Mgomo wa daladala morogoro mjini leo umeingia siku ya tatu mfululizo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo wa daladala morogoro mjini leo umeingia siku ya tatu mfululizo.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kituro, May 21, 2011.

 1. k

  kituro Senior Member

  #1
  May 21, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 176
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  leo ni siku ya tatu tokea mgomo wa daladala uanze mjini morogoro. watu wamekuwa wakitumia usafiri wa tax na pikipiki zijulikanazo kama bodaboda kama njia mbadala kutatua tatizo hilo ambalo kwa ujumla imekuwa ghali sana hasa kwa wafanyakazi wa kima cha chini pamoja na wanafunzi. ingawa baadhi ya maeneo mbunge wa morogoro pamoja na wafanyabiashara wengine wawili wamejitolea mabasi yao kusafirisha watu bure, wafanyabiashara hao ni mbunge wa morogoro mjini (ccm) Abood, Hood na watatu simkumbiki jina lake. pamoja na msaada huo lakini tatizo ni kubwa kwasababu mabasi hayo yakienda kule yanakokuwa yamepangiwa, huchukua zaidi ya masaa mawili kurudi tena, hivyo watu wanapanda mabasi hayo kama ikitokea ukilikuta ndiyo unapanda lakini kulisubiri inakuwa vigumu. ndugu zangu hiyo ndiyo hali halisi inayowakumba wananchi wa morogoro!
   
 2. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,060
  Likes Received: 3,089
  Trophy Points: 280
  Wapewa wanayoyadai...
   
 3. b

  binti ashura Senior Member

  #3
  May 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  leo umeingia siku ya nne sijui utaisha lini!, poleni sana wananchi wa morogoro!.
   
 4. b

  binti ashura Senior Member

  #4
  May 22, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  wale wanaotarajia kununua daladala mmeiona hiyo?
   
Loading...