Jackson Turary
Senior Member
- Jan 1, 2014
- 154
- 129
Hilo ndo tatizo la wanyonge wanavurugwa vurugwa kama maandazi kikangoni,Watendaji na wapangaji wa haya mambo sijui huwa wanafikiria vitu gani au kwa sababu wao hawatumii huu usafiri wa uma ndio maana hawazingatii athari kwa walaji.
Pale kivukoni ndio center kubwa ambayo watu kutoka viunga vyote vya kigamboni huletwa na mabasi kisha baada ya hapo wavuke kwenda mjini au wapande hizo machinga kupitia darajani, sasa leo unapohamisha basi za machinga na kuzipeleka ndani ya mji wakati bado kituo kikuu cha hizi basi nyingine kinabaki kuwa kivukoni hapo unakua unawalazimisha abiria wanaotaka kuvuka kupitia darajani wapande bajaj (Tsh 500) ili kuzifata hizo machinga huko Tungi na baadae alipe tena kiasi hicho hicho anapokua anarudi.
Kwa mtu wa kipato cha chini nyongeza hii ktk gharama ya usafiri ni kubwa, mamlaka husika inabidi walitazame vizuri ili maboresho wanayofanya yasiumize watumiaji wa huduma husika.