Tetesi: Mgomo mkubwa wa madereva wanukia, wasafiri jiandaeni

falcon mombasa

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
9,158
9,239
Wakuu habari

Habari za kuaminika za kutoka chanzo changu ninachokiamini kabisa zinanitaarifu niwaambie wale wanaotaka kusafiri siku hizi za karibuni wajiandae haswa

Madereva wote wa mabus wa Tanzania nzima kwa umoja wao wameadhimia kugoma kutoa huduma hiyo muda wowote kuanzia sasa (hapa sitasema siku)

Lengo kubwa la mgomo huu ni kutokana na kauli tata zinazopishana zinazotolewa na vyombo vinavyosimamia usalama wa barabarani,ambapo baadhi ya kauli ya viongozi wa usalama zimekuwa zikipishana kila kukicha

siku chache zilizopita alisikika afisa mmoja mkubwa wa jeshi la polis kitengk cha usalama barabarani akitumia vyombo vya habari akiweka katazo kuwa gari halitakiwi kusimama kwenye zebra endapo hakuna mtu bali lipunguze mwendo tu na ukisimama bila kuwepo mtu kwenye kivuko utakuwa umetenda kosa na utawajibishwa

Afisa wa pili mwingine wa juu kabisa alitumia vyombo vya habari kuwaonya madereva wasiosimama kwenye zebra hata kama hakuna mtu.Jambo lilozua utata mkubwa kwani madereva hawajui wafuate kauli ipi

kauli iliyoleta hasira zaidi ni hivi juzi ambapo kiongozi mwingine alinukuliwa akisema "madereva wanapaswa kuogopa kama shetani au kama simba"

Hayo ni baadhi yatakayopelekea kuanza mgomo huu mkubwa kabisa licha ya kuwa yapo mengi pamoja na yale ya kukosekana alama za barabarani na ubovu wa barabara huku lawama zote zikielekezwa kwa madereva pindi ajali zinapotokea

Narudia tena wasafiri wajiandae kisaikolojia
 
Polisi walishasema sheria haimuelekezi dereva kusimama katika zebra kama hakuna mtu.
Hata control room ukiwapigia kwa namba kwa namba za katika stika ya usalama barabarani wataeleza hivyo.
Mgomo labda utokane na kanuni mpya za usalama barabarani.
 
Back
Top Bottom