlikua pamoja na CDM huko nyanda za juu?
  raisi ingilia kati huko uliko, tunataabika au mpaka tufanye maandamano ndo mtajua shida tuliyonayo?
   
Loading...