Mgomo wa amani DIT- Dar es Salaam Institute of Technology. june 2 2014

Jerick06

Member
May 2, 2014
51
15
Serikali ya wanafunzi DIT kushinikiza uongozi wa chuo kufutilia mbali swala la wenzao kutokufanya mitihani ya kumaliza mwaka wa masomo.
Hii imetokana na wanafunzi takribani 620 kutoruhusiwa kufanya mitihani iyo. Kesho tarehe 2 june katika viwanja vyaa michezo DIT saa moja asubuhi kutakuwa na mgomo huo wa amani. Je swala la kufungiwa wanafuzi kwasiokamilisha ada ni sawa?
 
vijana mkimaliza exams...mkirudi mtaaani muhakikishe ccm inaondoka...
 
Hivi Profesa Kondoro bado ndo mkuu wa chuo hapo? kama bado ni yeye, sishangai.
 
Serikali ya wanafunzi DIT kushinikiza uongozi wa chuo kufutilia mbali swala la wenzao kutokufanya mitihani ya kumaliza mwaka wa masomo.
Hii imetokana na wanafunzi takribani 620 kutoruhusiwa kufanya mitihani iyo. Kesho tarehe 2 june katika viwanja vyaa michezo DIT saa moja asubuhi kutakuwa na mgomo huo wa amani. Je swala la kufungiwa wanafuzi kwasiokamilisha ada ni sawa?

Lete mrejesho wa kutafuta haki yenu ya kusoma na kufanya exams kama rais wa nchi alivyosema mwanafunz afanye mtiani lakin matokeo yake asipewe mpaka alipe ada, lakin sasa ni kinyume chake.
 
hali bado ni ya kinagaubaga, Wakubwa wa chuo bado wapo katika kikao ili kutoa muafaka. ntawajulisha katika maamuzi yao
 
Jamani!!! Haihitaji uprofesa waruhusiwe wafanye mitihani kisha wataangaliwa kwa kila mmoja uwezo wake wa kulipia hiyo ada. isiwe kwa pamoja wazazi tunatofautiana mno na wengine ni watoto wenyewe wanajilipia. wakimaliza watafanya vibarua watakomboa vyeti vyao
 
Wangetumia busara na hekima kuwaruhusu wafanye mitihani then matokeo mpaka watakapolipa ada. Haiitaji uwe na uprofesa kufanya hivi
 
Mpaka sasa, Mitihani imeamliwa kuendelea kwa mujibu wa kikao cha bodi ya chuo lakini bhado awajaelewana na serikali ya wanafunzi DITSO. mitihani itafanywa chini ya ulinzi mkali kuanzia saa nane hapohapo wanafunzi bado wanagoma kutokufanyika mitihan iyo mpaka wale wasiolipa waruhusiwe kufanya pia. hali tete
 
Hao ambao hawajalipa ada wanazingua elimu sio bure walipe ada wafanye mitihani msoto kiyaa unawasubiri
 
Mpaka dakika hii mgomo unaoendelea chuo cha DIT kushinikiza wanafunzi ambao hawajakamilisha ada kufanya mtihani ila matokeo yao ndo yashikiliwe bado hujatatuliwa na wanachuo wameamua kufanya maandamano kesho

nitaendelea kutoa taarifa kwa yatayojiri
 
Hiyo mbona iko wazi kabisa duniani kote..watu wanafanya mtihani unazuia matokeo...sijui wabongo zile akili zetu za kufikiria mambo ya kawaida kabisa tunazipeleka wapi..?!
 
Niliruhusiwa kufanya mtihani miaka hiyo, matokeo na cheti kilizuiliwa. Kwangu mimi ilikuwa adhabu ya wastani kabisa mambo yalipokaa sawa nilienda kulipa bakaa na sasa mambo yako poa sana. Wawe considerate tu, maana hao vijana wazazi wao wangekuwa ni wajumbe wa BMK ilikuwa ni ten days job na ada yote kwishaaaaaaa.
 
acheni mambo ya kijinga ya kugoma madogo , hamtafika popote . ingieni darasani mpige shule nyie
 
acheni mambo ya kijinga
ya kugoma madogo , hamtafika popote . ingieni darasani mpige shule
nyie

acha uboya ww,, unaona raha watu zaidi ya mia sita kufutwa chuo coz sheria ni usipofanya UE umedisco automatically,, assume ww uko kwny hilo kundi la watu mia sita af wenzio wafanye mitihani..... pu..mb...u kabisa!
 
Back
Top Bottom