Mgomo ujao: Utakuwa si wa watumishi wa umma... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mgomo ujao: Utakuwa si wa watumishi wa umma...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Aug 2, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,378
  Trophy Points: 280
  Migomo ya watumishi wa umma ni rahisi sana kuilazimisha kusimamishwa. Na ni rahisi kwa vile watumishi hao hulipwa moja kwa moja na serikali na hutawaliwa na sheria na taratibu za kiserikali. Tumeliona hili kwenye mgomo wa madaktari na sasa kwenye mgomo wa walimu. Nikiangalia na kutambua kuwa hakuna kitu cha msingi ambacho serikali imeweza kukibadilisha zaidi ya kutumia nguvu (ya mahakama na vinginevyo) kuzuia migomo hii mikubwa naweza kuona kuwa utakapotokea mgomo wa wasio kwenye utumishi wa umma basi utakuwa ni mgogoro mkubwa zaidi na wenye usumbufu mkubwa zaidi kwa wananchi.

  Itakuwaje kama watakaogoma huko mbeleni ni wale ambao hawasimamiwi na utaratibu wa utumishi wa umma? Mahakama itaweza kutumika vipi kuwarudisha "kazini"?
   
 2. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Muumba atuepushe na hilo maaana..........may be risasi
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nakumbuka wafanyakazi wa benki NBC waliwahi kutaka kugoma huko nyuma lakini serikali ikaenda mahakamani kuzuia mgomo, hata wafanyakazi wa sekta binafsi serikali inaweza kuingilia kati na kwa woga wetu watanzania tukatii. Inabidi tusimame kidete kutetea haki zinazoporwa na serikali kupitia mahakama kwani migomo duniani kote ni haki kwa mfanyakazi na imehalalishwa.
   
 4. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kama kina nani hao wasio watumishi wa umma? Wanajeshi? madereva wa teksi? au wauza magenge?
   
 5. Neiwa

  Neiwa JF-Expert Member

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 730
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Precarious line of thought.. Hata hivo bado we have a long way to go. Observe sana katika jamii yetu, watu ambao wanalalamika na kutaka kusimamia haki out of "Uzalendo" ni adimu ukifananisha na wale ambao wanalalamika tokana na njaa ama kutokuwa ma mahitaji ya kutosheleza mahitaji yao (a.k.a njaa). Mara nyingi huwezi kuta aliejitosheleza kifwedha akawa ni mlalamishi dhidi ya matatizo ndani ya jamii...

  WaTanzania tuna asili ya woga, unafiki, selfishness na lack of guts hasa ukiwa in the face ya mtu ambae anakusababishia hayo matatizo; na hasa kama huyo mtu is powerful hasa material-wise. Naamin kabisa kuna members hapa JF na wanaharakati wazuri sana na wana mawazo mazuri sana ila wakibahatika kuwa in the presence the the so called wahalifu/mafisadi ama wanyonyaji hata hakumbuki lawama zile kuweza zifikisha.
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Watumishi wasio wa umma sehemu kubwa wanalipwa vzuri angalau sitegemei umoja wa mgomo kutoka kwao,,labda na tuanze kuainisha wwatumishi hawa wasio wa umma,wasiofungamana na serikali moja kwa moja ni wepi
   
 7. sembuli

  sembuli JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 762
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  tatizo serikali imepewa nguvu sana katika katiba mimi nashauri tuanze na katiba kuipora serikali haya mamlaka ya kibabe: tumeona mgomo wa daladala arusha serikali kupitia sumatra ikatishia kupora leseni za biashara!
  dawa ni kuigomea katika karatasi ya kura
   
 8. O

  OLEWAO Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  MM,
  Uteuzi wa JM wa Tanzania ulizua maswali mengi yaliyokosa majibu (maelezo). Kumbe ilikuwa ni maandalizi ya kujikinga dhidi ya harakati za watu wa Mungu kudai haki zetu. Atakachofanya kama kutatokea mgomo wa wasio watumishi wa serikali ni kumtumia JM ambaye atatoa tamko kuwa MGOMO HUO NI BATILI KWA KUWA UMEVUNJA KATIBA YA NCHI.
  Baada ya hapo watawaagiza FFU na wanajeshi kuwashughulikia wale wote watakaokaidi agizo la mahakama.
   
 9. M

  Memory Senior Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Kuna mtu anahoji nguvu ya waajiriwa wasio wa Serikali ni akina nani? he must be empty headed...jana tu Bulyanhulu wameshitua siku moja. Vice President wa Barrick duniani katinga Tanzania...!! i can zoom to see what next.
   
 10. Bongo Pix Blog

  Bongo Pix Blog JF-Expert Member

  #10
  Aug 2, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 213
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MM,
  Mi naona twaatamia time bomb, kwa kufuga mamigomo haya, siku moja atapatikana fundi, ataunganisha nyaya mamigomo, mamigogoro yooote na kisha kuelekeza utambi kwa kibatari, cjui nini kitatokea, kule Tunisia mmachinga ndo aliunganisha nyaya.
   
 11. L

  Laizer Ole Naibio Member

  #11
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Madereva na makonda wa daladala ndio tu wanaweza kugoma fo real.
   
 12. B

  Bigman 2012 Member

  #12
  Aug 2, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo virungu ni lazima vitumike FFU wanapend sifa haooooooooooooooooooooooo!
   
Loading...