Mgomo baridi ticts.

Zero One Two

JF-Expert Member
Sep 16, 2007
9,347
3,020
Kuna mgomo baridi unaendelea bandarini kitengo cha container tangu tarehe 05/08/08.
Jamaa hawalipwi mishahara mizuri,pia kuna ufisadi wa manunuzi ya crane mbovu.
 
Madhara ya mgomo huo yanakula upande wa Karamagi au yanakula upande wao (wagomaji)?
 
Maana yake mgomo huo unakula kwetu Watz,kama mgomo huo utachangia kupatikana kwa suluhu au marekebisho fulani basi hao jamaa zetu wakaze buti ila wasisahau wasaliti na ndumila kuwili hawatakosa ktk kundi lao.
 
Walinyimwa bonasi ya mwezi July. Huwa wanalipwa a peanut of Shs. 70 elfu kwa kufikia/kuvuka malengo. Effect ya mgomo ipo. Meli zimeshaanza ku-foleni bandarini.

Swali ni kuwa, tunao leaders wa kuendesha na kuongoza migomo?

Waalimu wametishia jana. TUCTA wameahirisha wa kwao........
 
[I said:
malila;264068]Makubaliano ya kulipana bonus mkivuka lengo yako kwa maandishi?
[/I]

Mikataba ya ajira pale TICTS ni ya ujanja ujanja tu. Mfano, Contract ni za miaka miwili lakini ikiisha hulipwi kitu. Unaongezewa miwili tena.

Salaries wanazolipwa ni ndogo kuliko za huko ambapo Hutchson wanaendesha bandari zingine. Hata mishahara ya TPA - walikotoka wafanyakazi wa TICTS - ni mikubwa kuliko yao.
 
Kwa hiyo jamaa zetu hao ajira zao kama kwa mhindi,ktk salary slip mshahara kiduchu lakini jioni unapewa bahasha kiaina.Nawahurumia ndugu zangu,ila wakomae tu,maji wameshayavulia nguo.
 
Hiyo kwa namna moja au nyingine sioni tofauti sana na kuajiriwa kama kibarua maana hawawezi kufanya lolote la ajabu kwenye maisha yao kwa staili hiyo. Kwanini nchi hii imeshikwa sehemu kubwa hivi na wanyonyaji weusi??? ndio maana wana uhusiano mkubwa na akina RA maana ni wanyonyaji wenzao na wanafundishana kunyonya. Pumbaf kabisa, kazeni buti huenda Mungu akaona shida zenu mkakombolewa, hata hivyo msisahau, kuweni makini kufuata sheria mjue kamili pa kuanzia na pa kuishia maana hao ni wezi ambao tayari walishajipanga kuwaibia wakiwa na silaha kamili na kuua ama kujeruhi wanapopingwa. Msikabiliane nao kwa ubishi wa midomo, mtaishia kuvuliwa bukta zenu mkimbizwe mitaani bila nguo usiku.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom