Mgomo Umemalizika Rasmi!. Jee Bado Kuna Umuhimu Rais Kukutana na Wazee wa Darisalama?!. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo Umemalizika Rasmi!. Jee Bado Kuna Umuhimu Rais Kukutana na Wazee wa Darisalama?!.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Mar 10, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  JK ilikuwa akutane na Wazee wa Darisalama siku ya Ijumaa ili kutoa msimamo wake juu ya mgomo wa Madaktari!.
  Ijumaa hiyo akaamua kabla hajatoa msimamo, akatumia busara kuwasikiliza hao madaktari, yeye mwenyewe kwa masikioo yake, licha ya taarifa zote alizoletewa na wasaidizi wake na vyombo vyake!. Hivyo akaahirisha kukutana na wazee mpaka Jumatatu, ili kutoa fursa ya mawasiliano zaidi.

  Badda ya kuahirishwa ule mkutano wa jana, nilisema hivi
  Leo Chama cha Madaktari MAT, kimekutana na kutoa tamko la kuumaliza mgomo wao unconditional!.

  Sasa baada ya mgomo huu kumalizika rasmi, jee bado kuna haja ya JK kukutana na Wazee wa Darisalama?.

  Mkumbuke taarifa ya madaktari, haukusema, waliongea na rais Ikulu, na hakuna taarifa ya Ikulu kueleza wamekubaliana nini na madaktari, bali ni MAT, ndio wametoa taarifa ya kuumaliza rasmi mgomo huo!. Kwa vile sasa mgomo umeisha, bado kuna haja ya kuendelea kuuzungumzia mgomo huu?.

  Ningekuwa mshauri wa JK, ningemshauri hata hiyo Jumatatu, asizungumze na Wazee wa Darisalama, unless alikuwa na mengine ya kuongea nao na sio lazima lihusu huo mgomo wa madaktari!.

  Maadam ameonana na madaktari, walichozungumza wanakijua wenyewe, na baadae madaktari wametoa taarifa kusitisha mgomo unconditional, nadhani sasa ni busara, tusiendelee kuuzungumzia mgomo huu ili kuepusha kumtafuta mshindi na mshindwa!.

  Uamuzi wa madaktari kusitisha mgomo ni uamuzi wa busara unaopaswa kuungwa mkono na wote wenye mapenzi mema na nchi yetu!. Pia tuchukue fursa hii kuleta umoja na mshikamano, yale makundi yote tuliohasimiana kutokana na mgomo huu kwa baadhi ya wenzetu kuwaunga mkono madaktari na wengine tukipinga, sasa mgomo umeisha, tuwe wamoja tusonge mbele kwa maslahi ya taifa!.

  Wasalaam

  Pasco.
   
 2. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #2
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  unconditional kivipi mkuu? Unaweza ukatufafanulia labda...!
   
 3. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #3
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  taarifa rasmi ya MAT tunaitaka hapa kwanza
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Sweke, walipolianzisha tena, walitoa masharti lazima kibarua cha waziri na naibu wake kiote ndipo warejee kazini. Leo wamekubali kuumaliza rasmi mgomo wao bila masharti yoyote!
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Afadhali madokta wamemaliza huo mgomo wao. Nilijua tu yaani JK ashiriki kumaliza migogoro ya Kenya na Zanzibar pamoja na ule ww Mauritania wakati akiwa Mwenyekiti wa AU halafu leo ashindwe kumaliza mgogoro wa madaktari. Ilikuwa haiingii akilini.

  Mgomo umeisha, madokta fanyeni kazi kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya.

  Ni muhimu Rais akutane na wazee aongelee sakata zima la mgomo hadi alipoingilia jana na kuumaliza kidiplomasia.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Watanzania bwana mbwembwe nyingi ohooo, Jk atakiona na mengine kibao, sasa mnaenedelea na hayo hayo ili iweje. Jk ni rais wa watu bwana mnatapa tapa tu.
   
 7. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #7
  Mar 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Blue siyo conditions? Tafadhali sana uwe na kiwango cha kusema ukweli
   
 8. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco,
  Rais JK kama umemsoma ni mtu asiependa migogoro ebu angalia kundi lolote linalokwenda Ikulu kwa ajili ya mazungumzo uwa linarudi na majibu ya kukubaliana na JK.

  Watu wengi walikuwa wanategemea na kutaka waone JK kawafukuza kazi Madaktari wetu, ili mgogoro uwe mkubwa na usambae.

  Bahati mbaya au nzuri JK ni msikivu na mvumilivu ana akili za kesho, hujui kwa nini kabadilisha ratiba yake kabla ya kuongea na Taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam, kaongea kwanza na Madaktari na kutatua mgogoro kwa amani.

  Kuongea na Wazee Jumatatu JK hatakuja kivingine kabisa na hotuba ya huruma kwa Watanzania.

  Pamoja kuwa JK baadhi ya vitu kashindwa kufanya kama rais lakini kwenye mazungumzo ya kutatua migogoro JK siku zote anafanikiwa kuwashawishi wapinzani wake wakubaliane nae.
   
 9. Kivumah

  Kivumah JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 7, 2008
  Messages: 2,413
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  ..Huwa najiuliza hivi pale Ikulu kuna nini, "nna mashaka pale Getini kuna kitu kimewekwa ukiingia tu kutaka kuonana na Baba Riz unalainika". Walianza Chadema na issue ya Katiba wakalainika, leo hii na Madaktari wamelainika.
  Kuna nini Ikulu.
   
 10. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  hapo kwenye masharti yeyote nadhani ndiyo upatazame vizuri. Conditions zile bado zipo ila wamerudi kazini baada ya kuahidiwa hizo conditions zitashughulikiwa...!
   
 11. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Bravo mzee wa negotiation bwana JK

  Bravo doctors...
   
 12. O

  Ogah JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Ukishakubali kuingia pale........na wewe in a way unageuka (kisaikolojia) kuwa kama mmoja wao.........

  Nilishawaambia hawa madakta wetu............maneno yao ya kipuuzi eti wanataka Mawaziri wajiuzulu they were UTTERLY NONSENSE.........kama kuna mtu mpumbavu aliwashauri kusema hayo basi na wao siju tuwaweke kwenye kundi gani...........
   
 13. s

  sweke 34 JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2012
  Joined: Jan 29, 2012
  Messages: 694
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hapa umenena vyema ila si kila mara anafanikiwa kuwashawishi wapinzani wake...kuna wakati huwa hata hawasilikilizi.
  Ni kweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni...!
   
 14. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  There are times when children want to hear the voice of their father....
   
 15. O

  Ogah JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  It has been long overdue kubadilisha/kuli-amend baraza la mawaziri..........however the changes to baraza la mawaziri tuwaachie JK na Waziri wake Mkuu at their own pace that suits them...........na sio kutokana na ultimatum ya kipuuzi kutoka kwa madaktari........
   
 16. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Wamerudi bila madai yao mapya ya Mponda na Nkya kuwachishwa kazi, walisema hawarudi kazini mpaka hao waachishwe kazi. Kwa hiyo wamerudi "unconditional".
   
 17. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #17
  Mar 10, 2012
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Waandishi wa habari wawe na uelewa wa kutosha.
   
 18. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Upuuzi ni huu ulioandika wewe na huu wanaofanya kikwete na pinda. Ni nini kiliwanyima kufanya hiki alichofanya jana kabla hata ule mgomo wa kwanza haujatokea. naamini ni kweli IQ ya mwafrika haitilafiani sana na ya nyani. Mtu unaacha kidonda kigeuke kidonda ndugu kwa kukataa matibabu halafu baadae unapokubali mguu ukwatwe unapongezwa? Elimu inatusaidiaje waafrika? Mtu kama wewe ogah bila shaka umesoma angalau f 4 lakini mbona unatenda kufikiri kama kima? angalia unasema madiliko ya baraza waachiwe wafanya kipindi wanachotaka na kwa muda unaowafaa wao.... sio wananchi wote..... comments za aina hii zinatolewa na na wajinga wasiojua n nini maana ya kutawala.....
   
 19. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,593
  Likes Received: 18,589
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mimibaba, niendeshe na darasa la conditions?. Hiyo kwako ndio condition?. Walipogoma si waliweka masharti, kuwa hawarudi kazini mpaka Dr. Mponda na Dr. Nkya wang'olewe?. Jee tangazo lao la kumaliza mgomo lina masharti?., jee wameweka sharti lolote lazima litekelezwe ndipo warejee kazini?. Baada tuu ya kuongea na JK wamekubali kumaliza mgomo na kurejea kazini!. Hakuna sharti lolote lililowekwa, wanarejea kazini unconditional!.
   
 20. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2012
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  hivi ubongo wako unajaza kizibo cha bia kweli? sidhani
   
Loading...